Raia wa Myanmar Wachukizwa na Mashambulizi Dhidi ya Wahamiaji Wenzao Nchini Malasia.

Vurugu za kikabila nchini Mynmar inaonekana kusambaa hata katika nchi za jirani.

Baadhi ya wahamiaji wa Mynmar wa jamii ya budha wanaoishi nchini Malasia wiki chache zilizopita walishambuliwa tukio ambalo wengi wanaamini kuwa tukio hilo linahusiana na mvutano wa kimakabila na kidini unaoendelea nchini Mynmar. Kwa mujibu wa Eleven Media, watu 6 walifariki na wengine 12 walikimbizwa hospitalini kutoka na majeraha waliyoyapata wakati wa mashambulizi makali yaliyotokea kati ya Mei 30 na Juni 8 dhidi ya raia wa Mynamar wanaoishi nchini Malasia.

Ubalozi wa Myanmar nchini Malasia mapema ilitoa habari ambazo ziliwaghadhabisha sana watumiaji wengi wa mtandao wenye utaifa wa Mynmar. Ye Htut, ambaye ni naibu wa Waziri katika Wizara ya Mawasiliano alifafanua[ yangu] taarifa hiyo:

(Sisi) tulisoma habari hiyo katika mtandao wa intaneti kuhusiana na vurugu karibu na nyumba ya watawa huko KamPung pamoja na Selayang na kwamba baadhi ya watu wa Mynmar walipoteza maisha. Mara moja, tuliuuliza ubalozi wa Mynmar huko Malasia kuhusiana na tukio hilo mapema majira ya saa 11 jioni na tuliwauliza tena saa saa 2 usiku kupitia Wizara ya Mambo ya ndani. Balozi alituambia kuwa habari hizi zilikuwa ni za uongo […]

A Myanmar national put 11 red roses at Malaysia Embassy Yangon for Myanmar nationals killed at Malaysia.

Raia wa Myanmar akiweka maua waridi ya rangi nyekundu 11 mbele ya Ubalozi wa Malasia hukoYangon kwa heshima ya raia wa Mynmar waliouawa huko Malasia. Picha – Ukurasa wa Facebook wa Ye Moe.

Wai Lin Oo alionesha [my] kusikitishwa kwake na majibu ya Ubalozi:

Ni dhahiri kuwa kuna matukio haya! Kama unataka kuthibitisha maneno ya ubalozi, andaa safari ya kwenda Mynmar kuchukua miili ya watu waliopoteza maisha.

Fang Ran alikazia nilichotangulia kukisema.

Watu wanateseka. Ni wadanganyaji tu ambao hata hawezi ktoka nje ya ubalozi. Na wanatutoza kodi kubwa. Siwezi hata kutamka kwa jinsi ambavyo mara nyingi wamekuwa wakiwakaripia (raia ambao hufika hapo ubalozini kwa lengo la kutafuta usalama)[…] Ni lini tutaweza kuitegemea serikali ya Mynmar? Kwa kweli inakatisha tamaa sana. Heshima ya usawa wa haki za binadamu kwa watu wa Myanmar iko wapi? blockquote>
Myo Set alilinganisha namna serikali nyingine wanavyokabiliana na hali kama hizi zinazolikumba taifa la Mynamar:

Mjapani mmoja alipouawa nchini Mynmar mwaka 2007, waziri wa Japani aliiingilia kati mara moja. Pale wafanyakazi wa Mynmar walipokuwa na kutokuelewana na Mkorea mmoja ambaye alikuwa ni mmiliki wa kiwanda fulani, Ubalozi wa Korea mara moja uliingilia kati shauri hilo. Korea ya Kaskazini waliviondoa vitabu vya Kim Jong wa III haraka sana kutoka katika maktaba mbalimbali nchini Myanmar. Nni aibu gani hii! Marekani walifika haraka Myanmar pale tu lilipotokea suala laYettaw.

Msimamo wetu?

Huko Malasia, mdomo wa Balozi ulipatwa na ganzi. Wizara ya Mawasiliano imepatwa na kilema na serikali ya Myanmar imepooza.

Sisi ni Raia wa Barma , ukurasa wa jumuia ya raia wa Myanmar waishio pande zote za dunia ulihoji ukimya wa mashirika binafsi na vyombo vya habari kufuatia udhalilishaji wanaokabiliana nao watu wa jamii ya budha nchini Malasia:

Wakati vurugu zilipotokea huko katika mji wa Meikhtilar nchini Myanmar, vyombo vya habari vya kimataifa na mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Kimataifa, shirika la Haki za Binadamu yaliripoti matukio haya na pia baadhi yao walipotosha hali halisi ya mambo, wengine wakisema ni mpango wa kufutilia mbali makabila fulani, mauaji ya halaiki, waislamu ya Myanmar wanauawa kikatili na mambo vyanayofanana na hayo….. lakini ni kwa nini kumekuwa na ukimya uliopitiliza kuhusiana na mauaji ya kikatili yaliyotokea nchini Malasia yanayowalenga wabudha wa Myanmar. Wabudha wa Myanmar wajitoe mhanga kwa kiasi gani ili hali wanayokabiliana nayo ifahamike na kuchukuliwa hatua stahiki? Tafadhali onesha kile kinachofahamika kama HAKI ambacho kila mmoja wenu amekuwa akikitumia popote uonapo wabudha wa Myanmar wakifedheheshwa popote pale katika maandiko au kwa picha

Mapema Juni 4, kadiri hali hii ilivyozidi kupigiwa kelele, mashambulizi nayo ndivyo nayo yalivyozidi kushika kasi, Serikali ya Myanmar ilitoa tamko la kidiplomasia kwa balozi wa Malasia nchini Myanmar likiitaka serikali ya Malasia kufanyia uchunguzi matuko haya haraka iwezekanavyo na kuwachukulia hatua za kisheria watu wote watakaohusika na matukio haya. Manamo tarehe 6 Juni, serikali ya Malaysia ilitaarifu kuwa raia 900 wa Myanmar walishikiliwa wakati wa msako wa kiulinzi. Serikali ya Myanmar inajiandaa kupeleka jopo la wataalam nchini Malasia.

Kwa kuwa baadhi ya wahamiaji wa Myanmar hawezi kumudu gharama za matibabu, Timu ya Huduma za bure za Mazishi ya Kampung nchini Malasia (Kampung FFSS) ilitoa msaada kwa wahanga. U Aung Ko Win, ambaye ni Rais wa Benki ya Kanbawza ambaye pia ni mmiliki wa Shirika la Ndege la Kimataifa la Myanmar (MAI) alichangia dola za Kimarekani 50,000 na kutoa tiketi za ndege kwa punguzo la asilimia 50 kwa safari ya Malasia-Myanmar ili kuwarahisishia wahamiaji wote wanaotaka kurudi nchini Myanmar. Tajiri mwingine mashuhuri sana, U Zaw Zaw, ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka la Myanmar alitangaza kuwa atachangia tiketi 1,000 za ndege kwa wote wanaohitaji kurudi nchini Myanmar, pamoja na kuchangia dola za kimarekani 20,000 Kampung FFSS.

Watumiaji wengi wa mtandao katika mtandao wa Facebook walibadilisha picha zao na katika taarifa zao na kuweka picha nyeusi kuomboleza vifo ya raia wa Myanmar vilivyotokea huko Malasia.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.