Oktoba, 2009

Habari kutoka Oktoba, 2009

Trinidad & Tobago: Kampeni ya 350

  26 Oktoba 2009

“Trinidad na Tobago ni kisiwa tajiri na nchi inayoendelea tajiri kwa mafuta na gesi asilia. Lakini pia tunashuhudia madhara mabaya ya maendeleo ya haraka kwenye nyanja za viwanda katika visiwa vyetu. Hii ni fursa ya sauti za wanawake kusikika”: Attillah Springer anajihusisha na kampeni ya hali ya hewa 350.

Cambodia: Tuzo yamuenzi aliyenusurika na utumwa wa ngono

  26 Oktoba 2009

Sina Vann alikuwa na umri wa miaka 13 wakati alikupoja Cambodia kutoka Vietnam kwa kile kilichopaswa kuwa likizo. Badala yake, aliuzwa kama mtumwa kwa ajili ya ngono na alitumia miaka miwili iliyofuata ndani ya danguro. Alikombolewa wakati Somaly Mam, mwanaharakati wa kupinga utumwa na sura ya Taasisi ya Somaly Mam,...

Japan: Uchunguzi Mpya Juu ya Umaskini Waharibu Soga za Utajiri

  26 Oktoba 2009

Mjapani mmoja kati ya sita anaishi katika umasikini inasema ripoti mpya ya Wizara ya Ustawi wa Jamii [en]. Kwa mujibu wa takwimu za OECD, Japan ina kiwango kikubwa zaidi cha umasikini katika dunia iliyoendelea na ni ya 4 baada tu ya Mexico, Uturuki na Marekani. Mnamo mwezi wa Septemba, Makoto...

Bhutan: Mpito Usio na Mikwaruzo Kuelekea Demokrasi

  25 Oktoba 2009

Tshering Tobgay, kiongozi wa chama cha upinzani katika Bunge la Taifa la Bhutan, anatoa maoni kuwa: “mpito wetu kuelekea demokrasi, kwa hakika, umetukia bila mikwaruzo. Umetukia bila mikwaruzo kiasi kwamba wengi wetu walikuwa hata hawaufuatilii.”