Mnamo Januari 10, 2013 katika jiji la Quetta lililopo Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Pakistani, watu 82 walipoteza maisha kwenye milipuko ya mabomu yaliyolenga eneo ambalo kimsingi lina idadi kubwa ya watu wa jamii ya Waislamu wa Shia jamii ya Hazara.
Irfan Khudi Ali, mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu ambaye bila kuchoka aliweka wazi uonevu wa kikabila unaofanywa kwa waShia wa Hazara nchini Pakistan, alifariki katika shambulio lililofuata.
Katika ukurasa wa Twita, Ali alitaarifu kuwa, aliponea chupuchupu kwenye tukio la mlipuko mabomu wa kwanza huko Quetta:
@khudiali : #Quetta, nilikuwa ninaelekea nyumbani na ndipo nikaponea chupuchupu kwenye mlipuko wa bomu lililoua watu 11.
Maria Memon alitwiti:
Ali hakuweza kuepuka kwenye mlipuko wa pili wa mabomu. Pumzika kwa amani. @khudiali RT @khudiali #Quetta, alikuwa akielekea nyumbani na aliponea chupuchupu kwenye mlipuko wa mabomu ulioua watu 11
Kifo chake kimeamsha heshima ya juhudi zake na kupelekea kuamsha tena maandamano kuhusu mauaji ya watu wa Shia nchini Pakistani. Mara ya mwisho Ali alipoTwiti alituma taarifa kutoka katika eneo la machafuko iliyoelezea kuhama kwa watu wa jamii ya Hazara kulikotokana na unyanyasaji wa kiitikadi:
@khudiali #Familia za Hazara za #Machh,Khuzdir hatimaye imejikuta kwenye hali tete ya mauaji ya halaikifinally succumbed to the genocidal pressure&moving out. Siku mbaya itokanayo na utofauti wa asili #Balochistan.

Irfan Ali wakati wa maandamano ya kupinga vurugu za kidini huko Islamabad mnamo Septemba 2012. Kutoka katika ukurasa wa Facebook wa Umoja wa Vijana wa Pakistan.
Tangu mwaka 2001, waislam wa Shia wa Hazara kutoka Quetta – kwa kawaida wamekuwa wakitafutwa na makundi ya kijeshi. wakiwa kama kundi la watu wachache miongoni mwa kundi la watu wa tabaka la chini, mauaji ya Hazara Shia ni miongoni mwa matukio ya kikatili yasiyotolewa taarifa kabisa nchini Pakistan.
Hazara.net inaonesha takwimu za kumbukumbu ya mauaji ya watu wa Hazara ya Shiite nchini Pakistan, ikijumuisha idadi ya mashambulizi na idadi ya watu waliouawa hasi sasa. Kwa mjibu wa takwimu katika katika tovuti hiyo, jumla ya watu 1100 wa jamii ya Hazara Shiite wameshauliwa nchini Pakistan tangu mwaka 1999.
Vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa vikikabiliana na changamoto pale vinaposhindwa kuweka bayana kiini cha mashambulizi, na wnapofanya hivyo, wanalaumiwa kutumia ‘udhehebu’ pale dhehebu fulani linaposhambuliwa. Katika juhudi za kupigia kelele na kuongeza nguvu kwa mashirika ya kuhakikisha sheria zinasimamiwa pamoja na serikali, kumekuwa na mjadala endelevu katika vyombo vya habari vya kiraia kufuatia mauaji ya kukusudia yanayoelekezwa kwa watu wa Shiite, mjadala unaoendeshwa kupitia viungo ishara #mauaji ya Shia na #mauaji ya kimbari ya shia katika Twita. Kwa kipindi kilichopita, wanaharakati wa Shia, walitumia mitandao ya kijamii ili kupata kuungwa mkono na vyombo ya habari vya kimataifa ili habari zao ziweze kutangazwa.
Mwandishi wa habari anayeheshimika sana, Mohammad Hanif anaandika:
@mohammedhanif: inaonekana kutakuwa na muafaka siku za hivi karibuni kuwa kuita ni mashambulizi ya kidhehebu ni chanzo kikubwa cha mashambulizi ya kimadhehebu.
@zainabimam: Kazi nzuri, Faisal Qureshi (muigizaji) kwa kipindi cha asubuhi kuhusu imani ya watu wa Shia. Ameonesha ujasiri. Shukrani kutoka #Shia. #Pakistan
@adyadeel: #mauaji ya halaiki ya Shia lazima yaishe. Serikali lazima ichukue hatua stahiki ilikuonesha kuwa wako makini katika kuokoa maisha ya watu wa Shia wasio na hatia.
Mwanablogu Omar Biden, aliandika makala fupi ya heshima kuhusu Irfan Khudi Ali katika blogu yake:
Jana ilikuwa ni miongoni mwa siku nyingi za umwagaji damu kwa mji mkuu wa Balochistan ambao ni, Quetta. Mapema asubuhi ya leo, wakazi wa jiji wametoka kusikia sauti ya mlipuko wa mabomu ambayo yalitegwa kwenye gari la mgambo wanaolinda mpakani huko Bacha Khan Chowk. Mlipuko huo ulipelekea watu 12 wasio na hatia kuuawa. Kwa hakika, ilisababishaIndeed, it created helter-skelter kati ya wakazi kuzika miili ya watu waliofariki.
Bado, kanuni ya zaidi-halafu-itoshe haitumiki nchini Pakistani, angalao siyo huko Quetta. Baada ya masaa machache, barabara ya Almadar, makazi muhimu ya watu wa Shia Hazara, ilishuhudiwa mauaji makubwa ya kinyama, na tena kwa kutumia mbinu ileile iliyotumika kwenye mlipuko wa asubuhi. Hata hivyo, hii “Mardanawar”, lililotegwa kwa muda maalum, kwa ujasiri kabisa, mlipuko pacha uliosababisha uharibifu usiosahaulika (…)
Matukio ya kikatili yamegharimu idadi kubwa ya watu kwa hakika. Hali iliyopelekea pia kifo cha rafiki aliyekubalika, mwanaharakati wa haki za binadamu–Irfan Ali Khudi.
Kama inavyodaiwa, Irfan Ali Khudi mwenye umri wa miaka 33, alifika Quetta ili aweze “kutoa mafunzo kwa wanaharakati wanaochipukia”.
Pamoja na kuwa nililenga kuandika mawazo yangu, ninaiacha makala hii bila kuimalizia…
Siku ya damu Quetta, kama Omar anavyoiita, siyo ya kwanza ya aina yake na inaweza isiwe ya mwisho. Hali ya kutokuwa na maelewano imewakasirisha wengi, haswa hswa tokea kikundi cha kijeshi kilipofutwa, Lashkar-e-Jhangvi, waliotangaza kuhusika na mashambulizi, bado hawajakamatwa.
@sehartariq : kwa nini tunawaonea huruma Waislamu wa Gaza kuliko Waislamu wa #Pakistan ambao tuna historia moja na vinasaba vinayofanana; uraia #mauaji ya halaiki ya shia
@zzzAsad : Watu wa Shia mara nyingi huwa wanaviziwa na wanamgambo wenye mrengo wa kidini pindi wanaposafiri kwa mabasi kwenda kuhiji. #LeJ #ShiaGenocide
@FahidJaved : Wewe muuaji #LeJ uliye katili, niue mimi#WeAreAllHazara. Kila mtu wa Pakistani ni wa jamii ya Hazara, kila mmoja wetu. Mtawaua wangapi? Mna risasi ngapi? blockquote>
@Naseer_Kakar : Mapema katika #Quetta: Wahanga wote waehamishiwa katika hospitali ya kijeshi kutokana madaktari kutishwa na #LeJ katika hospitali za umma.#Balochistan #blasts
@AhmadShuja : RIP @khudiali. Walikuua lakini hamasa na ari uliyokuwa nayo inaendelea kubaki. #LeJ #Quetta
@ZakirChangezi : Quoting #KhudiAli “Watu wangu wa Shia wanaangamia. Kama initakufa, ninataka kufa huku nikijaribu kuwaokoa” #RIPKhudiAli
Familia za wahanga zilikataa kuzika miili ya ndugu zao na wametangaza kuwa wataendelea na maandamano ya kupinga unyanyasaji wa kikabila hadi hapo jeshi litakapochukua hatua ya kukomesha mauaji haya ya kinyama. Picha hii iliyopakiwa katika ukurasa wa Twita inawaonesha maelfu ya watu wa Hazara wakiwa wameketi huku wakinyeshewa mvua huku kukiwa pia na miili ya watu waliopoteza maisha katika mauaji ya halaiki wakati wa milipuko ya Quetta.
@ammar_faheem : Waandamanaji wa Shia protesters stage sit in on Quetta's katika barabar ya alamdaar wakiwa na miili ya watu waliokufa katikaa milipuko ya mabomu iliyotokea jana#ShiaGenocide
@AdnanSarparrah : Maandamano yanayofanywa na watu wa Shia ya kupinga unyanyasaji wa kikabila yanaendelea lakini kukabidhiSit-in by the Shia community continues but handing over #Quetta kwa jeshi haitakuwa njia muafaka, Quetta tayari ipo chini ya uangalizi wa Jeshi (FC)
Ali aliongea katika tukio la Tedx huko katika jiji la Rawalpindi mapema wiki chache zilizopita, tazama hapa hotuba yake iliyo na hamasa kubwa
Ali alitumia muda wake mwingi kuelezea hali ngumu wanayopitia watu wa Hazara, kjwa wale waliotokea kumfahamu na wale ambao hawakumfahamu, amekuwa ni mfano wa kuigwa katika harakati za kutafuta amani kwa jamii ya watu wa Hazara nchini Pakistani. Wakati maandamano hayo yakiendelea, katika hali ya baridi na mvua, huku familia zikikataa kuzika miili ya ndugu zao, je serikali itachukua juhudi za dhati za kukomesha mauaji haya ya Halaiki? Hadi wakati mwingine, habari ya Ali inapaswa kusikika.