Singapore: Kampeni ya “Kataa Ubakaji”

Nchini Singapore, kumbaka mke wako hakuchukuliwi kama tendo la kubaka.

Lakini inabidi lichukuliwe hivyo.

Huo ndio ujumbe mkuu wa kampeni ya “Kataa Ubakaji” ulichapishwa katika ukurasa wa Facebook wa kundi la wapiga kampeni. Waandaalizi wana nia ya kukomesha sheria inayokinga ubakaji ndani ya ndoa nchini Singapore.

Kampeni ya “Kataa Ubakaji” inatetea dhana moja rahisi: uvamizi au vurugu za ngono zinazofanywa na mtu yeyote, dhidi ya mtu yeyote, ni kosa la jinai. Kwa hiyo, uingiliaji kingono, bila kujali kama aliyetendwa au aliyetenda wameoana, kitendo hicho ni budi kichukuliwe kama ubakaji.

Kundi hilo limekwishakusanya zaidi ya saini 3000 kwa ajili ya kampeni ambazo zitawasilishwa kwa Waziri Mkuu.

Tunapenda kuwashukuru kila mmoja aliyeunga mkono kampeni ya “Kataa Ubakaji” ili kukomesha kinga kwa tendo la ubakaji ndani ya ndoa nchini Singapore. Dakika ishirini zilizopita, kampeni yetu imefikia kikomo ikiwa na zaidi ya saini 3,600.

Katika siku chache zijazo, tutakuwa tunaziweka pamoja takwimu tulizokusanya kabla ya kuziwasilisha kwa Waziri Mkuu wetu, Bw. Lee Hsien Loong, kwa njia ya barua pepe na katika nakala ya kawaida.

Barnyard Chorus anaona kuwa utamaduni wa ubakaji nchini Singapore ni jambo ambalo limetukamata kwa mshangao na kutusumbua wakati hatimaye lilipotokeza kichwa chake kisicho na haya, kinachochefua na chenye chuki dhidi ya wanawake.”

Syinc
anaunga mkono kampeni ya “Kataa Ubakaji”.

Hebu na tuangalie uso mmoja wa jinsi jambo hili lilivyo baya.

Wakati mtu asiyejulikana anapom’baka mtu mwingine asiyemjua, kuna uwezekano mkubwa kuwa hawataweza kuonana tena ana kwa ana.

Pale mume anapom’baka mke wake, wataendelea wanaonana kila siku. Kwa kweli, tendo hilo baya linawezekana sana kuendelea kutendwa. Pengine kila siku.

Pale mtu aliyeahidi kukupenda na kukulinda katika hali ngumu na nyepesi anapofanya tendo baya namna hii – huacha makovu yasiyofutika ndani ya mawazo ya mtu.

Jarida la The Temasek Review linafafanua kwa nini kampeni hii inamhusu kila mmoja.

Kampeni hii imewaleta pamoja wanawake na wanaume, vijana na wazee, watu wa rangi tofauti, waumini wa imani mbalimbali na wale wasio na imani yoyote. Bila kujali asili yako, sisi wote tuna maslahi katika hili. Kila mmoja anastahili kinga ya sheria dhidi ya vurugu, bila kujali ni nani anyefanya vurugu hiyo. Ubakaji ni kupiga, namna ya uonevu, ambao unafanyika kwa kupitia kiungo cha ngono badala ya ngumi.

Kampeni ya “Kataa Ubakaji” imetengeneza matangazo kadhaa yanayowataka watu wa Singapore kuunga mkono zoezi la kutia saini

Lakini raia wengine wa mtandaoni hawaiungi mkono kampeni hiyo. Toolang anatoa maoni kwenye blogu ya Raia wa kwenye Mtandao

Mwitiko dhaifu unaonyesha kuwa kama kila wanandoa wataiunga mkono kampeni na kufanya ubakaji ndani ya ndoa kuwa sheria, polisi watatingwa sana mwaka mzima na hawatakuwa na muda wa kuilinda Singapore salama dhidi ya jinai na ugaidi ila kuchunguza yale wanayofanya maelfu ya wanandoa kila usiku katika vitanda, kutathmini kama nguvu za ziada zilitumika dhidi ya mwanandoa mwenza. Na ikiwa nguvu za ziada zilitumika na kumaanisha ubakaji ndani ya ndoa, itawachukua polisi miezi kadhaa kuchunguza. Wakati huo huo, wanandoa hao wataafikiana na kuanza duru nyingine ya starehe kitandani ili kusuluhisha mgogoro na hawatataka kuendelea na kesi. Juhudi zote za polishi zitapotea bure. Ninawashauri watafiti waende mahakama kuu na mahakama ya familia na wafahamu fika matatizo ya familia na unyumba kwanza kabla ya kuanza kampeni hii.

Btan anaamini kuwa waandaaji walishindwa kukusanya saini za kutosha kwa sababu kampeni hiyo haiungwi mkono kwa dhati na umma

Waandaji wa kampeni ya kukusanya saini bado wamo kwenye hali ya kubisha. Uksefu wa saini hautokani na kukosekana kwa utangazaji au msukumo bali kwa sababu watu wengi wanafahamu kuwa kampeni hii ni ujinga na haina maana.

Wapiga kampeni ya kukusanya saini wanawatusi watu, hasa wanawake, kwa kuwa na dhana kwamba hawawezi kujiangalia wenyewe wakati wana uzito wote wa sheria nyuma yao.
Ni vyema wakielekeza nguvu zao kwenye masuala yanye uzito, kama vile kuanzisha mfumo wa vyama viwili vya kweli nchini Singapore ambapo wananchi hawatachapwa kama watumwa na ambapo wageni wanaingia kwa makundi makubwa na kupotosha moyo wa taifa.

Nyumba inaungua na wao wanahofia siku unayotoka bila kuchana nywele?

Wekeni vipaumbele vyenu sawa.

Kampeni ya “Kataa Ubakaji” pia ina akaunti ya Twita.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.