
Mwalimu Nyerere akiwa na Rais wa zamani wa Ujerumani Magharibi Richard von Weizsäcker mwaka 1985. Picha imetolewa kwa matumizi chini ya leseni ya Creative Commons na German Federal Archive.
Tanzania imekuwa marais watano tangu ijitwalie uhuru wake kutoka ukoloni wa Mwingereza mwaka 1961. Rais wa kwanza, Julius Kambarage Nyerere, anayefahamika zaidi kwa jina la heshima Mwalimu Nyerere, amekuwa mzalendo anayeheshimika na kupendwa zaidi katika historia ya Tanzania.
Nyerere, anayefahamika kwa jina la Baba wa Taifa, anakumbukwa kwa, pamoja na mambo mengine, kujenga umoja na utambulisho wa taifa katika nchi hiyo yenye makabila zaidi ya 120 — mafanikio nadra kupatikana katika siasa za Afrika — na alikuza Kiswahili, lugha isiyo ya kikabila inayozungumzwa zaidi barani Afrika.
Nyerere alikuwa mstari wa mbele katika harakati za ukombozi barani humo na aliunga mkono harakati za kupambana na ubeberu duniani kote. Haishangazi kwamba taasisi za kisiasa kama FRELIMO ya Msumbiji, ANC na PAC za Afrika Kusini, ZANU na ZAPU za Zimbabwe, MPLA ya Angola na SWAPO ya Namibia zote zilikuwa na ofisi na makambi ya mafunzo nchini Tanzania. Kwa nyongeza, nchi hiyo ilikuwa kimbilio la wanaharakati wa kimarekani wa haki za kiraia, wanachama wa chama cha Black Panther kama vile Pete O'Neal na Geronimo, pamoja na wapinzani wa vita vya Vietnam.
Miaka kumi na sita baada yakifo chake kilichotokea Oktoba 14, 1999, wa-Tanzania wanatumia alama habari ya #DearNyerere kumkumbuka, hasa katika mukhtadha wa uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika Oktoba 25, 2015.
‘Hutaamini kwamba nchi yako ni ombaomba’
twiti nyingi zimejaa mchanganyiko wa hisia, kukata tamaa na kutokuridhishwa na namna nchi inavyoendeshwa tangu afariki dunia.
Glady Shao alionesha kutokuridhika kwake na uongozi wa kisiasa uliopo nchini humo:
#DearNyerere if you came back today, you would definitely get a heart attack and die once again if u saw what some leaders hv been doing
— GLADYS SHAO (@GladyzShao) October 14, 2015
Kama ungerudi leo lazima ungepata shinikizo la moyo na kufa kwa mara nyingine kama ungeona kile kinachofanywa na baadhi ya viongozi
Nabil Omar alilalamikia usimamizi mbovu wa mali asili kama Tanzanite:
#DearNyerere Tanzanite is no longer Tanzanian, you preserved it for us but the people are gaining very little from it. Thievery everywhere.
— Nabil Omar (@NabilTanzania1) October 14, 2015
Tanzanite si mali ya wa-Tanzania tena, uliyahifadhi kwa ajili yetu lakini wananchi wananufaika nayo kidogo sana. Wizi kila mahali
Tanzanite ni madini adimu yanayopatikana Tanzania pekee. Hata hivyo, India inafahamika kama mwuuzaji mkuu wa madini hayo pamoja na zuio la serikali ya Tanzania dhidi ya uuzaji wa madini hayo nje.
James Ngonyani alitwiti kwa ki-Swahili:
#DearNyerere huwez amini nchi yako leo inajivunia kua ombaomba wakat ni ya tatu kwa uzalishaji wa dhahabu duniani.
— James ngonyani (@JamesXelebrity) October 14, 2015
W. Quiyenga alindika kuhusiana na mtazamo maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho Nyerere alisaidia kukiunda:
#DearNyerere watz wanasema bora wapigie kura jiwe kuliko ccm
— W.quiyenga (@qwille) October 14, 2015
‘Enzi zako, umaarufu ulitokana na matendo mema’
Steve Ole Moruo alilalamika:
#DearNyerere Zama zako umashuhuri ulikuwa kutenda mema ya kujenga nchi ila sasa hivi ni Followers wa Instagram Na Twitter 😂😂
— Steven Ole Moruo (@MoruoKing) October 14, 2015
David Nguma alibainisha:
#DearNyerere kauli zako zinatumiwa zaidi na upinzani. Cccm wanaona aibu kukunukuu kwenye mikutano yao maana wamekusaliti.
— David Nguma (@DavyNguma) October 14, 2015
Albert Secha alikuwa na matamanio yake:
#DearNyerere ungerudi uiongoze Tz hata for a year! just one year! .. We miss your integrity!
— Albert Secha (@SechaAlbert) October 14, 2015
#DearNyerere, ungerudi uiongoze Tz hata kwa mwaka mmoja! mwaka mmoja tu! …Tunakosa uadilifu wako
The Van Official alitwiti kuhusu kusafirishwa kwa wanyama hai nchini humo:
@SweetAnimal_ @franklin_tissa #DearNyerere ulituachia tembo siku hizi hakuna tena twiga wanapanda ndege
— the van official (@thevanofficial3) October 14, 2015
Tanzania imepiga marufuku kusafirishwa nje kwa wanyama pori baada ya takribani wanyama na ndege 130, ikiwa ni pamoja na twiga kusafirishwa nje ya nchi wakiwa hai. Wanyama hao walisafirishwa kwa ndege ya mizigo kutoka Tanzania kwenda Qatar.
Kuhusu uchaguzi mkuu, Othman alifikiri:
#DearNyerere Hata Wewe Ungekuwepo CCM Isingekuwa Sababu Ya Kuwafanya Watanzania WAKIPENDE CCM
— Othman CR Sixteen (@OthmanCRsixteen) October 14, 2015
‘Tanzania itapata nafuu’
si watumiaji wote wa twita walitumia alama habari hiyo kulalamika kuhusu mwenendo wa mambo nchini humo. Michael Paul Baruti, kwa mfano, alitwiti:
We still here, stronger than ever.. Transparency and accountability are starting to prevail… Tanzania will only get better… #DearNyerere
— Michael Paul Baruti (@michaelbaruti) October 14, 2015
Bado tupo, imara kuliko wakati mwingine wowote…uwazi na uwajibikaji vinaanza kuimarika…Tanzania inaanza kupata nafuu
Kibibi aliandika:
#DearNyerere nchi yetu inazidi kusonga mbele kwa maendeleo #HapaKaziTu pic.twitter.com/L7eX9spEud
— kibibi003 (@kibibi003) October 14, 2015
Unaweza kusoma mahojiano ya Nyerere, aliyoyafanya na Ikaweba Bunting wakati akiwa hai, kujifunza zaidi kuhusu maono aliyokuwanayo Nyerere kwa ajili ya Tanzania.