Syria: Propaganda ya Vyombo vya Habari vya Serikali Kuhusu Maandamano ya Tunisia na Misri

Mwanablogu wa ki-Syria Maurice Aaek amegundua[ar] kwamba vyombo vya habari vinavyoendeshwa na serikali nchini Syria vinachapisha habari za uongo na nusu-kweli kuhusu maandamano ya upinzani nchini Tunisia na Misri. Amegundua kwamba gazeti la Tishreen daily halikuweka sababu ambazo zilimfanya Ben Ali aondoke na kuwaachia watu wajitafsirie wenyewe, na kuwa gazeti la Al-Baath daily lilisema kwamba maandamano ya upinzani nchini Misri yana nia ya kutaka balozi wa Izraeli afukuzwe, na kutoyaweka kabisa madai ya kutaka Mubarak ang'atuke.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.