Wasiwasi wa Usalama wa Mfungwa wa Syria, Aliyehamishwa Kwenda Kusikojulikana

The FreeBassel poster from @freebassel on Twitter. Bassel Safadi has been imprisoned in Syria for almost four years and friends and activists fear for his life after he was transferred from his prison today to an unknown location

Bango la FreeBassel kutoka kwenye anuani ya mtandao wa Twita @freebassel. Mfungwa huyo amewekwa ndani nchini Syria kwa miaka minne na marafiki na wanaharakati wana wasiwasi na maisha yake baada ya kuhamishwa leo kutoka kwenye gereza alilokuwemo kwenda mahali kusikojulikana

Wanaharakati wanaitaka serikali ya Syria kumwachilia huru mara moja mfungwa ambaye ni mhandisi wa programu za kompyuta mwenye asili ya Syria na Palestina Bassel Khartabil, anayefahamika pia kama Bassel Safadi, baada ya kuhamishiwa kutoka kwenye gereza lake kwenda mahali pasipojulika mapema leo.

Safadi, ambaye amekuwa gerezani kwa zaidi ya miaka minne, anafahamika sana kama mtengenezaji wa zana huria za mtandaoni. Ni kiongozi wa taasisi ya Creative Commons nchini Syria na anafanya kazi bila kuchoka kwenye miradi kama Mozilla Firefox na Wikipedia, na amejizolea sifa kwa kufungua mtandao wa intaneti nchini Syria na kupanua upatikanaji na uelewa wa mtandao kwa wananchi. Kwa mujibu wa Bunge la Ulaya, kukamatwa kwake ni sehemu ya jitihada za serikali ya Syria kujaribu kuzuia upatikanaji wa mtandao kwa jamii ya mtandaoni na hata kuminya uhuru wa kujieleza nchini humo.

Kwa mujibu wa ukurasa wa Facebook ulioanzishwa na watetezi wake wakidai kuachiliwa kwake:

تم نقل باسل من سجن عدرا الى جهة مجهولة بعد ان اتت دورية لا يعرف بالضبط الى اي جهة تتبع وطلب منه اخذ كل اغراضه
من المتوقع ان يكون نقل الى مقر المحكمة الميدانية في الشرطة العسكرية في منطقة القابون
قلق ومخاوف على مصير باسل بعد ان اصبح وضعه مجهولا من جديد

Bassel alihamishwa kutoka gereza la Adra kwenda kusikojulikana baada ya walinzi wasiojulikana wanahusiana na nani, walipokuja na kumtaka akusanye vitu vyake. Inatarajiwa kwamba atakuwa amehamishiwa kwenye makao makuu ya mahakama ya kiraia kwenye eneo la Jeshi la Polisi huko Al Qaboun. Tuna wasiwasi na maisha yake baada ya kutokujulikana amepelekwa wapi baada ya hapo.

Khartabil alikamatwa mnamo Machi 15, 2012, siku ya kukumbuka mwaka mmoja tangu kuanza kwa mapinduzi ya Syria. Alihojiwa na kuteswa kwa siku tano na kikosi cha usalama cha Military Branch 215. Alihamishwa kwenye kwenye kitengo cha mahojiano namba 248 na hakuruhusiwa kuonana na watu kwa miezi tisa. Mnamo Desemba 9, 2012, Khartabil alipelekwa mbele ya mwendesha mashtaka wa jeshi bila kuwa na mwanasheria, na alishitakiwa kwa “kufanya upelelezi kwa ajili ya nchi adui”. Alipelekwa kwenye gereza la Adra jijini Damascus, ambako amekuwa anashikiliwa, mpaka leo. Taasisi ya Electronic Frontier Foundation (EFF) inasema:

Bassel alijikuta akikamatwa kwa sababu ya kuonekana kwake kama mtaalam wa teknolojia na mwanaharakati.

Tamko la mtandaoni, lililoanzishwa na rafiki yake na mwanaharakati Mohamed Najem, linapatikana kwenye tovuti ya Change.org kudai Khartabil aachiliwe huru. Tafadhali bofya kiungo hiki ili kutia saini.

Rafiki na mwanaharakti wa uhuru wa mtandaoni Jillian C. York, ambye pia ni Mkurugenzi wa EFF kwa ajili ya kutetea uhuru wa kujieleza kimataifa, anamwunga mkono. Alitwiti:

Rafiki yangu Bassel Safadi amehamishwa kutoka gereza la Adra nchini Syria, na hatujui aliko. Tafadhali tia saini tamko hili

Tunajua matamko hayataishawishi serikali ya Syria (au yeyote) lakini ndicho tunachoweza kukifanya. Tafadhali tusaidie kueneza ujumbe huu ili Bassel awe salama.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.