Uchafuzi wa Hewa wa Kutisha Jijini Tehran Waanikwa

Uchafuzi wa hewa umekuwa adui wa umma kwa mamilioni ya watu wa Tehran kwa miaka mingi sasa. Hivi leo, si habari za kushangaza tena kusikia kuwa siku fulani serikali imesitisha huduma katika taasisi za serikali kwa sababu ya uchafuzi wa hewa.

Mapema mwezi huu, Wizara ya Afya, ilitangaza kuwa katika mwaka uliopita zaidi ya watu 4, 400 walipoteza maisha kutokana na uchafuzi wa hewa huko Tehran, mji mkuu wa Iran.

Tehran iliyofunikwa Vumbi

Kuna baadhi ya katuni zinazosambazwa na watumiaji wa mtandao wa nchini Iran kuhusiana na uchafuzi huo wa hewa mjini Tehran. Omid alichora katuni katika mtandao wa Iroon.com ili kuonesha Tehran ilivyofunikwa na vumbi.

Omid, Iroon.com

Mana Neyastani hakuacha kupiga siasa kwa kutumia katuni kuhusiana na uchafuzi huu: “Babu” anasema “Kumekucha tena, na ninapaswa kuamka… habari mbaya hizi…adhabu, jela…” “Babu” anavuta pumzi nzito ili kuianza siku yake na kuanguka chini kando ya jarida lenye kichwa cha habari: “Uchafuzi uliokithiri wa hewa ya Tehran”

Mana Neyestani, Mardomak.

Jiji la Giza

Ifuatayo ni video inayoonesha Tehran iliyochafuka kwa moshi mweusi wakati wa adhuhuri, muda ambao ndege ilikuwa inatua katika uwanja wa ndege wa Mehrabad.

Hakuna Hewa ya Oksigeni

Mwanablogu wa Iran ajulikanaye kwa jina la Zeyton, anasema [fa]:

Tulizoea kusema kuwa hakuna sehemu ya kupumulia katika nchi hii. Kwa kusema hivi, tulikuwa na maana ya ukandamizaji wa kisiasa na wa kijamii uliofanywa na serikali. Lakini kwa sasa, kiuhalisia hakuna hewa ya Oxygen ya kuvuta. Serikali isiyoweza kuhakikisha watu wake wanapata hewa ya Oxygen ya kutosha ndiyo hii inayojigamba kuonesha mfano wa kuigwa wa kiutawala ulimwenguni kote.

Tusisahau kuwa watu katika miji mingine mingi nchini Iran nao pia wameshakuwa wahanga wa uchafuzi huu, kama ilivyo kwa jiji la Kaskazini,Ahwaz [fa].

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.