Martinique: Uchaguzi, utata na kugomea uchaguzi

Jumapili ya tarehe 14 Machi, raia wote wa Ufaransa wakiwemo wale wa idara za ng’ambo za Ufaransa (Martinique, Guadeloupe, French Guiana na Reunion) walitakiwa kupiga kura za majimbo na bunge la majimbo lenye madaraka katika majimbo hayo kama vile katika mipango ya mafunzo ya watu wazima, ujenzi na bajeti za shule za sekondari za umma, na kutoa fedha kwa miradi ya kukuza utamaduni.

Upigaji kura ulifanywa katika kipindi chenye hekaheka za uchaguzi: Watu wa Martinique walitakiwa kuamua kama wanataka uhuru zaidi katika idara yao, mwezi Januari tu.

Chaguzi mbili kubwa katika kipindi cha miezi mitatu zingeweza kuwa ni shughuli nzito kwa 55.55% ya wapiga kura wa ki-Martinique ambao waliamua kukaa nyumbani na kutopiga kura, kama inavyoonyeshwa katika makala ya Bondamanjak [Fr].

Mwanablogu Evolution Martinique anatoa maoni juu [Fr] ya idadi kubwa ya watu ambao hawakufika (kupiga kura):

Le grand vainqueur de ce 1er tour, est à l’évidence le taux record d’abstention (plus de 55%) […].

Mshindi wa duru la kwanza ni idadi ya kushangaza ya waliamua kutopiga kura (zaidi ya 55%) […].

Katika makala hiyo hiyo, mwanablogu huyo pia anatoa sababu zinazowezekana ili kufafanua kwa nini watu waliamua kutopiga kura:

1. La répétition soutenue des consultations et des scrutins sur une période très dense entre le 10 janvier et le 14 mars.

2. La question du statut institutionnel aura été un enjeu majeur aux yeux des électeurs, reléguant les régionales dans la sphère de la politique politicienne.

3. La qualité bien terne du débat et des propositions politiques de même que le climat délétère dans lequel se déroula cette campagne.

4. Le choix incongru du vote au 2ième tour.

1. Kurudiwa kwa kura katika kipindi kifupi sana tangu Januari 10 mpaka Machi 14.

2. Suala la nafasi au wadhifa wa taasisi kwa vyovyote vile lilikuwa na umuhimu zaidi katika macho ya raia, ambapo uchaguzi wa majimbo uanchukuliwa kama siasa tu.

3. Viwango vya mijadala na programu za siasa pamoja na mazingira yenye sumu ya kampeni.

4. machaguo ya hovyo ya kura katika duru la pili.

Mwanablogu wa ki-Martinique [moi]’s playground anatoa mawazo yake kuhusu duru la kwanza la uchaguzi, katika makala ambayo inabainisha matokeo katika kila orodha, pamoja na maoni yake binafsi. Na hivyo, anatoa muhtasari wa madau katika uchaguzi huu wa Martinique [Fr]:

Trois listes se maintiennent donc pour un second tour ou le duel Marie-Jeanne/Letchimy annoncé va connaître son épilogue.

Orodha tatu bado zipo kwa ajili ya duru la pili, ambamo ushindani mkali kati ya Marie-Jeanne na Letchimy utafikia mwisho wake.

Ushindani huo huo umetajwa na Bondamanjak katika makala yenye kichwa “André Lesueur, sauti ya tatu

Wote [moi] na Bondamanjak wanatoa maoni juu ya kupungua sana kwa wapiga kura wa mrengo wa kulia huko Martinique. Anajiuliza [Fr]:

Depuis combien de temps la droite ne s’était pas retrouvée à un second tour d’élections régionales ?

Tangu lini watu wa mrengo wa kulia walifuzu kwa ajili ya duru la pili la uchaguzi wa majimbo?

Oni katika makala ya Bondamanjak linasema [Fr]:

Juan […] j'ajouterai
pour terminer que la droite pour moi est menacée d'inutilité politique.

Juan […] ili kuhitimisha, ninaweza kusema kwa maoni yangu mrengo wa kulia unatishika kwa kukosa maana kisiasa.

Maoni hayo yaliyotolewa na wanablogu wa ki-Martinique kuhusu viwango duni vya kampeni za uchaguzi, watu kuchoshwa na chaguzi pamoja na nafasi ngumu ya vyama vya mrengo wa kulia si jambo ambalo linazikumba idara za ng’ambo peke yake, kwani uchaguzi katika Ufaransa bara ulifuata mtindo huo huo. Kama vile makala hii iliyoandikwa na mwanablogu wa Kifaransa Ma Liberté, inavyoeleza.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.