Kujitenga kwa Mtu wa Jamii ya Alawite: Jinsi Msichana wa Syria Alivyompoteza Mama Yake.

Kama sehemu ya ushirikiano wetu na Syria Deeply tuna mfululizo wa makala mbalimbali zinazogusa sauti za raia zilizopatikana katika machafuko sambamba na mitizamo ya waandishi kutoka ulimwenguni kote kuhusiana na mgogoro unaoendelea.

Loubna Mrie alipata pigo kubwa kutokana na msimamo wake kuhusiana na mapinduzi ya Syria. Kama mtu wa kikundi cha Alawite aliyeamua kuwa na msimamo tofauti dhidi ya Rais Bashar Al Assad, aliamua kujitenga moja kwa moja na jamii yake; watu wengine wa Alawite wameendelea kumtii Assad kama kiongozi wa dhehebu na mwangalizi wao kutokana na upendeleo wanaoupata kutoka kwa kiongozi wao akiwa kama Rais.
Kuanzia mwanzo wa harakati za kuwa kinyume na mamlaka, wazazi wa Loubna walikuwa katika pande tofauti: baba yake na wajomba zake walikuwa upande wa Assad, wakati Loubna na mama yake walikuwa wakiunga mkono maandamano yaliyokuwa yakishamiri.

Ulikuwa ni upande alipo baba yake na Loubna uliomfanya afikie msimamo wa kushindwa kuvumilia: baba yake alimtaka atii upande wa Assad. Mwezi Agusti, Loubna aliondoka katika mji aliokulia wa Latakia, Magharibi mwa Syria na alisafiri kwa ndege hadi Uturuki. Baba yake alimshikilia mama yake na Loubna kama mateka na kutishia kumuua kama sehemu ya adhabu. Loubna alipokataa kurudi, baba yake alitimiza adhabu aliyoipanga. Baba yake hatimaye alimuua mama yake na Loubna, alimkatisha maisha aliyoyajua kabla ya kuamua kuwa kinyume na mamlaka ya Syria..

Kwa sasa, Loubna ni mtayarishaji wa filamu wa Basma, kikundi cha uanaharakati wa vyombo vya habari. Anasafiri maeneo mengi ya Syria na kamera yake akikusanya matukio ya mapinduzi ya Syria katika filamu. Tulikutana naye huko Gaziantep, Uturuki ili kuongea naye kuhusu maisha na vita nchini Syria. Ifuatayo ni sehemu ya mazungumzo yetu naye.

SD: Latakia kulikuwaje wakati harakati za mapinduzi zilipoanza?

Mrie: Ilianza kama ilivyo kwa kila jiji nchini Syria. Maandamano yalikuwa na misemo ya amani kabisa kama vile, “tunahitaji shule nzuri”, “tunahitaji kazi zilizo bora”, “tunahitaji demokrasia”. Na hata hatukusema “al shaab yureed isqat al nizam”—“ watu wanataka serikali itoke madarakani”.

SD: Kulikuwa na watu wengi wa Alawite walioandamana?

Mrie: Hapana. Ilikuwa nadra sana kumuona mtu wa Alawite katika maandamano. Latakia kuna watu wa Alawite wengi sana na wengi wao walikuwa wanauunga mkono utawala ulioko madarakani. Tulikuwa na kikundi kidogo sana cha wanajamii waliokuwa kinyume na serikali, lakini hawakwenda kwenye maandamano kwa kuwa walikuwa wakiogopa kupita kiasi. Tokea siku ya kwanza, utawala ulijaribu kuwashawishi watu kuwa haya hayakuwa mapinduzi, ni magaidi tu au harakati tu za kiislam dhidi yenu.

SD: Haya yote yalitokea lini? Ni wakati gani ambapo familia yako ilijitenga?

Mrie: Mwezi Novemba mwaka jana. Ilisikitisha sana, hata sikuweza hata kuwaza kuhusu jambo lolote. Nilijisikia mwenye hatia, hatia kubwa. Nililia kwa siku tatu, lakini niligundua kuwa mama yangu hakunihurumia kabisa pamoja na kulia kwangu siku nzima chumbani mwangu, kwa hiyo, nilifanya maamuzi mengine: nilichukua kamera yangu haraka na kurudi Syria.

SD: Aliongea nawe katika ule mwezi wa misho??

Loubna

Mrie: Hapana, walimteka katikati ya mwezi Agusti. Baada ya hapo, hakuwahi kuwasiliana nami tena. Hata shangazi zangu na bibi yangu hawakutaka kuwasiliana nami tena kwa kuwa waliogopa sana kuwa kama serikali ingegundua kuwa walikuwa wanawasiliana nami, wangewadhuru. Hata majirani zangu na marafiki wa zamani hawakuwasiliana nami kabisa. Hawakunipa pole, hawakuonesha huzuni yao, wala kuonesha hali ya kutoguswa na lililotokea kabisa. Ni kama vile walikuwa wanasema nilistahili. Kwa hiyo, sio tu kifo cha mama yangu kilichonivunja moyo, lakini pia na mtazamo wa watu nilioishi nao toka utotoni.

SD: Baba yako alikuwa na mtazamo gani?

Mrie: Sifahamu kabisa. Labda walikuwa wanashawishiwa tu na hadithi hizi kuwa serikali ilishawaambia: kuwa hizi ni harakati za kiislamu, na watakuua, na kuwa, utapoteza kila kitu. Nafikiri kwa familia kubwa—familia yangu ni miongoni mwao—wanaogopa sana. Wanajua kuwa, kama utawala utaachia ngazi, watapoteza kila kitu, kwa sababu, serikali ilipokuwa na mamlaka yote ya kuongoza, walijua wangeweza kufanya lolote na kusingekuwa na yeyote wa kuwapa adhabu. Wangeweza kuiba, kudanganya na unyang’anyi.

Kwa upande wangu, ninapata mantiki ya kinachofanyika kwa familia tajiri au familia zilizo madarakani, lakini sizielewi familia masikini zinazomuunga mkono Assad. Ninawakumbuka majirani zangu… walikuwa masikini sana. Nilishangaa, ni kwa nini mnaendelea kuunga mkono mfumo wa utawala? Serikali imekufanyia nini?

Baada ya muda fulani, tuligundua kuwa, kwao, ilikuwa ni kama aina fulani hivi ya dini. Kwa miaka ya hivi karibuni, alikuwa ni Hafez Al Assad, na sasa ni Bashar Al Assad. Watu wanawaabudu hawa jamaa. Tangu mapinduzi yalipoanza, niliendelea kuwaambia watu kuwa, waandamanaji walioko mitaani, wapinzani, sio wakatili. Nilisafiri kwa ndege hadi Uturuki kwa msaada wa Jeshi Huru la Syria. Walikuwa wakarimu kwangu na walinisaidia sana. Walifahamu kuwa mimi ni miongoni mwa watu wa Alawite, lakini hawakuniua kama jinsi ambayo serikali kila mara inavyojaribu kusema,

SD: Unadhani wanabadili mitazamo yao? Unadhani jamii inabadili mtazamo wake?

Mrie: Kwa sasa wapo katikati. Wanapoteza watoto wao kwenye mapigano. Wanapoteza uzao wao katika jeshi. Kwa hiyo, wanatambua kuwa serikali haiwafanyii jambo lolote zuri, lakini, wakati huohuo, wanaogopa sana kuwa kinyume na serikali. Tuna chembechembe za kiislam katika mapinduzi, na hizi zinawafanya wawe na hofu sana.

Nimekuwa nikisikia habari za kwa vipi, na lini miili ya watu waliokufa ilivyoletwa katika vijiji vya watu wa Alawite, vijiji vyote vikaanza kumlaani Bashar Al Assad na Serikali yake kwa kuwa hawezi kuwalinda na wanajitolea kwa mtu asiyeweka juhudi yoyote.

SD: Kwa kile tunachoendelea kukisikia, serikali imeiogopesha sana jamii ya Alawite kiasi kwamba wanafikiri kuwa ni mapigano ya kuokoa uhai, maisha au vifo vyao. Unafikiri ni kwa namna gani utaweza kuiondoa hofu hiyo?

Mrie: Tatizo la jamii hii ni kuwa, hawataelewa. Wanachokifahamu wao ni kuwa, kama ulikuwa mtu wa Alawite, na ulikuwa mpinzani wa serikali, adhabu yako itakuwa mara mbili.

Laiti wangefuatilia habari na kutazama televisheni na wangezisikia kauli mbiu, wangejua kuwa haya si mapinduzi dhidi yao.

SD: Wakati huu katika jamii ya watu wa Alawite, kama mtu atasimama imara, kama ilivyo wewe, na akaunga mkono mapinduzi, kitu gani kitatokea?

Mrie: Wangemuua mama yake.

SD: Wanasema hivyo?

Mrie: Hapana, lakini ilinitokea mimi. Mimi siyo gaidi. Sikufanya jambo lolote baya. Nilijiondoa tu kutoka kwenye jamii yangu ndogo na kusema kuwa nipo upande wa mapinduzi, nipo na watu wangu. Sitaweza kuendelea kushuhudia damu inavyomwagika halafu nikaa kimya. Hali hii haisababishwi na siasa, kwa sasa inasababishwa na binadamu…haya ni mapinduzi kwa ajili yetu, kwa ajili ya watoto wetu, kwa ajili ya babu na bibi zetu.

SD: Serikali yote inaweza kubadilika kesho. Vyovyote itakavyokuwa, unafikiri jamii hii italipokeaje hili? Syria itabadilika vipi kama bado kuna hofu kubwa miongoni mwa jamii ya watu wa Alawite?

Mrie: Hadi sasa tuna maeneo ambayo yapo huru. Kuna watu wa Alawite katika maeneo hayo, kwa hiyo unaweza kuona mfano wa Syria mpya, jinsi itakavyokuwa. [Upinzani] hauwaui watu wa jamii ya Alawite, hawawaondoi katika nyumba zao. Sisi ni kitu kimoja. Sisi ni jamii iliyo njema. Sio kwa sababu ya Bashar Al Assad, sababu ni kuwa, sisi ni watu wenye amani.

SD: Wapo baadhi ya watu wa Alawite katika serikali ya mpito, kwa upande wa upinzani. Ni watu ambao wanaheshimika kwa jamii kubwa ya Alawite? Ni watu ambao wanaweza kuja kuwa viongozi na wakaisaidia jamii?

Mrie: Jamii inawachukia hao watu wa Alawite ambao wako na Moaz al Khatib. Wanasema hawa wala sio watu wa jamii ya Alawite—ni watu waliojitenga.

Loubna

Ninaishi maisha ya namna hii hii. Waliingia nyumbani kwangu. Waliiba vitu vyangu vyote. Waliiba karatasi zangu za chuoni. Yote haya yalifanywa na watu wa jamii yangu ya watu wa Alawite ambao wanaiunga mkono serikali, yalikuwa ni maneno mabaya tu katika ukurasa wa facebook.

SD: Walisemaje?

Mrie: Kuwa ulistahili na tunaombea lililomtokea mama yako litokee na kwako.

SD: Yawezekana wakati wote kukawa na kiasi fulani cha hasira dhidi ya watu wa Alawite kwa kumuunga mkono Assad? Hii inamaanisha nini kwa nchi ya Syria?

Mrie: Nchini Syria, mabomu bado yanaendelea kulipuliwa na kila siku watu wanaendelea kufa. Kwa hiyo, kwa sasa hatuwezi kwa hakika, kuamua muonekano wa Syria ijayo. Tunajua kuwa. Kulipiza kisasi hakujengi nchi wala demokrasia. Tuliingia mitaani na kujitoa sadaka ili kuijenga nchi mpya. Visasi havitatusaidia kulifanikisha hili. Lakini tutawap adhabu watu waliofanya makosa, wale walioua.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.