Raia wa Ufaransa Wastukia Hatari ya Muswada wa Udukuzi

Anti-surveillance demonstration in France. Photo via Amnesty International.

Maandamano ya kupinga udukuzi wa mawasiliano nchini Ufaransa. Picha kwa hisani ya shirika la Amnesty International.

Baada ya kushambuliwa kwa Charlie Hebdo, pamoja na serikali kukabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa makundi ya kiraia, mwezi Mei 2015 Bunge la Ufaransa lilipitisha muswada unaoiruhusu serikali kusikiliza simu na kusoma barua pepe za watu wanaohisiwa kuwa magaidi bila kulazimika kupata ruhusa kutoka kwa jaji wa mahakama ya sheria. Muswada huo unayalazimisha makampuni yanayotoa huduma za intaneti kuweka vifaa vinavyoitwa ‘boksi jeusi’ vyenye uwezo wa kuhifadhi na kuchambua taarifa za watumiaji wapatao milioni moja wa inteneti na unayalazimisha makampuni hayo kutoa taarifa hizo kwa mashirika ya kijajusi. Muswada huo unawaruhusu maafisa wa usalama kuweka kwa siri vinasa sauti, kamera na vifuatiliaji vinginevyo kwenye nyumba za washukiwa wa ugaidi. Chini ya sheria hiyo, serikali inaweza kuruhusu udukuzi kwa sababu zisizoelezwa vyema kama vile ‘maslahi makuu ya sera ya mambo ya nje’ na kuzuia ‘utukutu unaoratibiwa na vikundi.”

Makundi yanayotetea uhuru wa kiraia ikiwa ni pamoja na Amnesty International, ibara ya 19, Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari na Kitengo cha Utetezi cha Global Voices (Advox) vimeandika barua ya pamoja iliyoandikwa na kundi linaloongoza kwa kutetea haki za mtandaoni nchini Ufaransa La Quadrature du Net, iliyochapishwa mnamo Septemba 30 ikiwandikwa kwa wabunge wa Ufaransa na kutoa mapendekezo kadhaa ya mabadiliko ya vifungu vya muswada huo. Wameandika:

Kwa muswada huu, bunge linakaribia kuruhusu hatua za udukuzi wa mawasiliano zisizokubalika kwa lengo la kufuatilia mawasiliano ya kimataifa. Kwa kutumia kanuni ya ukusanyaji mkubwa wa taarifa, muswada huu unatafuta kuhalalisha ukiukwaji wa haki za kiraia na za binadamu kama alivyoonesha Edward Snowden kuhusu shughuli za mashirika ya kijasusi kama yale ya Marekani na Uingereza. Kwa sababu mawasiliano ya dunia kwa njia ya intaneti yanapitia kwenye mkongo wa mawasiliano ulioko chini ya bahari nchini Ufaransa, hseria hii inaweza kuiingiza Ufaransa kwenye orodha ya nchi zenye zenye uwezo mkubwa wa kudukua mawasiliano ya watu.

Pamoja na ukosoaji mkubwa kwenye makundi ya kutetea haki za kiraia, muswada huo ulipata upinzani mdogo sana kutoka kwa wananchi na vyama vya siasa. Rais wa Ufaransa François Hollande aliliomba Baraza la Katiba kuupitia muswada huo baada ya kuwa umeshapitishwa mwezi Juni, na kufanya hiyo iwe mara ya kwanza kwa rais kuupeleka muswada mahakamani kabla hajaruhusu utekelezaji wake. Tovuti ya ki-Faransa Les Moutons enragés ilieleza mchakato ulivyokuwa, na kuhitimisha kwa taarifa ya kina iliyoandaliwa na Nextimpact :

…le Conseil constitutionnel avait censuré un des articles du projet de loi gouvernemental, celui encadrant la surveillance internationale. Pourquoi cette censure ? Principalement, parce que la disposition législative renvoyait à décret en Conseil d’État le soin de définir les modalités d’exploitation, de conservation et de destruction des renseignements collectés. Un joli cas d’incompétence négative [puisque cette matière est réservée par la constitution au législateur]

[…] Après une longue période d’incertitude, le gouvernement a annoncé la semaine dernière le dépôt surprise d’une proposition de loi pour combler cette lacune. […] par ce biais, il évite le passage par un projet de loi, qui l’aurait obligé à publier une étude d’impact. Une étape potentiellement douloureuse où il aurait dû détailler le coût de ces mesures notamment.

Déjà, les articles sont beaucoup plus denses que la partie censurée par le Conseil constitutionnel. C’était prévisible puisque le gouvernement a dû (faire) replacer dans la future loi des dispositions qu’il tentait de publier dans un décret secret.

…Baraza la Katiba liliondoa moja wapo ya ibara ya muswada wa serikali iliyokuwa ikifafanua maana ya udukuzi wa kimataifa.

Kwa nini? Kwa hakika ni kwa sababu muswada huu ulikuwa na takwa la vigezo na masharti ya kuchukua, kuhifadhi na kufuta taarifa zinazokusanywa kwa njia ya agiza. Huu ni mfano mzuri wa kukosekana weledi [kwa mujibu wa katiba ya Ufaransa, hilo linategemea Bunge pekee].
[…]

Baada ya kipindi kirefu cha kusita sita kufanya maamuzi, juma lililopita serikali ilitangaza kuuondoa ghafla muswada mwingine uliokuwa umetengenezwa kwa lengo la kuziba pengo hilo […] na hivyo kukwepa kupitisha muswada ambao ungefanya iwe lazima kwanza kufanya tathmini ya madhara. Hatua hiyo ina hatari inayoweza kujumuisha kubainisha, hususani, undani wa gharama za hatua hizo.

Ibara hizo kwa hakika hazina matatizo kwa kulinganisha na sehemu nyingine zilizoondolewa na Baraza la Katiba. Hii haishangazi sana, kwa sababu serikali ililazimika iweke matakwa mengine badala ya vipengele vilivyokuwepo ambavyo ilijaribu kuvichomeka kwa amri ya siri.

For a detailed review of the provisions of this additional bill on international surveillance, read the comprehensive report published by French magazine l'Obs on September 9.

Makundi ya kutetea haki za kiraia yalijitokeza mbele baada ya kukubaliwa kwa sheria hiyo. Shirika la Amnesty International Ufaransa limelaani muswada huo kwa ksuema kwamba “ni janga kuu kwa haki za binadamu.”

Mtandao wa La Quadrature du Net ulieleza kwenye tovuti yake mnamo Septemba 15:

Mfumo huu mkubwa wa udukuzi una sura ya upepelezi wa dunia yote, na unaifanya Ufaransa kuwa adui wa haki za msingi. Kwa sababu muswada huu ni kuhalalishwa kwa vitendo vya siri vilivyoanza kutekelezwa tangu mwaka 2008, wakati umefika kwa wananchi na wawakilishi wao kutoa maoni yao kuhusiana na vita hivi katika karne ya 21.

Kisheria, hatua hii inapelekwa kwenye mahakama za Ufaransa, chini ya jitihada zilizoratibiwa na Haki za Kidijitali Ulaya (EDRI, kundi linalofanya kazi zake jijini Brussels.

Mnamo septemba 3, 2015, kampuni isiyo ya kibiashara ya kutoa huduma za intaneti (ISPs) French Data Network (FDN) na Shirikisho la FDN (FFDN) pamoja na makundi ya utetezi wa haki za kidijitali La Quadrature du Net walitangaza kuwasilishwa kwa mapingamizi mawili ya kisheria kwenye Baraza la Ufaransa linaloshughulikia masuala ya Nchi kupinga vitendo vya udukuzi wa mawasiliano ya intaneti vinavyofanywa na mashirika ya ujasusi wa kimataifa ya Ufaransa, kama vile Kurugenzi Kuu ya Usalama wa Nje (DGSE).

Uhamasishaji na uelimishaji kuhusu muswada huu unashika kasi, ingawa ni kwa kuchelewa.

Tutarajie kwa sababu ya demokrasia tutampata ‘Snowden’ wa ki-Faransa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.