Kazakhstan: Wanablogu Wajadili Dini

Kwa kuwa Kazakhstan haina sera bayana ya dini, imekuwa ada kwamba kila mtu ana uhuru wa kuwa na mtazamo wake katika masuala ya kiimani. Kama ilivyokuwa miaka ishirini iliyopita, hakuna ambaye kwa hakika anajishughulisha na mitazamo hii lukuki ya kidini, ambayo inathibitishwa na mjadala kuhusu dini na desturi , ambayo hivi karibuni ililipuka miongoni mwa wanablogu.

Mjadala uliwashwa na ngoma ya Kara Zhorga , ambayo imekuwa maarufu katika nchi hiyo katika miaka michache iliyopita.

Urimtal anaandika [kaz]: “Nadhani Kara Zhorga si ngoma tu, bali jambo ambalo limeliunganisha taifa. Hata Wakazakh wanaoishi ughaibuni wanashiriki. Wakati serikali yetu inapowaelezea raia wake waishio ughaibuni katika namna isiyowapamba, Kara Zhorga ni aina ya jibu kwa ukosoaji wa aina hiyo.”

Orken aliandika makala juu ya mada hiyo [kaz]:

““Hebu tuseme ngoma hii ina asili ya Kimongolia au utamaduni wa Kalmyki, lakini sisi ndio tuliifanya kuwa alama ya Kitaifa. Wamongolia, Wachina na Wakalmyk hawakuikana kwa namna yoyote. Hii ndio sababu nadhani ni dalili za ujinga kwamba wengi wetu tuna kumbukumbu fupi linapokuja suala la desturi au hata kuuleta Uislamu kama nguvu ya kuupinga.”

Mwaka 2011, Wakazakhtan wataongoza Mkutano wa Umoja wa Kiislamu. Lakini bado kulikuwa na mjadala [kaz] si muda mrefu uliopita kuhusu “ “sheria iwezekanayo ambayo ingepiga marufuku kuvaa vitambaa vya kufunika kichwa yaani hijab .” Malimetter.org inathibitisha taarifa , au kusema, naibu Waziri wa Elimu na Sayansi Mahmetkali Sarbyev anafanya hivyo[kaz]:

“ Kazakhstani ni nchi yenyewe watu wa imani nyingi. Kama tukiruhusu watu kuvaa hijab, basi kesho wanafunzi thelathini katika darasa moja watajitokeza wamevaa kitu tofauti –na hiyo haitasababisha chochote chema,” anaeleza.

Timurr anaandika kwamba sheria itakuwa kinyume na katiba, kwa sababu katiba inalinda uhuru wa kudhihirisha imani za kidini wazi wazi [kaz]:

“Kwa kutazama kila kinachotokea sasa hivi, sidhani kama maafisa wetu na Mawaziri hawana habari kwamba wanaenda kinyume cha sheria. Lakini, kama hivi ndivyo ilivyo, kwa nini wanafanya hivyo?”

Makala ya awali ilichapishwa kwenye neweurasia.net

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.