Habari Kuu kutoka Januari 2013
Habari kutoka Januari, 2013
Msumbiji: Uhamasishaji wa Kiraia Kuwasaidia Waathirika wa Mafuriko
Baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko kusini mwa Msumbiji yaliyowaacha maelfu ya raia bila makazi na wengi kupoteza maisha, kikundi cha kiraia cha Msumbiji Makobo kimeanza kampeni ya mshikamano inayoitwa “S.O.S. Chókwè” kukusanya misaada ya hisani kwa ajili ya waathirika.
Jukwaa la Kiafrika Lenye Makala za Bure za Kitaaluma
Januari 24, ni siku ambayo inategemewa kuwa ya kuzindua rasmi Hadithi, ambalo ni jukwaa la kuhifadhia zana za bure za kitaaluma mjini Nairobi, Kenya. Wasomi mbalimbali na wadau wa mitandao watakusanyika pamoja kujadili upatikanaji wa zana huru za kitaaluma katika elimu ya juu nchini Kenya. Hadithi itasaidia kutafuta, kuona na kushusha...
“Wanasemaje Bamako?” Mazungumzo na Awa anayeishi Mali
Anne Morin na Awa Traoré wanabadilishana mawazo kuhusiana na maisha ya kila siku mjini Bamako, ujira usiokidhi mahitaji, gharama za maisha na hali ya kisiasa isiyotabirika wakati huu ambapo vita vinanukia nchini humo.
Mwanaharakati wa Pakistani Khudi Ali Auawa Katika Mlipuko wa Bomu
Mnamo Januari 10, 2013 katika jiji la Quetta lililopo Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Pakistani, watu 82 walipoteza maisha kwenye milipuko ya mabomu yaliyolenga eneo ambalo kimsingi lenye idadi kubwa ya Waislamu wa Shia jamii ya Hazara. Irfan Khudi Ali, mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu ambaye bila kuchoka aliweka wazi uonevu wa kikabila unaofanywa kwa waShia wa Hazara nchini Pakistan, alifariki katika shambulio lililofuata. Kifo chake kimechochea watu kumpa heshima kwa juhudi zake kwa kuanzisha tena maandamano kupinga mauaji ya watu wa Shia nchini Pakistani.
Mashoga Washambuliwa Kaskazini mwa Kameruni
Oscarine Mbozo’a anaripoti [fr] katika blogu ya L'Actu kuwa shoga mmoja akiwa ameambatana na mwenzi wake walizomewa karibu na soko mnamo tarehe 6, Januari 2013, mjini Maroua, Kaskazini mwa Kameruni: Goche Lamine, mfanyabiashara wa madawa, alikamatwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari aitwaye Sanda, mwenye umri wa miaka 17. Umati wa...
Rais wa Chadi Awateua Wanawe Kushika Nafasi Nyeti
Djamil Ahmat anaripoti kuwa rais Déby wa Chadi amemteua mwanae wa kiume Mahamat Idriss Déby, 24, kuwa brigedia jenerali [fr] pamoja na maafisa wengine wanne. Tchadanthopus anaongeza kuwa mwanae mwingine Zackaria Idriss Deby alisemekana kukabidhiwa umakamu wa rais [fr] nafasi ambayo inampa madaraka yote wakati baba yake anapokuwa nje ya...
Kujitenga kwa Mtu wa Jamii ya Alawite: Jinsi Msichana wa Syria Alivyompoteza Mama Yake.
Loubna Mrie alipata pigo kubwa kutokana na msimamo wake kuhusiana na mapinduzi ya Syria. Kama mtu wa kikundi cha alawite aliyeamua kuwa na msimamo tofauti dhidi ya Rais Bshar Al Assad, aliamua kujitenga na jamii yake; watu
Mwaka Mpya na Mienendo ya Zamani Nchini Bahrain
Wakati nchi mbalimbali ulimwenguni kote zikiukaribisha mwaka mpya kwa fataki na shamrashamra, serikali ya Bahraini iliandaa utaratibu wa aina yake kwa waandamanaji nchini humo. kwa bahati, watumiaji wa mtandao wa intaneti walikuwa tayari, kuonesha na kuweka kumbukumbu ya baadhi ya matukio kwa ajili ya kushuhudiwa na sehemu nyingine yote ya ulimwengu.