Afrika Kusini Yakumbuka Mashindano ya Kombe la Dunia 2010 Yalivyokuwa

Soccer fans holding vuvuzelas watching the opening game of the World Cup. Photo by Marcello Casal Jr. Published by Agência Brasil under Creative Commons.

Mashabiki wa soka waliobeba mavuvuzela wakitazama mchezo wa ufunguzi wa Kombe la dunia. Picha ya Marcello Casal Jr. Imechapishwa na Agência Brasil kwa leseni ya Creative Commons.

Miaka mitano iliyopita mnamo Juni 11, mashindano ya 19 ya Kombe la Dunia la FIFA yalianza Afrika Kusini. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika kwenye ardhi ya Afrika. Kwa kutumia alama habari ya #2010Memories [#KumbukumbuZa2010], Waafrika Kusini kwenye mtandao wa twita walikumbuka siku ambayo mavuvuzela yalitawala ulimwengu wa kandanda.

Vha Musanda aliweka picha mtandaoni iliyoonesha dakika muhimu iliyoitoa mchozi ya furaha Afrika Kusini. Lilikuwa ni goli la kwanza kwenye mashindano hayo lililofungwa na mshambuliaji wa Afrika Kusini Tshabalala kwenye mchezo dhidi ya Mexico, uliomalizika kwa bao 1-1:

Dakika iliyowatoa machozi mashabiki wa Afrika Kusini. Tuliunganishwa. Shukrani kwa serikali kwa mchango wa raia waishio ughaibuni

Video ya YouTube hapa chini inamwonesha Shakira akiimba Waka Waka, wimbo rasmi wa Mashindano ya Kombe la Dunia 2010 wakati wa sherehe za ufunguzi:

Wakati kila mmoja alikuwa na ‘kichaa’ cha mashindano, Khulekani Mathe anakumbuka alivyochanganyikiwa kwa jambo jingine kabisa:

Siku kama ya leo 2010 nilikuwa India. Wakati kila mmoja akifuatilia mechi ya ufunguzi, nilikuwa nimechanganyikiwa nisijue wapi nikatazame mchezo huo

Mtumiaji wa twita King Billy anasema hakuwahi kujisikia salama kwenye mitaa ya Johannesburg, inayosemekana kuwa moja wapo ya mitaa hatari zaidi duniani:

Sikuwahi kujisikia salama kwenye mitaa ya Johannesburg mwezi huo kuliko kipindi chochote MAISHANI MWANGU

Vuma Augustus alisema hakuwahi kuona watu walioungana pamoja kama hao kwenye maisha yake:

Sikuwa kuwaona watu walioungana kiasi kwenye maisha yangu, nimekumbuka nyakati hizi sana

Baadhi ya Waafrika Kusini wanaoonekana kushangazwa na madai kwamba nchi hiyo ilitoa rushwa ya dola za Marekani milioni 10 ili kupewa nafasi ya kuandaa mashindano hayo.

Mtumiaji wa Twita ‘Yang and Reckless’ alisema kashfa hiyo haimsumbui:

Nilikuwepo kushuhudia nchi nzuri iliyoungana. Rushwa iwepo au isiwepo Kumbukumbu ya Kombe la Dunia la 2010 itaendelea kuwepo

Watu wengine mtandaoni hawakuwa tofauti sana:

Nani anajali kama rushwa ilitolewa au haikutolewa…tulipata viwanja vizuri…watalii bado wanakuja…sasa nini

Nchi nyingine, anasema Nkateko Baloi, zina wivu wa maendeleo ya Afrika Kusini mwaka 2010:

Kwa nini tubaki kukumbuka mambo ya zamani wakati nchi nyingine zina wivu wa namna mashindano yalivyokuwa mazuri

Kwa mujibu wa Kabwe Songolo, vitendo vya serikali ya Afrika Kusini na FIFA havipaswi kutupotezea mwelekeo wa kufurahia kandanda lenyewe:

Vitendo vya serikali ya Afrika Kusini na maafisa wa FIFA visitufanye kushindwe kufurahia tukio la Kombe la Dunia. Achacheni nao!

Baadhi ya watumiaji wa mtandao walielekeza maoni yao kwa wapepelezi wa Serikali ya Marekani, ambao ndio waliohusika kuwakamata wakubwa wa FIFA nchini Uswisi.

Lakini kimoja ambacho [wapelelezi wa] FBI hawawezi kukichukua kutoka Afrika Kusini, ni fahari na kumbukumbu ya 2010!

Hata hivyo, kumbukumbu za Charlie Langa hazikuwa chanya kama ilivyo kwa wa-Afrika Kusini wengine kwenye mtandao wa Twita:

Kumbukumbu ya Ufisadi. Rushwa, mipango ya wizi, Uhamishaji wa Fedha haramu, Ukwepaji wa kodi. Orodha ni ndefu

Wakati Tom Moultrie akishangaa kiasi gani cha uungwana walichokipoteza Waafrika Kusini tangu kumalizika kwa Kombe la Dunia:

Kumbukumbu za 2010 zimetamalaki kwenye mitandao yangu yote ya kijamii leo. Tumepoteza uungwana kiasi gani katika siku 1826 zilizopita?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.