Ecuador: Serikali Yaifungia Idhaa ya Televisheni ya Teleamazonas

Mnamo Disemba 22, Idhaa ya televisheni ya Ecuador Teleamazonas iliondolewa hewani na Msimamizi wa Mawasiliano [es], chini ya sheria ya kufungiwa kwa muda wa masaa 72. Teleamazonas ni idhaa ambayo ina wasifu wa kuwa idhaa ambayo haifuati msimamo rasmi wa serikali. Katika miaka 3, imeweza kushikilia tofauti kati yake na utawala wa Rais Rafael Correa, ambayo mara nyingi imetoa wito wa kufungwa kwa idhaa hiyo.

Msimamizi wa Mawasiliano alihalalisha kufungwa kwa idhaa hiyo kwa sababu ya matukio ya tarehe 22 Mei, 2009, ambapo ilisambaza habari zilizotokana na dhana kuwa uchimbaji wa mafuta kwenye kisiwa cha Puna kungewaathiri wakazi wa kisiwa hicho, ambao wanapata kipato chao kutokana uvuvi. Kwa mujibu wa Msimamizi, kutokana kusambaza habari hizo, Teleamazonas ilikiuka kifungu 18, namba 1 cha katiba ya sasa ambayo inaweka haki ya watu wote “kutafuta, kupokea, kubadilishana, kutengeneza na kusambaza habari, zilizothibitishwa, katika muda muafaka, zenye vyanzo mablimbali na tofauti tofauti, ambazo hazijachujwa pamoja na matukio yenye maslahi ya jumla kunaambatana na wajibu ambao haujulikani.”

Mara baada, kulikuwa na sauti za upinzani kutoka nyanja tofauti nchini Ecuador, ambazo zinaandaa maandamano na upinzani dhidi ya hatua hiyo. Kwa wengi hili ni shambulio dhidi ya uhuru wa kujieleza. Tukio hili la hivi karibuni pia lina umuhimu wakati ambao Bunge la Taifa linajadili Sheria Mpya za Mawasiliano, ambayo ilitangazwa baada ya kuvunja makubaliano yaliyopita kati ya wabunge wa chama cha serikali na wale wa upinzani.

Pia kuna maoni kwenye mtandao yanaounga mkono na yale yanayopinga hatua hii. Kwa wengi, kufungwa kwa idhaa ya televisheni ni shambulio la wazi kwa vyombo huru vya habari na pia ni kitendo cha kutishia. Kwa Xica wa blogu ya La Alharaca [es]:

Por más de que el gobierno ecuatoriano haya decidido sacar del aire a Teleamazonas por solo 3 días, esto es suficiente para enviar un fuerte mensaje a los demás medios y a los asambleístas: podemos cerrar un medio y no necesitamos la ley de comunicación para hacerlo.

Kwamba serikali ya Ecuador imeamua kuiondoa hewani Teleamazonas kwa muda wa siku tatu, kunachotosha kutuma ujumbe mkali kwa vyombo vingine vya habari na kwa wabunge: tunaweza kufunga idhaa ya habari na hatuhitaji sheria ya habari kufanya hivyo.

Msimamo wa wahariri wa teleamazonas, ambao unaipinga serikali, pia una maadui, na mtangazaji wa habari nyingi Jorge Ortiz ni kiongozi anayeonekana, ambaye kila mara hutoa maoni yanayong’ata dhidi ya serikali. Na kwa nyongeza, ukweli kwamba idhaa hiyo inamilikiwa na mmiliki wa benki Fidel Egas pia unasababisha mashaka kuhusu kutokuwa na upendeleo pamoja na kutofungamana kwake na upande wowote. Kuhusu hili, Eduardo Varas wa blogu ya Más Libros, Autores y Otros Riesgos [es] anaandika:

Aplaudir que sea el Ejecutivo el llamado a prohibir opiniones o a definir lo que es o no una profesión es un acto de lo crueles que confunden todo y no les importa. Todos debemos tener la libertad de decir lo que quisiéramos, así seamos un medio con todo el dinero del mundo y con un dueño que se crea el portador de la verdad, o un presidente que también se crea dueño a la verdad, o un gil como yo, o giles que celebran lo cierres de medios como maniobras justas. Todos.

Kushangilia kuwa ni upande wa Utawala ambao unataka kuzuia maoni au kubainisha ni nini au kipi kisicho taaluma ni tendo la kikatili ambalo linachanganya kila kitu na halina umuhimu kwao. Sisi sote tunapaswa kuwa na uhuru wa kusema kitu tunachotaka, ikiwa ni chombo cha habari chenye pes azote duniani na kilicho na mmiliki ambaye anajifikiria kuwa ni njia ya kutoa ukweli, au rais ambaye pia anajifikiria kuwa ni mmiliki wa ukweli, au mjinga kama mimi, au wajinga wanaoshangilia kufungwa kwa idhaa ya habari kama mbinu sawia. Kila mmoja wetu.

Kufungwa huko tayari kumeshahitimishwa na inasubiriwa kuona ikiwa kitendo hicho kitaathiri Sheria ya Mawasiliano ambayo hivi sasa inajadiliwa katika Bunge la taifa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.