Mwanahabari-mwanablogu mkongwe anashtakiwa katika kesi ya kudhalilisha na mwanasiasa anayejulikana kwa kutetea uhuru wa habari nchini Malaysia.
Zaid Ibrahim, Waziri wa zamani katika Ofisi ya Waziri Mkuu, aliguswa vibaya na makala iliyoandikwa na A Kadir Jasin mwezi Oktoba uliopita. Mbali na kumshtaki mwanablogu huyo, Zaid anamtaka mwandishi aombe msamaha.
Kitu cha pekee katika shauri hili ni kwamba Zaid anajulikana kwa kuwaunga mkono wanablogu wa Kimalaysia ambao wameshtakiwa na watu wenye nguvu na mashirika. Zaid mwenyewe naye pia ni mwanablogu. Na kwa kweli, alipiinga makala “inayoshambulia vibaya” iliyoandikwa na Jasin katika blogu yake mwenyewe.
Rocky's Bru anashangaa kwamba hivi sasa Zaid ni sehemu ya kundi la watu wenye nafasi ya juu ambao wanawashtaki wanablogu.
Siwezi kuelezea jinsi gani Zaid Ibrahim ambaye wakati fulani alielezewa kama “mtu mwenye maamuzi machachari”, amekwenda chini katika njia hii.
Sasa Zaid amejiunga na msululu wa watu wenye ushawishi na matajiri ambao wanawashtaki wanablogu.
Kwa kitendo chake hiki kipya zaidi ya vyote, sitaki tena kumuelezea Zaid kama “mtu mwenye maamuzi machachari”. Mtu mwenye maamuzi machachari ni mtu wa aina ya pekee, mtu ambaye anathubutu kwenda kinyume cha mkondo, mtu unayemheshimu – hata kwa manung’uniko – kutokana na kanuni au misimamo yake.
Mat Cendana anahofia kuwa kesi hii inaweza kusababisha kesi nyingine zaidi za udhalilishaji nchini Malaysia.
Kwa maoni yangu, makala hii, huku kwa hakika haimpambi Zaid, haipo kwenye “hadhi ya saman”, kama hii itaamuliwa kama shauri la madai, basi tutashuhudia kesi kama 10 hivi zitakazoandikishwa mahakamani kila siku!
Jebat anahoji msingi wa kusajili shauri hili:
Ni kipi kina ubaya katika makala ambacho kimemfanya atoe tamko la kumuita mahakani Kadir Jasin?
Je kuna chembe yoyote ya udhalilishaji ndani yake? Je Zaid kadhalika hakuandika matamko ya madai yanayomhusu Kadir Jasin katika makala yake ya kujibu?
Kwa hiyo, suala tat ani lipi? Mashabiki wote wa Pakatan Rakyat wanamuunga mkono Zaid Ibrahim. Ni nani anayejali ikiwa makala moja hasi ilichapishwa katika ulimwengu wa blogu?
Unataka kusema, watu hawawezi kuandika chochote wanachotaka? Tangu lini?
Wakati yeye na wanablogu wote wa upinzani wanapoandika idadi kubwa ya madai yasiyo na haki na makala zisizo na ustaarabu zinazowapaka matope wengine wote, ni sawa. Lakini mtu anapokabiliwa na mzimu wa kale, anakereka na kushindwa kulala vizuri.
Jambo la kinyume ni kuwa, anapenda kuonekana kama mtu mwenye mawazo huru na mpiganiaji wa uhuru wa habari na wa kujieleza.
Hata hivyo, ni hali yake kuwashtaki watu kama vile ilivyo haki ya Kadir Jasin kuandika makala ile. Sio kama walivyo watu wengine ambao hukimbia kama waoga, nina hakika Kadir Jasin atachukua hatua zote zinazotakiwa za sheria ili kuitetea makala yake katika msingi wa ushahidi atakaoweza kuutoa.
Katika bigdogdotcom, mwandishi anasikitishwa na kwamba Zaid anatumia kesi hii kupata faida kwenye siasa na kwenye vyombo vya habari
Kitu anachokitaka Zaid hakipo wazi. Wazi, tangu ajiunge na PKR, Zaidi sasa ameambukizwa vikali “Ugonjwa wa Suti” ambao mtu mwingine pekee ni Aliyekuwa-Mtumiaji-Vibaya-wa-Madaraka Anwar “”Mfalme wa Zulia La Ngozi” Ibrahim anayesumbuliwa nao.
Sasa Zaid ameambukizwa vikali ugonjwa wa kukosakutiliwamaanani.
Ni umbali gani ambao Zaid anaweza kwenda pia ni jambo ambalo halipo wazi. Wazi, alihitaji sarakasi ya vyombo vya habari na sheria ili kujipa “umuhimu” ili aweze kuonekana.