Makala hii ni miongoni mwa makala zetu maalumu kuhusu Vurugu za mwaka 2011 nchini Ivory Coast..
Habari mpya ziliingia saa 7 GMT siku ya Aprili 11, 2011: Laurent Gbagbo alikamatwa katika makazi yake ya Cocody, pamoja na mkewe, Simone, na msafara wa watu wa karibu. Miezi mitano baada ya kukataa kukabidhi madaraka kwa rais anayetambuliwa kimataifa kama rais mpya wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara, mgogoro nchini humo hivi sasa unaelekea kufikia tamati.
Mtiririko wa matukio kuanzia Aprili 10 mpaka 11, 2011
Ofisi ya rais wa Ufaransa (@Elysée) [fr] ilitangaza kwa njia ya Twita kwamba Ufaransa imekubali kushiriki katika shambulio la kijeshi nchini Côte d'Ivoire siku ya tarehe 10 Aprili, 2011:
@Elysée: En accord avec le Président #Ouattara, le SG #ONU a demandé à N #Sarkozy la poursuite de la participation française aux opérations ONUCI
Kwa kutoa tamko hilo, ofisi ya rais wa ufaransa Elysée ilijithibitishia uhalali wa kuanza tena [fr] mashambulizi ya mabomu yanayolenga Makazi ya rais eneo la Cocody, Abidjan, ambako Laurent Gbagbo alikuwa amejificha.Uamuzi huu ulifanywa kama jibu la shambulio [fr] lililoelekezwa na vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Gbagbo (FDS) kwenye Hoteli ya Golf, makao ya zamani ya kambi ya Ouattara. Mashambuli ya mabomu yalianza saa 11 GMT (kwa saa za Abidjan).
video hii ilitumwa na mtumiaji wa YouTube terryko0 siku ya tarehe 11, Aprili. Kichwa chake: “Abidjan 10-04-2001. Tirs de missiles contre la résidence de Laurent Gbagbo” (Makombora yapigwa kwenye makazi ya Gbagbo):
Shambulio hilo liliidhoofisha sana kambi ya Gbagbo, kama vile filamu hii iliyopigwa saa chache baada ya shambulio, iliyowekwa kwenye YouTube mnamo Aprili 10, 2011 na mtumiaji Atteby. inavyothibitisha. Katika Video hiyo unaweza kumuona Sidiki Bakaba, muigizaji wa Ki-Ivory ambaye hivi karibuni alifanya mahojiano kwenye tovuti ya Slate Afrique [fr]akiwa amejeruhiwa:
Katika video, hii iliyopakiwa kwenye YouTube na mtumiaji atteby, wafanyakazi wa utibabu wanaonekana wakiwa kazini, wakiwahudumia wanajeshi kwenye makazi ya rais:
Asubuhi ya Aprili 11, 2011, video ifuatayo iliyopigwa kutoka kitongoji cha Ebrie katika eneo la Cocody, Abidjan, inaonesha vifaru vinavyomilikiwa na UNICORN, jeshi la Ufaransa nchini Côte d'Ivoire vikiwa vinasonga. Kwa mujibu wa lgconnectTV, mtumiaji ambaye alituma habari kwenye YouTube mnamo Aprili 11, vifaru hivyo vilikuwa vinaelekea kwenye makazi ya Laurent Gbagbo:
Mnamo majira ya saa 5 Asubuhi GMT, idhaa ya kimataifa ya televisheni ya Ufaransa, France24 ilithibitisha taarifa hiyo kwenye ukurasa wake unaotoa habari moja kwa moja kama zinavyotukia [fr]:
Kwa mujibu wa taarifa ya habari iliyotolewa na Reuters [fr] na kuchapishwa saa mbili baadaye, Laurent Gbagbo alikamatwa na Jeshi Maalum la Ufaransa, na kukabidhiwa kwa majeshi ya Jamhuri ya Ouattara. France24, ilipozungumzia jeshi la Ouattra iliandika:
Amani Katikati ya kila Pingamizi
Baada ya kukamatwa, Gbagbo na Mkewe walipelekwa kwenye hoteli ya Golf, chini ya ulinzi wa karibu wa majeshi ya kimataifa. Videohii inayofuata iliyorushwa na TCI, idhaa ya televisheni inayojulikana kwamba ipo karibu na Alassane Ouattara, Laurent Gbagbo anapewa gwanda la kuzuia risasi ili kuyakinga maisha yake wakati anapokamatwa:
Alassane Ouattara, rais wa Côte d'Ivoire anayetambuliwa kimataifa aliamuru wanajeshi wake wasikiuke haki za binadamu za Laurent Gbagbo na mkewe Simone.
TCI pia ilituma video nyingine ambayo rais wa zamani Gbagbo anatoa wito wa kusitisha mapambano, na kurejesha amani:
http://www.youtube.com/watch?v=Qca5nDIw4yc
Je souhaite qu'on arrête les armes, qu'on rentre dans la partie civile de la crise, et qu'on la conclue rapidement pour que le pays reprenne.
Katikahotuba kwa watu wa Côte d'Ivoire na kwa jumuiya ya kimataifa mnamo Aprili 11, 2011, Alassane Ouattara alisisitiza tena nia yake ya kusimika utawala wa sheria, kuhakikisha ‘uzima na heshima’ kwa Gbagbo na mke wake, na kuchukua hatua za kwanza kuelekea kwenye kurudisha haki.
Msukumo huu wa amani unaungwa mkono na wa-Ivory wengi, kama vile Diouf Mamy (@mymaluydealbi) ambaye aliandika kwenye Twita:
@mymaluydealbi: Après ce qui s'est passé, j'espère que Ouattara sera le président de tous les Ivoiriens sans exception. Que la paix revienne en #civ2010
Makala hii ni miongoni mwa makala zetu maalumu kuhusu Vurugu za mwaka 2011 nchini Ivory Coast.