Aprili, 2009

Habari kutoka Aprili, 2009

Rwanda: Miaka kumi na tano baada ya mauaji ya Kimbari

Hivi karibuni zilifanyika sherehe za kitaifa nchini Rwanda kuadhimisha kumbukumbu ya kutimiza miaka 15 tangu mauaji ya Kimbari. Mauaji hayo yaliangamiza maisha ya watu wapatao 800,000. Mnamo tarehe 7 Aprili, maadhimisho yalifanyika katika mji mkuu wa Kigali, na pia katika mji wa Nyanza, ambapo watu wapatao 5000 waliuawa kinyama. Katika Uwanja wa Mpira wa Kigali, maelfu ya mishumaa iliwashwa na kupangiliwa katika namna ambayo iliunda neno "Matumaini" katika lugha tatu.

Nguvu ya Watu Maarufu Katika uchaguzi wa India

  21 Aprili 2009

Waigizaji na watengenezaji filamu maarufu nchini India wana ushawishi mkubwa. Kushiriki kwa watoa burudani kutoka Bolywood (watengeneza wa filamu za Kihindi) wenye makao yao huko mjini Mumbai na wale wa filamu za Kitamil na Kitelugu kumepanda ghafla wakati huu wa kampeni za uchaguzi ujao wa India. Soma jinsi ambavyo wachezaji filamu maarufu wa India wanavyotoa ushawishi wakati wa kampeni.

Paraguai: Rais Lugo Akiri Kuzaa Mtoto Wakati Bado Akiwa Askofu

  19 Aprili 2009

Hivi karibuni Rais wa Paraguai Fernando Lugo alikiri kuwa alizaa mtoto wakati alipokuwa askofu wa kanisa la Katoliki la Roma. Habari hii imesababisha utata kati ya wanasiasa, vyombo vya habari, na wanablogu ambao wanaandika kuhusu kusikitishwa kwao na kiongozi huyo, na kadhalika jinsi ambavyo kuna matatizo mengine makubwa zaidi yanayotisha ambayo yanapaswa kutiliwa mkazo ikilinganishwa na vitendo vinavyofanywa na wanasiasa wengine.

Wanawake na Uchaguzi Nchini India

  14 Aprili 2009

Demokrasi kubwa zaidi duniani, India, itafanya uchaguzi mkuu utakaoanza katika wiki chache zijazo kutoka sasa. Wanawake wa India, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakinyimwa nafasi yao ya haki majumbani, kazini na katika hatamu za uongozi wana dau kubwa katika uchaguzi ujao. Japokuwa wanawake wengi wanaanza kuwa na ufahamu wa haki zao za kupiga kura na wanashiriki katika siasa kwenye ngazi za chini, ripoti hii inaeleza kwamba inavyoelekea mwaka huu ni wanawake wachache zaidi watakaochaguliwa katika bunge la nchi.

Irani: Mwaka Mpya Waanza na Ujumbe Kutoka Kwa Obama

  10 Aprili 2009

Siku Wairani waliposherehekea Norouz (Nowruz) kama sikukuu ya mwaka mpya nchini Irani, raisi wa Marekani Barak Obama alituma ujumbe kwa watu wa Irani na kwa viongozi wa Jamhuri ya kiislamu, ujumbe huo ulitoa rai ya kutaka mwanzo mpya kati ya nchi hizo mbili. Wanablogu kadhaa wametoa maoni kuhusu ujumbe huo, angalia baadhi ya maoni hayo.