Habari Kuu kutoka Mei 2011
Habari kutoka Mei, 2011
Ripoti ya UNESCO kuhusu vyombo vya habari vya Singapore
Repoti ya Unesco inaonesha ‘udhibiti wa hali juu’ wa vyombo vikuu vya habari nchini Singapore huku ikizitambua blogu na tovuti za vyombo vyauanahabari mpya kuwa vinatoa “mazungumzo makini mbadala juu ya masuala muhimu ya kisiasa na jamii kama vile siasa za ndani ya nchi, haki za mashoga na wazee.”
Singapore: Wanablogu Waikosoa Ilani ya PAP
Chama kinachotawala Singapore, People’s Action Party (PAP), kilitoa ilani yake ya uchaguzi tarehe 17 aprili, 2011, ambayo mara moja ilikosolewa na wanablogu wengi kwa “kutokuwa wazi”. PAP tayari kimekuwa madarakani kwa miongo mitano. Uchaguzi mkuu nchini humo umefanyika tarehe 7 Mei.
Nepal: Mwanzo wa Mapinduzi ya Facebook?
Pradeep Kumar Singh anaweka picha na habari za kampeni ya hivi karibu ni ya Facebook iliyopewa jina la “Jitokeze. Simama. Ongea. Vinginevyo, kaa kimya. Takriban vijana 400 wa Nepali walijitokeza sehemu ya Maitighar Mandala tarehe 8 Mei, 2011 na kudai katiba mpya.
Pakistani: ISI Walikuwa Wanafahamu Nini Kuhusu Laden?
Faheem Haider katika blogu ya Sera ya Nchi za Nje ya Pakistani anahoji kile ambacho Jeshi na Usalama wa Taifa (shirika la kijasusi) la Pakistani vilikuwa vinafahamu kuhusu gaidi mkuu Osama Bin Laden, ambaye aliingiliwa na kuuwawa huko Abbottabad, karibu na mji mkuu wa Pakistani.
Naijeria: Gavana wa Kinaijeria Kwenye Twita
Gavana wa Kinaijeria Kayode Fayemi yumo kwenye Twita, mwanablogu wa Naijeria Lord Banks anaripoti.
Uganda: Wananchi Wakasirishwa na Kukamatwa Kikatili kwa Kiongozi wa Upinzani
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dk.Kiiza Besigye alikamatwa tena katika mji mkuu wa Kampala kutokana na kushiriki kwake katika Kampeni ya Kutembea Kwenda Kazini usiku mmoja baada ya kuachiwa huru kwa dhamana. Besigye alipewa dhamana kwa sharti kuwa asijihusishe na kampeni ambayo imeuweka utawala wa Uganda kwenye vichwa vya habari kwa majuma matatu sasa.
Msumbiji: Polisi Washambulia Waandamanaji
Siku ya tarehe 6 Aprili, maofisa wa tawi la Polisi wa jamhuri ya msumbiji (PRM) – Kikosi cha Askari Maalum wa Dharura (FIR) – walitumia nguvukusitisha maandamano ya wafanyakazi wa shirika binafsi la ulinzi Group Four Security (G4S). Kwenye Facebook, wanamtandao walionesha kuchukizwa kwao kutokana na vitendo hivyo vya kikatili na kuhoji wajibu wa polisi, sheria na haki za binadamu.