Mapendekezo kwa ajili ya Tuzo ya Kuvunja Mipaka yatafunguliwa leo (Disemba 29, 2009), hii ni tuzo mpya aliyoundwa na Google pamoja na Global Voices ili kuienzi miradi ya kwenye mtandao wa intaneti iliyoanzishwa na watu au vikundi ambavyo vinaonyesha ujasiri, ari na uwezo katika kutumia intaneti ili kukuza uhuru wa kujieleza. Tuzo hiyo pia inaungwa mkono na Thompson Reuters.
Tuzo ya Kuvunja Mipaka inaendeleza maadili yaliyowekwa katika Ilani ya Global Voices, ambayo iliandikwa kwa pamoja kwenye wiki mwaka 2004 ili kubainisha kanuni za kuiongoza asasi na jamii ambayo ilikuja kujulikana kama Global Voices. Ilani hiyo inaanza kwa maneno haya:
“Tunaamini katika uhuru wa maoni: katika kuilinda haki ya kuongea – haki ya kusikiliza. Tunaamini katika upatikanaji huru wa zana za kujieleza.
Ili kufikia lengo hilo, tunataka kumwezesha kila mmoja ambaye anataka kusema kuwa na njia za kusema – na kila mmoja anayetaka kusikiliza, awe na njia za kisikilizia kauli hizo.”
Tuzo ya Kuvunja Mipaka pia inaboresha kazi za Idara ya Utetezi ya Global Voices, ambayo iliundwa mwezi Februari 2007 ili kutilia mkazo kazi za asasi zinazohusiana na uhuru wa kujieleza.
Tuzo ya Kuvunja Mipaka iko wazi kwa watu wa kila taifa. Washindi watachaguliwa na jopo la wataalamu katika nyanja ya uhuru wa kujieleza. Zawadi ya dola 10,000 taslimu itatolewa katika kila moja ya maeneo haya:
1. Utetezi, itatolewa kwa mwanaharakati au kikundi ambacho kimetumia nyenzo za kwenye mtandao kukuza uhuru wa kujieleza au kuhamasisha mabadiliko ya kisiasa
2. Teknolojia, itatolewa kwa mtu au kikundi ambacho kimetengeneza nyenzo muhimu ambayo inawezesha uhuru wa kujieleza na kupanua upatikanaji wa habari
3. Sera, itatolewa kwa mtengeneza sera, ofisa wa serikali au kiongozi wa Asasi Isiyo ya Kiserikali ambaye ametoa mchango unaotambulika katika nyanja
Mapendekezo kwa ajili ya Tuzo ya kuvunja Mipaka yanaweza kuwasilishwa hapa http://www.breakingborders.net na zoezi litafungwa tarehe 15, Februari, 2010.