Habari kutoka 29 Disemba 2009
Malaysia: Mtetezi wa Uhuru wa Vyombo vya Habari Amshtaki Mwanablogu
Mwanahabari-mwanablogu mkongwe anashtakiwa katika kesi ya madai na mwanasiasa anayejulikana kwa kutetea uhuru wa habari nchini Malaysia. Angalia maoni ya wanablogu wa Malaysia.
Rwanda: Video za Wanaojitolea
Mfululizo wa video zilizopakiwa na mtumiaji kdarpa kwenye YouTube, zinaonyesha wafanyakazi wa kujitolea na watu waliokutana nao wakiwa safarini nchini Rwanda ambapo walifanya kazi na jamii za sehemu hiyo.
Uganda: Rais Kuzuia Muswada Unaopinga Ushoga
Muswada Unaopinga Ushoga wa 2009 uliopendekezwa nchini Uganda bado unasubiri uamuzi wa mwisho utakaotolewa na bunge la nchi hiyo, lakini gazeti la Daily Monitor lilitaarifu Jumatano kuwa Rais Yoweri Museveni ameihakikishia Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani nia yake ya kuukwamisha muswada huo
Ecuador: Serikali Yaifungia Idhaa ya Televisheni ya Teleamazonas
Serikali ya Ecuador iliiondoa idhaa ya televisheni ya teleamazonas kwa masaa 72 kwa kusambaza habari za uongo. Wakosoaji wanaona kuwa hatua hii ni tishio kwa uhuru wa kujieleza.
Podikasti: Mahojiano na Sudanese Drima
Sudanese Drima ni jina la bandia la mwandishi wa Kisudani wa Global Voices anayeishi nchini Malaysia. Katika mahojiano haya ya dakika kumi tunajadili jinsi uanahabari wa kijamii unavyoathiri Uislamu, mgogoro wa dafur, na masuala ya nafsi ya Uafrika-Uarabu katika Asia ya Kusini Mashariki.