Sudani: Kura ya Maoni ya Sudani ya Kusini katika Picha

Kura ya maoni inaendelea kupigwa huko Kusini mwa Sudani tangu tarehe 9 mpaka 15 Januari 2011 kuamua iwapo sehemu hiyo ya kusini itaendelea kubaki kuwa sehemu ya Sudani ama iwe nchi huru inayojitegemea. Hizi ni picha zinazoweka kumbukumbu muhimu ya kihistoria ya kura hiyo ya maoni katika Sudani ya Kusini.

Tazama kidole changu:

Mwanamke katika Sudani ya Kusini akionyesha kidole chake kilichochonfywa wino. Picha kwa hisani ya Suleiman Abdullahi (http://upiu.com/)

Safari ndefu kwenda kupiga kura:

Safari ndefu kwenda kupiga kura: Picha kwa hisani ya Alun McDonald

Bendera mpya ya Sudani ya Kusini. Tafsiri ya rangi za bendera: Nyeusi – Rangi ya watu wa Sudani ya Kusini, Nyekundu – Damu iliyomwangwa kupigania uhuru, Kijani – Ardhi, Bluu – maji ya mto Naili, Nyota ya dhahabu, Umoja wa majimbo yaliyoko Sudani ya Kusini.

Bendera mpya ya Sudani ya Kusini. Picha kwa hisani ya Giulio Petrocca.

Subira ya muda mrefu ya uhuru:

Wapiga kura walisimama kwa masaa kadhaa kwenye foleni kwa uvumilivu. Picha kwa hisani ya Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji.

Ni wazi, Televisheni ya Sudani Kusini haiwezi kuandika Kiarabu kwa usahihi:

Runinga ya Sudani ya Kusini haiwezi kuandika neno “Piga kura sasa” kwa kiarabu: Hapa waliandika صويت badala ya صوت . Picha kwa hisani ya Sate3

Namna ya kuweka alama kwenye karatasi ya kura:

Namna ya kuweka alama kwenye karatasi ya upigaji kura ya maoni

Wakusubiri kupiga kura kwa ajili ya uhuru:

Wasudani ya Kusini wakisubiri kupiga kura kwa ajili ya kujipatia uhuru. Picha kwa hisani ya David McKenzie

Karatasi ya kupigia kura:

Karatasi ya kupigia kura ambayo Wasudani ya Kusini wanaitumia kupigia kura zao. Picha kwa hisani ya Usamah

Unaweza kuniletea kiti?:

Mistari ilikuwa mirefu. Watu walifika na viti vyao. Picha kwa hisani ya Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.