Disemba, 2009

Habari kutoka Disemba, 2009

Je, China Iliharibu Makubaliano ya Copenhagen?

  30 Disemba 2009

Uln alijaribu kuchambua ni nini kilichotokea Copenhagen na kuhoji kwa nini nchi zinazoendelea hazikusaini baina yao wenyewe makubaliano ya kupunguza utokaji wa gesi ya ukaa. Inside-Out China ametafsiri taarifa inayosimulia habari kutoka kwa walio ndani kuhusu mienendo ya Wen Jiabao kule Copenhagen.

Msumbiji: Je, ni Lugha Ngapi Zinazungumzwa Nchini?

Kuna lugha 20 zinazozungumzwa nchini Msumbiji, kwa mujibu wa tovuti ya serikali, zaidi ya lugha ya serikali ya Kireno. Carlos Serra [pt] anajiuliza kama kuna lugha nyingine zaidi, kwa mujibu wa wataalamu wa lugha mashuhuri:”Kuna mtu aliniambia kuwa zipo kati ya 20 na 26; mwingine akaniambia zipo 17 zilizoandikwa na...

China na Iran: #CN4Iran

  28 Disemba 2009

Jana, maelfu ya Wa-Irani waliingia mitaani ili kupinga dhidi ya utawala wa kiimla. Maandamano hayo yaliwakumbusha watu wa China juu ya vuguvugu la demokrasi la Tiananmen la 1989 na watumiaji wa Ki-China wa twita wanatumia alama ya #cn4iran ili kuonyesha mshikamano na wenzao wa Irani.

Misitu ya Madagascar Inateketezwa kwa $460,000 kwa Siku

Wakati mataifa ya dunia yanakutana huko Copenhagen kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, Madagascar, ambayo imekwishapoteza 90% ya misitu yake ya asili, inakabiliwa na tishio la biashara ya magendo ya magogo, inayotishia kuharibu kile kilichobakia katika moja ya mifumo ya mazingira yenye viumbe na mimea mingi inayotofautiana.