Abel Wabela: “Kupambana na Hali ya Kutokuchukua Hatua na Kutojali…Hii Ndio Nia Yangu Kama Mwanadamu”

abel_wabela_freezone9bloggers_2

Abel Wabela. Mchoro na Melody Sundberg.

Mnamo mwezi wa Aprili, wanablogu tisa pamoja na waandishi wa habari walikamatwa nchini Ethiopia. Baadhi ya wanaume na wanawake hawa walikuwa wakifanya kazi na Zone9, blogu ya ushirika  iliyokuwa inazungumzia masuala ya kijamii na ya kisiasa nchini Ethiopia ikiwa ni pamoja na kuhamasisha uzingatiaji wa haki za binadamu na uwajibikaji wa serikali. Miongoni mwao, wanablogu wanne walikuwa ni waandishi wa Global Voices. Mapema mwezi Julai, walishitakiwa chini ya tamko la wazi la nchi dhidi ya ugaidi. Wamekuwa gerezani tangu wakati huo na kesi yao hivi karibuni ndio imeanza kusikilizwa.

Makala hii ni ya tatu katika matoleo ya makala zetu za – “Wanayo Majina” – iliyo na madhumuni ya kuwazungumzia wanablogu ambao hadi sasa wapo gerezani. Tunataka kutambua utu wao, tunataka kuelezea habari zao za kipekee na mahususi kabisa. Wiki hii, mwanablogu wa Swideni na msanii, Melody Sundberg aandika kuhusu Abel Wabela, mmoja wa wanakikundi cha Zone9 na msimamizi wa jukwaa la Global Voices’ katika Lugha ya Kihabeshi.

Sikuwahi kufika Ethiopia, lakini nimefuatilia kwa ukaribu kupitia mitandao ya kijamii pamoja na kwenye majadiliano mashitaka ya wanablogu hawa yasiyoisha. Jina ambalo limekuwa likitanjwa mara nyingi ni la Abel Wabela, mwanablogu mwenye umri wa miaka 28, mwandinshi na mtafsiri wa Global Voices. Katika kipindi cha miezi mitatu ya kushikiliwa kwa mwanablogu huyu huko Maekelawi*, Abel alikataa kutia saini hati ya kiapo ambayo ingewaweka hatarini yeye pamoja na wanablogu wenzake. Kufutia kukaa huku, Abel aliteswa isivyo mithilika. Kwa mujibu wa Mradi wa Haki za Binadamu wa Ethiopia (EHRP), Abel alipigwa na mtu kwa kutumia fimbo na mwingine aliichapa miguu yake mara kwa mara kwa kutumia waya wa kuchajia ngamizi. Alilazimishwa kulala sakafuni huku waliokuwa wakimhoji wakimkanyaga mgongoni mwake, kwenye shingo na usoni. Tangu hapo, amekuwa akitumia vifaa vya kumsaidia kusikia kutokana na kusababishiwa tatizo la kiwango cha juu la kutokusikia.

Kwa mujibu wa Endalk Chala, mmoja wa aanzilishi wa kundi hili la ku-blogu, Abel amekuwa akipata tendwa visivyo hata kabla ya kukamatwa kwake. Siku moja, wiki moja kabla ya kukamatwa kwake, Abel alivamiwa na kupigwa wakati akielekea nyumbani alipokuwa akitoka kazini. Watu kadhaa walijotkeza na kumpiga vibay sana kiasi cha kupoteza fahamu na pia walichukua simu yake ya mkononi pamoja na ngamizi mpakato yake. Alihisi kuwa kwa kumpiga ilikuwa kama onyo, lililokuwa na lengo la kumfanya asiendelee kublogu. Hata hivyo, abel aliendelea na kazi yake.

Abel Wabela. Photo courtesy of family.

Abel Wabela. Picha kwa idhini ya familia.

Nilitaka kufahamu zaidi kuhusu Abel, kwa hiyo niliwaomba wale marafiki zake wa karibu kumzungumzia Abel. Endalk Chala anamzungunzia Abel kama mtu mwenye kujali sana na wa kipekee kabisa. Abel ni mtu mweledi sana na amminiye katika masikilizano, na anayeami katika majadiliano ya wazi na ya kweli.. Jomanex Kasaye anamuelezea Abel kama mtu asiyepindisha maneno na anayefahamu fika kile anachokisimamia. na wakati huo huo, Abel ni mnyenyekevu sana. Mara zote Abel anakuwa na uchu wa kutaka kujua. Mara nyingi anapenda sana kutumia muda wake kujadili na wanahistoria, wahadhiri wa vyuo vikuu na waandishi. imani yake ni moja ya vipau mbele vyake. Anapenda kuhudhia ibada kanisani. Mara kwa mara alikuwa akiwatembelea wafungwa, akiwa na upendo wa dhati kwa nchi yake na watu wake. Mara nyingi alikuwa akiwafikiria wengine kuliko anavyojifikiria yeye.

Matukio yasiyo nya utu dhidi ya Abel yaliendelea hata mara baada ya kushiliwa Maekelawi. Kufuatia shitaka lake la mwezi Februari, maafisa wa polisi walisahau kumfunga pingu wakati wakimrudisha gerezani. Kwa sababu hii, Abel aliadhibiwa. Walimfunga kwa mnyororo wa mbwa kwa siku nzima na pia kumnyang'anya kifaa chake cha kumsaidia kusikia. Wakati wa shitaka lake la mwezi Mei, kwa mara nyingine tena Abel aliadhibiwa kwa kutumia haki yake ya kujieleza. Abel aliwauliza majaji ni kwa nini hawakutoa ruhusa kwa washitakiwa kujieleza. Kwa sababu hii, Abel alihukumiwa kifungo cha miezi minne kwa kuibeza mahakama.

Aina ya matukio yasiyo ya utu alyokwishakabiliana nayo Abel yangeliweza kumkatisha tamaa mtu mwingine. Lakini, abel ameendelea kuwa na msimamo. Ninajiuliza: Ni nin haswa kinachomsukuma mtu hata kuweka reahani maisha yake kwa kufungwa jela, kupigwa na kuteswa? Kusoma Reading barua, ya hivi karibuni ya Abel kumenifanya nipate jibu:

Lengo langu ni kufanya mawasiliano. Lengo langu ni kujifunza. Sababu yangu kubwa ni kujihusisha kupata ufahamu wa kimaono na wa kina kabisa wa maisha na kupambana na hali ya kutokuchukua hatua na kutojali. Hii ndio nia yangu mimi kama mwanadamu. Hii siyo kazi niliyopewa na mtu asiyefahamika. Sitaruhusu yeyote yule kuminya haki hii ya msingi. Sitakubaliana na yeyote yule hata kama akiwa ni mwanasiasa, mtu binafsi, taasisi hata na jamii inayotaka kunipokonya haki yangu ya kujieleza. Ninatumia uhuru wangu wa kujieleza kwa watu kwa nafasi yangu binafsi, kwenye mitandao ya kijamii, gerezani, kwenye chumba cha mahakama, na hata kwenye vyumba vya polisi vya mahojiano. Ninatumia haki zangu za kujieleza ipasavyo bila la kuingilia haki za wengine, na hili ninataka kulionesha popote pale. Kwa kuweza kung'amua maangalizo, vitisho, kukamatwa na kuteswa hakujanifanya niache kutumia haki zangu za kujieleza na hata wakifanya hivi kwa siku zijazo.

“Kupambana na hali ya kutokuchukua hatua na kutojali… Hii ndio nia yangu mimi kama mwanadamu.” Sentensi hizi zinatoa jibu rahisi kwa swali gumu. Sababu inayomfanya Abel aendelee kutumia haki yake ya msingi ya uhuru wa kujieleza ni kwa kuwa ni haki ya msingi ambayo inaweza kutumiwa kila mahali na kwa kila hali. Ameafanya uamuzi wa kuitumia haki hii, kwa kuwa kuzungumza dhidi ya ukandamizaji ndio kupambana na hali ya kutokujali na kutochukua hatua. Nina uhakika zaidi ya asilimia mia kuwa ataendelea kutetea haki yake hadi mwisho wa maisha yake.

Tunaishi kwenye ulimwengu ambao kuna baadhi ya watu wanaouchora uhuru wa kujieleza kama kitendo cha ugaidi. Pia tunaishi kwenye ulimwengu ambao baadhi ya watu wanatoa sadaka uhuru wao katika kutetea uhuru wetu wa kujieleza. Wanablogu wa Zone9 walitetea haki za binadamu. Wameamua kusimamia kidete dhidi ya ukiukwaji wa haki. Wameamua kuusema ukweli. Kwa minajili hii, walipokonywa uhuru wao.They chose to stand up against injustice.
Hadi sasa, simfahamu Abel, lakini nina imani siku moja nitamfahamu.

* Kufuatia kukamatw kwao, wanablogu na waandishi hawa walifungwa gerezani huko Maekelawi. Maekelawi ni Sekta ya Polisi ya Shirikisho la Upelelezi wa Matukio lililopo Addis Ababa. Wafungwa wa kisiasa, waandishi wa habari, wanablogu, waratibu wa maandamano na wngine wengi huwekwa kizuizini huko kabla ya kupelekwa jela. Waangalizi wa haki za binadaPolitical prisoners, journalists, bloggers, protest organizers among others are held there before proceeding to prison. Shirika la uangalizi wa haki za binadamu, Human Rights Watch lilitoa ripoti kuhusiana na mateso, njia katili za kuhoji, na hali ilivyo huko ya mazingira duni ya mahabusu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.