Kama uanahabari wa kijamii unabadilisha mtindo ya mawasiliano katika nchi za Magharibi, basi kwa hakika haujapungukiwa katika kufikia sehemu zinazovutia barani Afrika. Wakati wa Uchaguzi wa Rais wa mwaka 2008 nchini Ghana, Wa-Ghana wengi walitumia tovuti za uanahabari wa kijamii kama vile Twita na Facebook ili kushirikiana hofu zao na maoni kuhusu mchakato huo (wa uchaguzi). Mshindi wa mbio hizo alipotangazwa, tovuti hizo hizo ziligeuka kuwa sehemu za chereko chereko – angalau kwa mashabiki wa chama kilichoshinda.
Sherehe za kwenye mtandao wa intaneti zilipangwa, kwa mfano, baada ya uchaguzi wa Rais wa Marekani 2008, na mamia ya watu kutoka sehemu zote duniani walijiandikisha kushiriki, kwenye mtandao. Kwa hiyo haishangazi kwamba watu wa zama hizi hizi za kidijitali wameamua kuutumia mtindo wa maisha wa teknolojia-teknolojia na kurukia tamasha la Accra Twestival huko nchini Ghana. Na wakati huu tamasha hilo litafanyika kwenye wavuti.
MacJordan, wa Global Voices, anashirikiana na Rodney Quarcoo, mpiga picha wa Ghana anayetambulika vizuri ili kulifikisha tukio hili la kuburudisha kwa watu wa Ghana. Lakini hili si jambo la kawaida. Kama vile MacJordan alivyoliweka katika makala kuhusu tukio hilo:
[tukio hilo] lina lengo la kuunga mkono jambo kubwa; nia hilo ni kupata vifaa vya elimu kwa ajili ya watoto walio katika sehemu zenye umasikini nchini Ghana.
Na anafafanua katika makala hiyo:
Alhamisi tarehe 25 Machi 2010, mamia ya watu katika miji mingi duniani pamoja na Accra watakutanika nje ya mtandao na kukusanya nguvu kwa ajili ya jambo muhimu la Elimu kwa kuandaa matukio ya kufurahisha na kuelimisha umma. Twestival™ (au Tamasha la Twita) linatumia uanahabari wa kijamii kwa ajili ya manufaa ya jamii. Matukio yote yanaandaliwa kwa 100% na watu wanaojitolea na 100% ya michango inakwenda moja kwa moja kwenye miradi.
Je fedha zitakwenda wapi? Mlolongo huo huo unatoa taarifa hii:
Kila mji utakaokuwa na Tamasha la Twestival utapewa fursa ya kuchagua sehemu ya elimu ambayo wataiunga mkono. Kitendo hicho kitatambuliwa kwa alama maalum katika tovuti yao wakati watakapo weka lengo lao. Kwa kiasi kido cha fedha kama dola za Kimarekani $28 wataweza kuchangia sare, vitabu, penseli, na makaratasi ambayo motto atahitaji ili aweze kwenda shule kwa kipindi cha mwaka mmoja. Shirika la Concern Worldwide linaweza linaweza kuhakikisha kuwa 100% ya fedha za Twestival zitakwenda moja kwa moja kwenye gharama za mradi. Hii inamaanisha kwamba fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kununulia vifaa (mitaala, madawati, kalamu) pamoja na shughuli nyingine za mradi kama vile ujenzi wa shule; ukarabati wa madarasa; mafunzo ya utawala/waalimu; Vikundi vya Wazazi na Waalimu; vilabu vya VVU/UKIMWI; maji na usafi wa majitaka mashuleni; mafunzo ya afya shuleni; utetezi wa elimu; elimu ya ufundi/ na maisha kwa vijana, wakulima na wanawake; na maendeleo ya mitaala kwa vyuo vikuu na shule za sekondari.
Nembo iliyobuniwa vizuri ya tukio hili, iliyotengenezwa na Quarcoo, inafanya kazi nzuri ya kuamsha hamasa ya tamasha hilo. Ujumbe wa Twita wa februari 9 katika ukurasa wa Twita wa Quarcoo katika kuitikia tangazo la tamasha unasomeka:
Twendeni wana-twita. Tufanikishe.
Ukurasa wa tamasha la Twestival wa Accra umekuwa ukiwahimiza watu wajiandikishe kufanya kazi za kujitolea kwa ajili ya shughuli hiyo. Kwa mujibu wa ukurasa huo, waandalizi wanaonekana kuwa wanawazengea wasanii maarufu wa Ghana ili wajiunge na kufanikisha shughuli hiyo.
Ujumbe wa kuvutia katika ukurasa wa Twestival unasomeka:
Elimu inawapa watu sauti katika jamii. Pia inawafanya watu wafahamu haki zao na fursa zilizopo.
Hakika. Elimu ni nyanja ambayo inahitaji msaada barani, hasa huko vijijini. Itavutia kuona kiasi gani cha mahitaji kitakidhiwa na tamasha la twestival huko Accra.