
Rais wa Burundi Pierre Nkuruzinza. Picha imetolewa chini ya leseni ya Creative Commons na World Economic Forum.
Jaribio la Pierre Nkurunziza Rais wa Burundi kujiongezea muhula mwingine wa madaraka lilisababisha maandamano na baadae mapinduzi ya kijeshi mnamo Mei 13, 2015 wakati akiwa kwenye mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Tanzania. Mapinduzi hayo yalimchelewesha kurejea nchini Burundi.
Jumla ya nchi 18 za ki-Afrika hazina ukomo wa mihula ya urais, ingawa utafiti mpya unaonesha kwamba wa-Afrika wengi wanakubaliana na kuwepo kwa ukomo wa mihula ya urais. Kuwepo kwa wanasiasa wanaong'ang'ania madaraka kinyume na matakwa ya wananchi si jambo la kuchekesha tena, ila kicheko kidogo wakati mwingine kinaruhusiwa na daktari.
Mapinduzi yaliyoshindwa nchini Burundi yamesababisha twiti za kuchekesha, hasa kutoka wa-Ganda ambao rais wao wenyewe anasaka uwezekano wa muhula wa tano.
Kemigisa Jacky, mwanafunzi wa uandishi wa habari raia wa Uganda, akirejea madai yanayodaiwa kuwa ya Nkurunziza kwamba Mungu amebariki harakati zake za muhula wa tatu, aliandika:
Lakini nina wasiwasi na kile ambacho Mungu anakuambia sasa hivi Nkurunziza! Labda ni Mungu aliyeruhusu harakati za kugombea muhula wa tatu.#AskNkurunziza
— kemigisa jacky (@JackyKemigisa) May 13, 2015
Lakini nina wasiwasi na kile ambacho Mungu anakuambia sasa hivi Nkurunziza! Labda ni Mungu aliyeruhusu harakati za kugombea muhula wa tatu
Mtumiaji mwingine wa mtandao wa twita MartinAhabwe alimwuliza Nkurunziza:
Any improvement on your Maths chief,which term is it now,1st,2nd or Zero? #AskNkurunziza
— MartinAhabwe (@AhabweMartin) May 13, 2015
Mkuu hesabu zako vipi tena, huu ni muhula wa ngapi sasa, wa kwanza, wa pili au bado hata mmoja?
Wengine walitengeneza alama ishara ya #NkurunzizaPlaylist, ambapo walituma vichwa vya nyimbo kwa ajili ya Nkurunziza.
Video ya YouTube hapa chini iliwekwa kwenye mtandao wa Twita kwa kutumia alama ishara ya #NkurunzizaPlaylist na Mkandamizaji. Hii ilikuwa kabla Nkurunziza hajarudi Burundi kutokea Tanzania kufuatia mapinduzi. Wimbo wenyewe ni ule wa “I Am Coming Home” ulioimbwa na Morgan Heritage:
Allan Ssenyonga, mwalimu na mwandishi wa Uganda, alichagua wimbo wa mwimbaji marehemu wa miondoko ya kufoka foka Tupac Shakur:
It's me against the world – 2Pac (Nkurunziza is on the extreme right) #NkurunzizaPlaylist pic.twitter.com/QK4eKkwkYy
— Allan Ssenyonga (@ssojo81) May 13, 2015
Niko kinyume na ulimwengu wote -2pac (Nkurunziza anaonekana mkono wa kuume)
Mtumiaji wa mtandao wa Twita kutoka Uganda Ellis Ralph alipendekeza wimbo wa Tyrese:
How You Gonna Act Like That – Tyrese #NkurunzizaPlaylist
— Ellis Ralph (@akorabirungi) May 13, 2015
Utafanyaje hivyo – Tyrese
Odokonyero, mwanafunzi wa ufamasia alichagua wimbo wa R.Kelly:
#BurundiCoup #NkurunzizaPlaylist If I Could Turn Back The Hands Of Time | R.Kelly.
— Odokonyero (@OdoKent) May 13, 2015
Kama ningeweza kubadili nyakati – R. Kelly
Elizabeth Paulat, mwandishi wa habari wa kujitegemea aishie Kampala, Uganda, alichagua wimbo wa mtunzi wa nyimbo Mwingereza Imogen Heap:
HA! Amazing #NkurunzizaPlaylist I'll add “Hide and Seek” by Imogen Heap https://t.co/74fnVHxcPd
— Lizabeth Paulat (@LizabethPaulat) May 13, 2015
HA! Inafurahisha!
@mmnjug alichagua ule wa mwimbaji wa Kiingereza Mark Morrisson:
#NkurunzizaPlaylist – Return of the Mack!
— mmnjug™ (@mmnjug) May 15, 2015
Kurudi kwa Mack!
The Royco Guy alihisi Nkurunziza amekwama Tanzania huku na suti moja tu:
When yo stranded in Tanzania and you only got 1 suit pic.twitter.com/8kwaSSYfqX
— The Royco Guy (@Currie_Powder) May 13, 2015
Unapokuwa umekwama Tanzania na una suti moja tu
Akafikiri Hoteli ingemhudumiaje akiwa “Rais wa zamani”:
When the hotel manager in Dar Es Salaam asks you to get out of the VIP room coz it's only reserved for presidents…. pic.twitter.com/D5QKNhZ2NW
— The Royco Guy (@Currie_Powder) May 13, 2015
Meneja wa Hoteli hapo Dar es Salaam akikuomba kuondoka kwenye chumba cha watu maarufu (VIP) kwa sababu chumba hicho kimetengwa kwa ajili ya Marais….
Pamoja na mgogoro unaoitafuna Burundi, kicheko bado ni afya.