Januari, 2011

Habari kutoka Januari, 2011

Kazakhstan: Wanablogu Wajadili Dini

  31 Januari 2011

Kwa kuwa Kazakhstan haina sera bayana ya dini, imekuwa ada kwamba kila mtu ana uhuru wa kuwa na mtazamo wake katika masuala ya kiimani. Kama ilivyokuwa miaka ishirini iliyopita, hakuna ambaye kwa hakika anajishughulisha na mitazamo hii lukuki ya kidini, ambayo inathibitishwa na mjadala kuhusu dini na desturi , ambayo...

Dunia ya Uarabu: “Acheni Kulia Juu Sudani”

  31 Januari 2011

Kura ya maoni kwa ajili ya uhuru wa Sudani ya Kusini leo imeiweka nchi hiyo kwenye uangalizi wa karibu miongoni mwa watumiaji wa twita wa Kiarabu. Kuanzia Saudi Arabia mpaka Palestina, watumiaji Twita wa Kiarabu wanajadiliana kuhusu mshikamano, kugawanyika na rasili mali za Sudani.

Syria: Propaganda ya Vyombo vya Habari vya Serikali Kuhusu Maandamano ya Tunisia na Misri

Mwanablogu wa ki-Syria Maurice Aaek amegundua[ar] kwamba vyombo vya habari vinavyoendeshwa na serikali nchini Syria vinachapisha habari za uongo na nusu-kweli kuhusu maandamano ya upinzani nchini Tunisia na Misri. Amegundua kwamba gazeti la Tishreen daily halikuweka sababu ambazo zilimfanya Ben Ali aondoke na kuwaachia watu wajitafsirie wenyewe, na kuwa gazeti...

Urusi: Mlipuko Katika Kiwanja cha Ndege cha Domodedovo

RuNet Echo  25 Januari 2011

Bomu lililipuka katika kiwanja cha ndege cha Domodedovo mjini Moscow, kwa uchache vifo vya kadri ya watu kumi vimeripotiwa. Mmiminiko wa Twita unapatikana hapa (RUS) na hapa (RUS, ENG). @ann_mint, ambaye anafanya kazi Domodedovo, alikuwa ni mmoja wa watumiaji wa kwanza wa Twita kuripoti juu ya mlipuko huo; “Kuna wahanga...

Kura ya Maoni ya Sudani Kusini 2011

Yaliyomo Habari Kusini mwa Sudan wakati Global Voices Habari zilizochaguliwa za Global Voices Rasilimali: Tovuti Twitter Facebook Videos Sudani Kusini ilianza kupiga kura ya maoni mnamo tarehe 9 Januari, 2011 ili kuamua kama waendelee kuwa sehemu ya Sudan kama sehemu ya Makubaliano ya Jumla ya Amani yaliyofanyika mwaka 2005 kati...