Mali: Vitambaa Vyasuka Nguzo za Uchumi na Utamaduni


Kwa kupitia video, tunaona na kujifunza kuhusu umuhimu wa utamaduni na ongezeko la kiuchumi ambalo utengenezaji vitambaa huwapa baadhi ya watu na mashirika nchini Mali. Kutoka katika kikundi cha wanawake kinachodai kuwa kimeifanya Mali kuwa nguvu katika nyanja ya kutia rangi nguo, mpaka kwa wasanii ambao wameamua kuufanya mtindo wa Bamako au mtindo wa nguo zinazotiwa rangi kwa matope kuwa ni chapa yao, mpaka kwenye nyanja ya utalii ambayo imekua kwa njia ya hii sanaa.

Kwanza, kwa kupitia Ustadi: tumejifunza juu ya shughuli za kuchangisha fedha ambazo Maureen Gosling aliandaa ili kusaidia kuimalizia filamu yake inayohusu wanawake wanaotia rangi vitambaa wa mjini Bamako (Mji Mkuu wa Mali). Katika patigazeti ya video hii, watia rangi nguo wa kike wanaongelea umuhimu wa nguo hizo zinazotiwa rangi nchini Mali na jinsi ambavyo utengenezaji wake umenufaisha maisha yao:

Aina nyingine ya utamaduni wa vitambaa ni ile ya nguo za matope. Video hii inayofuata inatoka kwa TravelWestAfrica na ilipigwa huko Ségou, tunaona jinsi wanavyotengeneza rangi ambazo zinajumuisha matope ambayo yavipa vitambaa hivyo jina lake:

Jina lingine la nguo za matope ni Bogolanfini; katika video hii inayofuata iliyopigwa na hubuf mwaka 2006, mkufunzi anaelielezea kundi la wanafunzi bogolan ni kitu gani, imetengenezwa kwa kutumia nini naina maana gani kwa utamaduni wa Mali:


Katika video hii inayofuata iliyopigwa na claudiodumali
tunaweza kuona kundi la wageni likijifunza kwa vitendo; kwa kutumia vipande vidogo vya vitambaa wanafanya majaribio kwa rangi tofauti na matope ambayo hutumika katika kutengeneza Bogolan huko Ségou:

Kama utapenda kufahamu zaidi kuhusu Bogolan, polbenmali amepakia filamu yenye sehemu mbili (sehemu ya 1, sehemu ya 2 [fr]) inayomuonyesha Issiaka Dembele, msanii aliyeuchukua mtindo wa Bogolan kama zana yake. Katika video hizo, Dembele anaongea kwa Kifaransa kuhusu kazi yake, lakini picha zinaonyesha wazi mchakato mgumu na wenye kuchukua muda mwingi wa kuvitia vitambaa rangi ya njano, na kuvisiliba kwa matope ya kwenye mabwawa ambayo yaliachwa yaoze kwa miezi kadhaa ambayo yatavibadilisha vitambaa kuwa vyeusi, kasha kupitia juu ya maeneo ya njano ili kuondoa rangi katika maeneo fulani, na kupaka rangi juu ya rangi nyingine katika vitambaa vingine:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.