Pasipoti za Kidiplomasia kwa Viongozi wa Kidini nchini Brazil?

Hivi karibuni mjadala mkali umepamba moto nchini Brazil baada ya Wizara ya Mahusiano ya Kimataifa, inayoitwa Itamaraty, kutoa pasipoti mbili za kidiplomasia [pt] kwa viongozi wa makanisa ya kiinjili Igreja Mundial do Poder de Deus (Kanisa la Dunia la Nguvu la Mungu/World Church of the Power of God) mchungaji Valdemiro Santiago de Oliveira na mke wake Franciléia de Castro Gomes de Oliveira.

Nchini Brazil utoaji wa pasipoti za kidiplomasia unadhibitiwa na katiba ya nchi Kifungu ya 5.978 [pt] kinachotamka kuwa nyaraka hizo rasmi zinaweza kutolewa kwa marais, makamu wa rais, mawaziri, wabunge, wakuu wa idara za kidiplomasia, majaji wa mahakama kuu na marais waliopita. Hata hivyo, pasipoti za kidiplomasia zimekuwa zikitolewa kwa wawakilishi wa Kanisa Katoliki, kwa kutumia tafsiri ya Ibara ya 6, kifungu cha 3:

Photo of Pastor Valdemiro Santiago on facebook.

Picha ya Mchungaji Valdemiro Santiago iliyotoka kwenye ukurasa wake wa wazi wa Facebook

…às pessoas que, embora não relacionadas nos incisos deste artigo, devam portá-lo em função do interesse do País.

…kwa watu ambao, ingawa hawajaorodheshwa katika ibara hii, wanahitaji kuipata ili kutimiza majukumu yenye maslahi ya nchi.

Ingawa, kama ilivyotajwa awali, Makadinali wa Kanisa Katoliki wamekuwa wakinufaika na takwa hilo la kikatiba, taasisi nyingine za kidini zinazotambuliwa na serikali ya Brazil hazijatengwa katika kuomba pasipoti za kidiplomasia na hata wakuu wengine wa madhehebu ya kiprotestanti, kama mchungaji ambaye ni vigumu kueleweka kirahisi Edir Macêdo, kiongozi wa Kanisa la Ulimwengu (Igreja Universal) walipokea pasipoti za kidiplomasia siku za nyuma.

Tushukuru siku hizi kuna uwazi ulioletwa na vyombo vya habari ambao uliwezesha jambo hili kufahamika na kufikia Wizara husika kupata upinzani mkali kutoka kwa raia watumiao mtandao kufuatia uamuzi huo. Ukosoaji wa hatua hiyo umechochea kwa namna mpya mjadala uliokuwepo wa mamlaka ya taasisi husika na kukiukwa kwa dhana ya nchi kutokuwa na dini kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.

Msomaji wa gazeti la Folha de São Paulo, Renato Khair, alituma maoni yafuatayo akijibu makala [pt] iliyokuwa ikiangazia suala hilo:

É inaceitável que o governo tenha se utilizado do Itamaraty para fornecer passaporte diplomático para o pasto líder da Igreja Mundial. É uma aberração que pessoas que não preencham os requisitos legais recebam passaporte diplomático, como é o caso dos filhos de Lula, do referido pastor e tantos outros. É desmoralizante o que estão fazendo com o Ministério das Relações Exteriores e o Itamaraty, que eram considerados instituições sérias e respeitadas.

Ni jambo lisilokubalikaa kwa serikali kuitumia Wizara ya Mahusiano ya Kimataifa kutoa pasipoti za kidiplomasia kwa Kanisa liitwalo World Church. Ni kupotoka kuona watu wasiokidhi vigezo vya kisheria wanapokea pasipoti za kidiplomasia, kama watoto wa Rais wa zamani Lula, Makasisi watajwa na wengine wengine. Kinachofanywa na Wizara ya Mahusiano ya Kimataifa ni kudhalilisha taasisi ambazo awali zilionekana kama zenye heshima na zenye umakini katika utendaji wake.

Mwanablogu Parsifal Pontes vilevile alikosoa [pt] utoaji huo wa pasipoti za kidiplomasia kwa kusisitiza:

A nossa chancelaria banaliza de tal maneira o passaporte diplomático que daqui a pouco as autoridades portuárias alhures vão gargalhar quando virem um.

Namna tu wizara yetu inavyochukulia kiwepesi suala la kutoa pasipoti za kidiplomasia na kutumia vibaya mamlaka yake itasababisha idara za uhamiaji nje ya nchi waangue vicheko wanapoona aina ya watu wanaotembea na nyaraka hizo.

Igreja Mundial do Poder de Deus. Photo by Roberto Castelhano on Flickr.

Igreja Mundial do Poder de Deus. Picha ya Roberto Castelhano kwenye mtandao wa Flickr. (CC BY-NC-ND 2.0).

Kwenye Mtandao wa twita, kupitia alama habari #estadolaicoja (nchi isiyo na dini sasa) mwenendo wa majadiliano unaonyesha kuwa nchi ya Brazili imevuka mipaka kwa kuvunja kanuni za msingi za nchi kutokufungamana na dini dhana ambayo ilipaswa kuheshimiwa.

Lawyer Thiago G. Viana (@thiago_fiago), ambaye hublogu na Comendo o Fruto Proibido, alitwiti:

Legalidade, igualdade, moralidade e laicidade: são “só” esses princípios violados pelos passaportes especiais para pastores.

Heshima ya sheria, usawa, maadili na nchi kutokuwa na mfungamano na dini: hii ni misingi “pekee” iliyovunjwa katika kutoa pasipoti za kusafiria kwa wachungaji.

Mwendesha mashitaka wa serikali Chico (@chiconob) anaendelea katika msimamo huo huo wa mawazo:

Simplesmente NAO HÁ argumento plausível pra conceder passaporte diplomático pra religiosos. Que vexame!

Hakuna hoja yenye mashiko kutetea kitendo cha kutoa pasipoti za kusafiria za kidiplomasia kwa viongozi wa kidini. Inachefua mno!

Mjadala huo mtandaoni unaurudisha tena mezani mdahalo wa siku nyingi na unaoendelea kuhusu dhana ya serikali kutokuwa na dini nchini Brazili. Ingawa katiba inatenganisha bayana masuala ya utawala wa Serikali na yale ya dini, katika hali halisi utoaji wa pasipoti za kidiplomasia kwa viongozi wa kidini unaonekana wazi kuvunja kanuni hiyo, na tuwe wakweli, inawezekana vipi kiongozi wa kidini kubeba pasipoti ya kidiplomasia bila kuvunja kanuni ya msingi kabisa ya nchi kutokuwa na dini? Kiongozi yeyote anayebeba nyaraka nyeti ya kumwezesha kusafiri kidiplomasia hapaswi, kwa wakati wowote ule, kubeba bendera ya kidini, achilia mbali kuhubiri imani zake za kidini katika nchi ya kigeni.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.