Makala hii ni sehemu ya habari maalumu tunazowaletea kuhusu Mapinduzi ya Misri ya Mwaka 2011.
Miezi michache tu iliyopita, raia wengi wa Misri walitamani sana kumwona aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Rais Mubarak, akitupwa jela, hata hivyo, pengine ni wachache miongoni mwao waliofikiri kwa uhakika kabisa kwamba siku moja jambo hili lingetimia.
Hata hivyo, mnamo Jumatano ya tarehe 13 Aprili, 2011, raia wa Misri waliamka na mapema asubuhi ya siku hiyohiyo kukutana na habari zinazohusu Mubaraka kutupwa kizuizini. Hapa chini tunawaletea jinsi habari hizi zilivyopokelewa katika ulimwengu wa uandishi wa habari wa Kijmii miongoni mwa Wamisri.
Kusherehekea kutiwa nguvuni kwa dikteta
Mwandishi wa Misri, Ibrahim Farghali, alilinganisha wakati huo [ar] na wakati ule kulipokuwa na habari za mtu wa kwanza kufika katika anga za juu:
…
نتمنى أن نرى مصر قريبا تحتفل بإنجازات شبيهة بمنجزات دول العالم المتقدم
والثورة لا تزال في الشارع
Tuna matumaini kwamba siku moja Misri isherehekee mafanikio kama hayo ya ulimwengu uliondelea, na tunatumaini kwamba hata wakati huo ule moyo wa mapinduzi utaendelea kuwepo mitaani.
Zeinobia naye aliandika makala mpya ya blogu kuhusiana na wasaa huo, aliupa jina rahisi tu, “A Historical Moment” yaani “Wakati wa Kihistoria”. Kisha alieleza jinsi watoto wa rais huyo wa zamani nao walivyokamatwa na kutiwa kizuizini:
Kisha Zeinobia aliendelea kueleza kwamba Mubarak anakabiliwa na mashtaka ya kuua waandamanaji na kuiba fedha za umma; hata hivyo, hadi wakati huu Mubarak bado yupo hospitalini kwa sababu ya matatizo ya kiafya. Alaa na Gamal Mubarak wanakabiliwa na mashtaka kama hayo ya baba yao.
Jinsi watu waliyopokea
Mchora katuni wa Brazil Carlos Latuff aliweka kumbukumbu ya wasaa huo kwa namna yake,alichora mifululizo ya series katuni .
Nyingi ya Twita za hivi punde zilizotumwa katika siku mbili zilizopita nazo zilihusu kukamatwa kwa Mubarak na kutiwa kizuizini.
Ujumbe wa sauti iliyorekodiwa wa Mubarak[ar], ambao aliutuma Al-Arabiya (Kituo cha Habari za Televisheni) ambaoulitokea kuwa kumbe uliandikwa na mwanasheria maarufu wa Misri, Fareed El-Deeb, unasemekana kuwa ni msumari wa mwisho kwenye jeneza la Mubarak:
Katika majuma machache yaliyopita, Gereza la Torah liligeuka siyo tu kuwa makazi ya watoto wa Mubarak, lakini pia limekuwa makazi ya nguzo (watu) wengi tu waliokuwa katika utawala wa Mubarak. Kupitia Twita, watu hawakuiachia fursa ya kufanyia mzaha jambo hili:
Akaunti za uongo kadhaa za Twita za Mubarak, familia yake (Suzanne Mubarak, Alaa Mubarak, Gamal Mubarak na mkewe Khadija), na za watu katika utawala wake (Fathi Sorour, Safwat El-Sharif na Ahmed Nazif) zimetengenezwa ili kuwakebehi.
Hatimaye, pamoja na yote haya, na licha ya orodha ya upingaji wa mafanikio ya Mubarak kama ilivyoandikwa na Ahmed Hayman, bado kuna wanaomwonea huruma rais huyo wa zamani:
Makala hii ni sehemu ya habari maalumu tunazowaletea kuhusu Mapinduzi ya Misri ya Mwaka 2011.