Sudani: Kura ya Maamuzi ya Uhuru wa Sudani Kusini kwenye Twita

Wapiga kura wa Sudani ya Kusini waliingia kwenye zoezi la upigaji kura leo kuamua ikiwa watajitenga ama kubakia kuwa sehemu ya Sudani. Huu hapa ni mkusanyiko wa habari zilizotawala kwenye Twita zinazohusiana na kura hiyo ya maoni. Unaweza kufuatilia habari za moja kwa moja kwa kutumia alama ya #SudanRef.

Alun McDonald amebaini kwamba salamu ya kawaida ya Kisudani imebadilishwa:

Inaonekana kama salamu ya kawaida ya Kisudani leo imegeuka kuwa, “Habari, umekwisha kupiga kura?” #SudanRef

“Upigaji kura unaendelea vizuri mpaka sasa,” anahabarisha Wandering Tracy:

Upigaji kura unaendelea vizuri mpaka sasa. Bila shaka siku baada ya upigaji kura na hata baada ya utangazaji wa matokeo zitakuwa nyakati za amani vile vile. #Sudanref #sudan

Ben amevutiwa na taadhima ya wapiga kura:

Ninavutiwa na umakini na taadhima ya wapiga kura inayojidhihirisha kwenye #Sudanref nje ya Khartoum. #Sudan

Wapiga kura wamejipanga kwenye foleni ndefu kwa masaa sita bila kulalamika, anasema Lindy Janssen:

Mtindo wenye utaratibu ambao kura hii ya maoni (#sudanref) inaendeshwa ni mzuri sana. Kwenye foleni ndefu kwa masaa sita sasa joto kali na hakuna malalamiko. #respect

Kuna mazingira na hisia nzuri ajabu kwenye vituo vya kupigia kura:

Foleni kwenye vituo vya kupigia kura ni ndefu sana, zinaenda taratibu na ni joto, lakini hakuna mtu anaonekana kujali. Hali ya ajabu. Wote wakipigia kura kujitenga “bila shaka” #SudanRef

Degner anajiuliza lipi litakuwa jina jipya la Sudani ya Kusini:

Kuna yeyote anayejua nchi hii mpya ya Sudani itapewa jina gani? Sudani Mpya, Sudani Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Magharibi ya Kati? #SudanRef

Mjukuu wa kike wa Waziri Mkuu wa zamani amekamatwa kwa kosa la kuandamana kupinga kura hiyo ya maoni:

Abeer Osman mjukuu wa Waziri Mkuu wa zamani Azhari alipelekwa kwenye kituo cha polisi kwa kwa kosa la kuandamana kupinga kura hiyo ya maoni ya Sudani.

Mwanamke ajuza anaimba, “Kwa heri Waarabu”:

Mwanamke ajuza akicheza nje ya kituo cha kupigia kura kwenye makumbusho ya Garang (Dr. John) akiimba “Kwa heri waarabu” #SudanRef

Mwanaume akilia kwa furaha kwenye kituo cha upigaji kura:

Mwanaume kwenye kituo cha kupigia kura akilia kilio cha furaha mara tu alipopiga kura. Mamia wakiwa kwenye mstari wakimpigia makofi na kumwonyeshea ishara inayooashiria kujitenga ya kuinua kidole gumba#SudanRef

Upigaji kura na nyimbo pamoja na maombi huko Marekani (Wasudani Kusini wanashiriki katika Kura ya Maoni katika nchi 8 duniani):

Upigaji kura unaanza kwa wimbo na maombi kwa lugha ya kiarabu kama ilivyoombwa na wapiga kura mjini Dallas. #SudanRef

Vijay anajiuliza inawezekanaje kura ya maoni ya Sudani ya Kusini kufananishwa na ile ya Timor Mashariki:

Ninashangaa namna kura ya maoni ya Sudani (#SudanRef) inavyofananishwa na Timor Mashariki. Swali kubwa, Je, mafuta yaliyoko Sudani ya Kusini yatayavutia makampuni ya Marekani na Uingereza na kuiondoa China? Je, amani itakuja?


Mpiga kura wa kwanza
huko Dallas, Texas;

Mpigaji kura wa kwanza mjini Dallas alikuwa mfanyakazi mzee wa upigaji kura, ambaye baada ya kutumbukiza karatasi yake ya kura kwenye sanduku, alinyanyua mkono wake na kupunga kwa ishara ya kuaga #SudanRef #Sudan

Je, sheria ya kiislaamu (Sharia) ni muhimu kuliko umoja?:

Alama mjini Khartoum: “Hakuna umoja kwa gharama ya sharia,” ikimaanisha Sharia ni muhimu kuliko Sudani iliyoungana. Hiyo inaogopesha wengi hapa. #sudanref

Mwisho, binti wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Sudani aliandamana kupinga kura hiyo ya maoni:

Binti wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Sudani huru alipeperusha bendera nusu mlingoti, alifunika kuta kwa kitambaa cheusi kuandamana #sudanref

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.