Mwandishi wa Kike wa Yemeni Asumbuliwa kwa “Kutokuheshimu Dini”

Samia Al-Agbhari

Samia Al-Agbhari..mwandishi wa Yemeni anakabiliwa na mashambulizi ya kipropaganda. Picha iliwekwa kwenye mtandao wa Facebook na Afra Nasser

Kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, mwanablogu wa Yemeni Afra Nasser anazungumzia kwa kina suala la kubana uhuru wa kujieleza katika nchi yake na namna mwandishi huyo wa kike anavyosumbuliwa -kama anavyodai yeye kwa kutokuheshimu dini. Anaandika:

Kubana uhuru wa kujieleza katika nchi ya Yemeni kunaendelea. Mwandishi mwingine wa Yemen anakabiliwa na mashambulizi makubwa; akikashifiwa na kutuhumiwa kutokuheshimu dini. Akiwa mmoja wapo wa waandishi bora kabisa nchini Yemeni, Samia Al-agbhari anashambuliwa mno na propaganda za vyombo vya habari na kumtishia kufuatia msimamo wake wa kishujaa.

Wakati wa akitoa hotuba yake ya hivi karibuni alisema, “Matatizo makubwa zaidi nchini Yemen ni, Jeshi, Dini na Ukabila.” Si tu kwamba nakubaliana na kauli yake hiyo, bali namwunga mkono kwa dhati kabida. NIna hakika ataendelea kuwa imara na jasiri, lakini nina wasiwasi na usalama wake baada ya hapa.

Wakati unaokaribiana na huu, mwaka jana, Boushra al-Maqtary alikumbana na bado anakumbana na suala kama hilo. Nilikutana na Boushra mwezi mmoja uliopita, ninaweza kusema kwa hakika kabisa, namna wakubwa wa dini wanavyopambana na waandishi, ndivyo tunavyokuwa na mwelekeo madhubuti na imara. Waandishi wa kweli ni mashujaa. Wataelewa ukweli huu lini!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.