Habari kutoka Disemba, 2009
China na Iran: #CN4Iran
Jana, maelfu ya Wa-Irani waliingia mitaani ili kupinga dhidi ya utawala wa kiimla. Maandamano hayo yaliwakumbusha watu wa China juu ya vuguvugu la demokrasi la Tiananmen la 1989 na watumiaji wa Ki-China wa twita wanatumia alama ya #cn4iran ili kuonyesha mshikamano na wenzao wa Irani.
Palestina/Gaza: Matayarisho ya Maandamano ya Uhuru Gaza
Ni kama wiki moja hivi mpaka Maandamano ya Uhuru Gaza yatakapoanza. Lengo lake ni kuonyesha mshikamano na Wapalestina na kuongeza ufahamu kuhusu vikwazo vinavyoizingira Gaza. Katharine Ganly anatazama baadhi ya matukio yaliyotokea katika maandalizi ya maandamano hayo.
Singapore: Kampeni ya “Kataa Ubakaji”
Nchini Singapore, mara nyingi kumbaka mke wako hakuchukuliwi kama tendo la kubaka. Waandaji wa kampeni ya “Kataa Ubakaji” wanataka kukomesha sheria inayokinga ubakaji ndani ya ndoa kwa kuzindua kampeni ya kukusanya saini ambazo zitawasilishwa kwa watunga sera. Wengi wa raia wa mtandaoni wanaiunga mkono kampeni hii.
Misitu ya Madagascar Inateketezwa kwa $460,000 kwa Siku
Wakati mataifa ya dunia yanakutana huko Copenhagen kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, Madagascar, ambayo imekwishapoteza 90% ya misitu yake ya asili, inakabiliwa na tishio la biashara ya magendo ya magogo, inayotishia kuharibu kile kilichobakia katika moja ya mifumo ya mazingira yenye viumbe na mimea mingi inayotofautiana.
Ethiopia: Meles Zenawi aisaliti Afrika
Lucas Liganga aandika kuhusu usaliti wa Waziri Mkuu wa Ethiopia: “kwa bahati mbaya, Waziri Mkuu wa Ethiopia meles Zenawi ambaye ni msemaji wa Afrika kuhusu mabadiliko ya tabianchi amejiunga na Ufaransa na kubadili nakala ya Afrika, jambo ambalo limewastua wajumbe wa Afrika.”
Morocco: Mwanablogu Mwingine Atupwa Gerezani
Mnamo tarehe 14 Desemba, siku ya Jumatatu, mwanablogu Bashir Hazzam na mmiliki wa mgahawa wa Intaneti Abdullah Boukhou walihukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa huyo wa kwanza na mwaka mmoja kwa huyo wa pili pamoja na kulipa faini ya MAD 500 (sawa na dola za Marekani 63) kila mmoja katika mahakama ya Goulmim.
Misri: Makao Makuu ya Kuzimu Duniani
Wanablogu na wanaharakati wengi wa Kimisri wamekuwa wakikamatwa na Usalama wa Taifa katika nyakati tafauti kwa sababu mbalimbali –za kweli au za bandia –Wa7da Masreya aliwahoji wanablogu mbalimbali na kuweka makala ya kina kuhusu mbinu za utesaji na hila za kisaikolojia ambazo wanablogu wale wamekuwa wakikumbana nazo kwenye makao makuu ya Usalama wa Taifa katika wilaya ya Jiji la Nasr.
China: Kujitoa Uhai kwa Msomi Mwingine tena – Kisa cha Yang Yuanyuan
YANG Yuanyuan, binti msomi mwenye miaka 30 aliyekuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Shanghai Maritime, alijinyonga kwenye bafu la nyumbani kwake mnamo Novemba 25 mwaka huu. Siku moja kabla hajachukua uamuzi huo alimwambia mama yake kwamba maarifa hayawezi kubadili majaaliwa. Miaka ya hivi karibuni imeshuhudia ongezeko la...
Canada Imesema Nini? Upotoshaji wa Habari Kwenye Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi
Serikali ya Canada inasemekana imetoa tamko la jazba leo, ikikanusha upotoshaji wa habari zinazodaiwa kufanywa nayo kwa mujibu wa Jarida la Wall Street likidai kwamba Canada imebadili sera yake na itakuwa ikikubaliana na malengo ya kupunguza hewa ya ukaa.
Urusi: Simulizi Tatu za Umaskini Uliokithiri
Mwandishi wa habari mpiga picha wa Urusi, Oleg Klimov, anatusimulia visa vitatu vya umaskini uliokithiri ambavyo alipata kusikia habari zake wakati akisubiri treni katika kituo cha treni cha Syzran, jiji lililo katika eneo la Samara la Urusi.