[ Viungo vyote vinaelekeza kwenye makala zilizo katika lugha ya Kireno]
Maandamano ya nne ya Harakati za Kudai Usafiri wa Bure , yaliyotokea Alhamisi ya tarehe 13 Juni huko São Paulo lilikabiliwa na upinzani kutoka kwa polisi waliokuwa wakinyunyiza maji ya pilipili, risasi za plastiki na mabomu ya machozi. Kwa mujibu wa habari za hivi karibuni, takribani watu 235 walikamatwa wakati wa maandamano hayo.
Takribani waandamanaji elfu tano walikusanyika mbele ya uwanja wa Halmashauri ya Jiji kama sehemu ya maandamano yanayoendelea ya kupinga ongezeko la nauli kutoka 3.00 BRL (dola za Marekani 1.40) hadi 3.20 BRL (dola za Marekani 1.50). Maandamano yamekuwa yakiendelea tangu Juni 6 kufuatia nauli mpya zilizoanza kutumika siku nne zilizopita. Jambo hili tayari limeenea na yanafuatiliwa kimataifa
Harakati hizi zimekuwa zikitumia ukurasa wa Facebook kuhamasisha kiasi kwamba, maandamano mengine yalifuata katika majiji mengine ya Brazil ambayo pia yanapinga ongezeko la nauli kwa usafiri wa umma. Waandishi wa habari pamoja na viongozi wa kisiasa wamekuwa wakijadiliana kwenye vyombo vya habari vya nchini humo kuhusiana na uongezekaji wa nauli, wakati kwa upande mwingine, raia wao wamekuwa wakitoa maoni yao kupitia mtandao wa intaneti. Waandamanaji ambao wamekuwa wakikabiliana na ukatili kutoka kwa polisi wakati wa maandamano, Gavana Geraldo Alckmin aliwaita “wahuni” na Meya Fernando Haddad (ambaye kwa sasa yupo jijini Paris) alikosa vitendo vyao. Hata hivyo, serikali kuu pamoja na mamlaka za majiji walionesha msimamo wao kwa kusisitiza kutokubadili ongezeko hilo la nauli.
Video hapa chini inaonesha polisi wakiwashambulia waandishi wa vyombo vya habari.
Sao Paulo
Waandamanaji pembezoni mwa mtaa wa Consolação wanaweza kuonekana kwenye kipande cha filamu kilichopatikana kutoka kwenye kamera za ulinzi zinazomulika mtaa ya miji , na iliwezekana kutazama moja kwa moja maandamano katika mtaa wa Consolação.
Tovuti ya O que não sai na tv (Kile wasichokionesha kwenye Televisheni) inafuatilia maandamano na kupakia matukio kwa muda yanapotokea.
Rio De Janeiro
Pilipili dhidi ya Siki
Watumiaji wa mtandao wa nchini Brazil katika mtandao wa Twita wanapinga ongezeko la nauli kupitia kiungo ishara #pimentavsvinagre ( pilipili dhidi ya Siki). Maneno haya yanatokana na udhalilishaji wa polisi wa unyunyizaji wa maji ya kuwasha pamoja na nguo zilizolowanishwa kwa siki au leso ambazo waandamanaji walizitumia kuzuia wasiathiriwe na matumizi ya vitu hivyo.
Kiungo ishara kingine kilichoshika kasi kilikuwa ni #Consolação, jina la mtaa ambao ndio maandamano yalipofanyikia
Mkazi wa Sao Paulo, Gabriela Reimberg (@gabyreimberg) alitwiti:
@gabyreimberg: Brasil mostra a tua cara #pimentavsvinagre
@gabyreimberg:Brazil, jioneshe mwenyewe #peppervsvinegar
Wakala wa Matangazo, Luis Salsicha (@LuisSalsicha) alisema:
@LuisSalsicha: e que esses manifestos não parem por aqui… hora de mostrar de quem é esse país! #pimentavsvinagre
@gabyreimberg: Matumaini yangu ni kuwa maandamano haya hayataishia hapa, ni muda muafaka wa ulimwengu kuifahamu vyema nchi hii! #peppervsvinegar
Mwanablogu Rafael Takano (@telefone) aliweka maoni yake:
@telefone: Bombas em direção de fotógrafos e do posto de gasolina no cruzamento entre consolação e Maria Antônia. Agora mais… http://fb.me/2SpxemWOX
@telefone: Mabomu yanatupwa kwa wapiga picha na kurushwa katika kituo cha gesi kilichopo katika njia panda ya mitaa ya Consolação na Maria Antonia. Na sasa, zaidi…http://fb.me/2SpxemWOX
Watu wa Brazil wanaweka Passe Livre SP maoni katika ukurasa wa Facebook ujulikanao kama Nauli Bure kama sehemu ya maandamano kupitia mtandao wa intaneti ya kupinga ongezeko la nauli. Makala za tukio hili katika mitandao ya kijamii imekuwa ikichangiwa na wastani wa watumiaji wa mtandao 1000 kwa kila makala, kama hii hapa inayoshinikiza maandamano ya tano siku ya Jumatatu, Juni 17.
Kwa ushirikiano na Luis Henrique. Imehakikiwa na Melissa Mann
[ Viungo vyote vinaelekeza kwenye makala zilizo katika lugha ya Kireno]