Mradi wa Picha Waelezea Maisha Nchini Nepali Baada ya Kutokea kwa Tetemeko la Ardhi

A date none of us will forget, sketched on a wall in Pokhara. The quake spared Pokhara, but aftershocks have hit in the form of cancelled bookings and empty hotel rooms. Photo by @paavan11

Siku ambayo kamwe sote hatutaweza kuisahau, iliyochorwa kwenye ukuta huko Pokhara. The quake spared Pokhara, but aftershocks have hit in the form of cancelled bookings and empty hotel rooms. Picha na @paavan11 kupitia Mradi wa Picha wa Nepal. Imetumiwa kwa rushusa

Kwa muda wa miezi mitatu iliyopita, matetemeko matatu ya ardhi yaliiharibu kabisa nchi ya Nepali. Zaidi ya watu 8,000 wameuawa, mara mbili zaidi ya idadi hii wakiwa majeruhi, watu milioni 2 wakiwa wameachwa bila makazi, na watu wanaokadiriwa kufikia milioni 8 wakisadikiwa kuathiriwa kwa namna moja ama nyingine. (Kwa taarifa zaidi, fuatiliaGlobal Voices ukurasa wa habari maalum .) Mradi wa Picha wa Nepali unafanya kazi ya kukusanya picha za dhoruba hii ya kihistoria.

Mradi huu unamilikiwa na kundi la wapiga picha 10 wanaotoka nje pamoja na wale wa Kathmandu, linaloongozwa na mpiga picha Sumit Dayal na mwandishi Tara Bedi, ambaye alizindua mradi huu siku chache mara baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi la tarehe 25 Aprili. Hadi sasa, mradi huu una zaidi ya wafuatiliaji 61,400 katika Instagram na zaidi ya wafuatiliaji 7,600 kwenye Facebook.

Wakitumia mtindo wa ukusanyaji wa picha kutoka katika maeneo tofauti, wapiga picha katika mradi huu wanasimulia simulizi za maisha ya baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi: uharibifu, uokozi, misaada, ujenzi mpya, pamoja na miale ya matumaini kwa nyakati zijazo.

Umaarufu wa haraka wa mradi huu unatokana haswa na urahisi wake: wachangiaji wanaweka tu kiungo habari katika picha zao na kuandika #nepalphotoproject, na kisha kujumuisha na maelezo kidogo yanayohusiana muktadha wa picha pamoja na wahusika katika picha ile. Wanaoratibu mradi huu wanalenga kuufanya mradi huu kuwa na ufanisi mzuri na ulio ndani ya uwezo wa mtu binafsi.

Makala za hivi karibuni za mradi huu zinaonesha jinsi maisha nchini Nepali yanavyorejea katika hali ya kawaida na namna watu wanavyojiimarisha tena.

Photo by @sachindrarajbansi

Hii ni Manju Gurung. Nilipotaka kumpiga picha, mara zote alijikuta katika kicheko na kisha alikimbia. Yeye na familia yake wamekuwa wakiishi pamoja na familia nyingine mbili katika banda la kuku tangu Aprili 25. angalao ameweza kwenda shule, na sasa anafurahi pamoja na marafiki zake. Aliniambia kuwa, hawasomi, bali hucheza tu na wenzake ili muda uende. Aanategemea kuwa, kuanzia wiki ijayo, masomo yatarejea kama kawaida. Picha na @sachindrarajbansi Kupitia Mradi wa Picha wa Nepal. Imetumiwa kwa ruhusa

Photo by @ujwalgarg0412 Used with permission

Sikrighyang, Nepal. Mann Bahadur akichukua vipimo vya ubao kutoka kwa Bilong kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yake. Bilong, mwenye umri wa miaka 31, kutoka India na ana uzoefu wa kujenga nyumba aina ya bamboo kwa takribani miaka tisa. Pamoja na kutofautiana kwenye lugha ya mawasiliano, wanaelewana vyema na wanashirikiana kwa pamoja kujenga nyumba ya Mann Bahadur ambayo iliharibiwa na tetemeko la ardhi. Picha na @ujwalgarg0412 kupitiai Maradi wa Picha wa Nepal. Imetumiwa kwa ruhusa

Photo by @saagarchhetri Used with permission

Hatimaye, baada ya siku 46 mfululizo za matetemeko, angalao ardhi kwa sasa inatulia. Leo kulikuwa na tetemeko moja la kiwango cha 4.1, mawili yalitokea leo asubuhi, angalao kila baada ya siku mbili. Watu wameanza kuishi maisha yao waliyoyazoea. Kwa sasa watu wanalala kwa amani, hata kuzima taa wakati wa usiku. Magari sasa yanasafiri. Jiji la Kathmandu linarudia hali yake ya kawaida sasa. Picha na @saagarchhetri kupia Mradi wa Picha wa Nepali. Imetumiwa kwa ruhusa

Memories in the rubble. Photo by @sachindrarajbansi Used with permission

Kumbukumbu katika vifusi vya majengo – Nilipokuwa nikitembea katika mji mdogo wa Sankhu uliosheheni vifusi vya majengo, niliiona picha hii. Nilipotaza kwa karibu, niliwaona watu wakiwa wanaota jua. Haya yalikuwa ni matukioa na tabia za watu wa maeneo haya ambayo ungeweza kuyaona katika vitongoji hivi. Nionapo vifusi kila mahali, kwa hakika, picha hii inatukumbusha mbali sana. Kupitia Mradi wa Picha wa Nepali. Picha na @sachindrarajbansi bask

Students of Dibya Jyoti School in Bungamati. Photo by @kishorksg Used with permission

Wanafunzi wa shule ya Dibya Jyoti huko Bungamati inside a makeshift hut prepared by KUArt ‪#‎RebuildingBungamati‬ team. Baadhi ya wanafunzi wanaendelea kujifunza katika shule ya zamani sana na pia jopo linaendela na maandalizi ya utoaji wa hifdhi wa namna hiyo sehemu ya jirani.
Shule nyingi za Nepali zilifunduliwa wiki iliyopita mara baada ya kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi mapema mwezi wa Aprili. Kwa kuwa majengo mengi ya shule bado siyo salama, wanafunzi hujifunzia katika maeneo ya wazi, na maeneo mengine, hata kwenye majengo ambayo ni hatari. Picha na @kishorksg kupitia Mradi wa Picha wa Nepali. Imetumiwa kwa ruhusa

Photo by @kevinkuster Used with permission

Kama vile aliyetolewa kwenye kipande cha filamu ya Steven Speilberg, Nilimuona mvulana huyu akiendesha kitu mfano wa baiskeli alichokiunda yeye mwenyewe kwa kutumia vapande vya miti pamoja na matairi mawili ya chuma, akiwa anapita kwenye vifusi vya majengo ambavyo awali yalikuwa makazi ya jirani zake. Nilimuona akiwa anaendesha kigari hicho cha kuchezea kwenye vifusi na majabali. Picha na @kevinkuster kupitia Mradi wa Nepali wa Picha. Imetumiwa kwa ruhusa

Photo by @sachindrarajbansi

Wakati wa vita kati ya Nepal na Tibet vya kati ya miaka ya 1855 hadi1856, watu wengi sana wa kutoka pande zote mbili walipoteza maisha.mara baada ya vita, wanajeshi wa Haibung walirejea kwenye vijji vyao na kupanda mti huu kama kumbukumbu ya wenzao waliopoteza maisha na kama ishara ya kutubu kufuatia mauaji ya maelfu ya waliokuwa wapinzani wao. Mti huu bado upo pemezoni mwa kata namba 1 ya kijiji cha Haibung. Picha na @sachindrarajbansi imeyumiwa kwa ruhusa

Making a small ‪#‎dharahara‬ at ‪#‎sahidgate‬. Photo by @inspiredmonster Used with permission

Ujenzi wa ‪#‎dharahara‬ ndogo huko ‪#‎sahidgate‬. Wanaume wawili wakijishughulisha kwenye ujenzi wa mnara mdogo wa dharahara kama kumbukumbu ya waliopoteza maisha. Mnara wa Dharahara wa kihistoria iliharibiwa vibaya katika tetemeko la April 25. Picha na @inspiredmonster kupitia Mradi wa Nepali wa Picha. Imetumiwa kwa ruhusa.

Sulochana Maharjan, 16, spins wool in Chapagaon, Nepal. At the time she and her family were sleeping in a tent near their home, uncertain whether their home was safe to stay in after the quake.

Sulochana Maharjan, mwenye umri wa miaka 16, akisokota sufu huko Chapagaon, Nepal. Kwa sasa, yeye pamoja na wanafamilia wenzake wamekuwa wakilala kwenye hema lililo karibu na nyumba yao, wakiwa hawana uhakika kama nyumba yao bado itakuwa na usalama wa kuishi kufuatia tetemeko lililotokea. Wakiwa wamezungukwa na vifusi na waliojawa na huzuni, lakini maisha yanasonga mbele. Picha na @eliegardner kupitia Mradi wa Picha wa Nepali. Imetumiwa kwa ruhusa.

Photo by @prach_is_here

Watu wa Nepali wanafanya kila juhudi ya kujenga upya nchi yao. Hata wasanii wanatumia vipaji vyao kuendesha kampeni pamoja na kukusanya fedha. Hawa ni wasanii wanaohusishwa na kundi la watu mchanganyiko lijulikanalo kama Art Lab lilio na maskani yake huko Kathmandu. Wanatumia kuta za maeneo mbali mbali ya umma katika kusambaza ujumbe matumiaini, amani, kujali na kuhamasisha. Pia, wanatumia nafasi hii kutumia sanaa kama namna ya kuwatuliza wale wanaoweweseka mara baada ya kutokea kwa tetemeko. Picha na @prach_is_here kupitia Mradi wa Nepali wa Picha. Imetumiwa kwa ruhusa

Photo by @mikaness

Sule zimefunguliwa wiki hii nchini ‪#‎Nepal‬i mara baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi la April 25‬. Sule hii inaendelea chini ya kivuli kizuri cha mti wa Kibaniani huko Salyantaar,karibu na Gorkha. Picha na @mikaness kupitia Mradi wa Nepali wa Picha. Imetumiwa kwa ruhusa

Photo by @paavan11

Konstebo wa pilisi na mchezaji wa judo, Pramila Khadka na timu yake wakitoa mafunzo ya elimu ya ulinzi binafsi kwa wanawake na watoto katika kambi moja huko Kathmandu. “Kuishi kambini siyo sawa na kuishi nyumbani, Kuna mengi sana yanayohatarisha maisha yetu. Kwa sasa mwanaume akinichokoza tu, kamwe hatakuwa salama” mshiriki mmoja ananiambia. Shukrani kwa polisi wa Nepali! Kazi yao inafurahisha. Picha na @paavan11 kuptia Mradi wa nepali wa Picha

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.