Misitu ya Madagascar Inateketezwa kwa $460,000 kwa Siku

Wakati mataifa ya dunia yanakutana leo huko Copenhagen kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, Madagascar, ambayo imekwishapoteza 90% ya misitu yake ya asili, inakabiliwa na tishio la biashara ya magendo ya magogo. Biashara haramu ya mbao ngumu zinazojulikana kama rosewood (miti iliyo katika kundi la mikwaju au mpingo), ni mada ya mazungumzo katika ulimwengu wa habari wa ki-malagasy kwa miezi michache sasa, na hivi sasa imewekwa wazi na timu ya wapelelezi kanzu. Maelezo ya kina ya biashara hii yenye faida yametolewa kwa ajili ya umma na yamepokewa na kushirikishwa na wanablogu wengi na majarida ya kisayansi. Taarifa ya karibuni zaidi imeandikwa na Global Witness panoja na Asasi ya Uchunguzi wa mazingira (EIA) inasema kwamba takriban magogo yenye thamani ya dola za Kimarekani 460, 000 hukatwa kila siku, huku juhudi za kudhibiti zikikwamishwa na kutokuwepo kwa serikali ya umoja. Taarifa kamili inapatikana hapa (na kwa lugha ya Kifaransa hapa).

Rosewood kupitia Achille52, at http://reflexiums.wordpress.com

Rosewood kupitia Achille52, at http://reflexiums.wordpress.com

Taarifa hiyo ina majina ya wahalifu na ukubwa wa biashara hiyo haramu

Mwanablogu wa ki-Malagasy Achille ananukuu kutoka kwenye taarifa hiyo (fr):

En 2009, huit navires porte-containers ont quitté Vohémar avec à leur bord un total de 19 730 rondins et 50 584 planches dans 324 containers autorisés par le MEF (voir Annexe 9). Cela revient à environ 9 700 tonnes de bois de rose.

Katika mwaka 2009, makontena manane yaliondoka kutoka bandari ya Vohemar yakiwa na magogo ya duara 19, 730 na magogo bapa ndani ya makontena 324 yaliyopewa kibali na MEF (angalia kielelezo 9). Hii ni sawa na tani 9700 za miti ya rosewood.

Video inayoonyesha maisha ya wanakijiji wanaoishi katika eneo hilo inaonyesha kuwa hawajanufaika kutokana na biashara hiyo ya rosewood:

Mtu akilinganisha dola za Kimarekani 460, 000 kwa siku zinazotokana na biashara hiyo na ukweli kuwa 89% ya wa-Malagasy wanaishi kwa chini ya dola 2 kwa siku, inakuwa rahisi kuelewa ni kwa nini ufisadi na kutokuwa na usawa vinachukuliwa kama vikwazo kwa maendeleo ya watu katika Madagascar.

Taarifa nyingine huru inaungwa mkono na Taasisi ya jane Goodall Schweiz ilichapishwa wiki hii na kuthibitisha upeo wa kile waandishi , Schuurman na Lowry, walichokiita “Mauaji ya Kimbari ya Rosewood nchini Madagascar” (pdf).

Waandishi hao pia walichangia video hii ili kuongeza ufahamu juu ya kupotezwa kwa bayoanuai kunakotokana na biashara hiyo:

Bungela Seneti la Marekani lilipitisha sheria kuhusu suala hili na mbunge wa Congres (Chama cha Demokrati – Oregon) http://blogs.nationalgeographic.com/blogs/news/chiefeditor/2009/11/us-house-condemns-madagascar-logging.html:

Baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Machi, serikali mpya dhaifu ya Andry rajoelina ilitoa amri za haraka zinazoruhusu uvunaji na usafirishaji nje wa magogo kutoka kwenye misitu inayohifadhiwa na maeneo ya Hifadhi za Historia Duniani. Serikali ya Obama imeshutumu serikali hiyo isiyo rasmi, na Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori, Mfuko wa Wanyamapori Duniani pamoja na Shirika la Conservation International yameshutumu vikali uvunaji wa jumla wa baadhi ya misitu yenye mimea mingi tofauti na kuteketezwa kwa nyenzo za maisha za watu wa eneo hilo

Suala hili la ufisadi wa rosewood hivi sasa unaathiri mchakato wa kisiasa nchini Madagascar. Rais wa zamani Albert Zafy ametishia kuyaweka wazi majina ya watu walio kwenye serikali ya sasa ya Rajoelina kama ufumbuzi wa kutatua mgogoro juu serikali ya pamoja ya taifa hautapatikana mapema. Ulazima wa kufikia serikali ya umoja wa kitaifa pia unashinikizwa na masharti ya wawekezaji wan je yaliyotolewa na Marekani (AGOA na MCC) kadhalika na Umoja wa Nchi za Ulaya (fr) (70% ya bajeti ya wa-Malagasy inatokana na misaada kutoka nje).

Jambo jingine, amri hii iliruhusu uchunguzi wa kisheria wa watengeneza magitaa, Gibsons Guitars. Makao yao makuu yalivamiwa na Shirika la Samaki na Wanyamapori la Marekani kwa kuwa magitaa yao yanatengenezwa kwa mbao za rosewood zinazotokana na biashara haramu huko Madagascar. Kwa kuangalia maoni ya watumiaji wa twita, kwamba Gibson guitars walihisishwa ni ukweli ambao ulisababisha maoni mengi zaidi kuliko kupotea kwa makazi pekee ya nyani mwenye mkia wa miaraba (ambaye anapatikana huko Madagascar pekee).

Suala la kupotea kwa misitu huko Madagascar kwa bahati mbaya haliishii kwenye biashara ya magogo ya rosewood. Kilimo cha kukata na kuchoma kimesababisha zaidi upoteaji wa misitu kunakotokana na vitendo vya binadamu. Asasi isiyo ya kiserikali Vakanala imetengeneza onyesho la pande 3 la moto katika misitu inayoiathiri Madagascar:

Picha kupitia http://vakanala.org

Picha kupitia http://vakanala.org

Vivyo hivyo, Asasi Isiyo ya Kiserikali, Mistinjo inaelekeza juhudi zake kwenye kujenga uwezo wa jamii za sehemu hiyo ambazo zinafanya kazi ya kupanda tena misitu na kuokoa gisi ya ukaa katika Andasibe.

Wanablogu wa sehemu hiyo wamekuwa wakielimisha umma juu ya kupotea kwa misitu ya mvua ya taifa kwa muda mrefu sasa. Lakini wanafanya zaidi ya ya kuelimisha umma, Patrick, mwanablogu kutoka Tamatave, amekuwa akipanda miti katika eneo la Toasmasina na amehusisha jumuiya nyingi katika mchakato huu:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.