Iangazeni Naijeria: Imetosha Sasa Basi


Pamoja na kuwa nchi yenye utajiri wa mafuta, hali ya ugavi wa umeme nchini Naijeria hairidhishi. “Katika sehemu nyingi za nchi, giza linatawala na majenereta yamechukua nafasi kama vyanzo vya nishati ya umeme” Inasema blogu ya Adebayo. “Umeme unapokatika – jambo ambalo hufanyika wakati wote – watu hukaa gizani au, kama wana bahati, huwasha majenereta ambayo yanaigharimu nchi Dola za Kimarekani bilioni 140 kuyatia mafuta (ongeza na gharama nyingine kwa ajili ya mtaji na matengenezo)”, anasema David Steven kwenye blogu ya Global Dashboard. Adebayo anaongeza:

Lakini kueleza au kufikia kiini cha sababu za hali kuwa hivi ni jambo lenye gumu. Kuanzia kwa makundi ya waagizaji wanaoingiza majenereta, wahandisi wanaoshindwa kumaliza miradi ya umeme, wananchi wanaohujumu misongo ya umeme na mitambo, tabia ya serikali mpaka watengenezaji wa majenereta (katika nchi zilizoendelea) ya kufanya mambo bila haraka; wote hawa wana maslahi fulani katika kukwama huku kwa upatikanaji wa nishati ya umeme nchini Naijeria.

Sasa Wanaijeria wameanza harakati kubwa za mtandaoni zinazoipinga hali hii inayokeheresha katika watuvi za habari za kijamii, hasa kwenye Twita yenye anuani #lightupnigeria (#iangazenaijeria). Lipo pia kundi la Facebook, lenye maelezo yafuatayo:

Je umechoshwa na visingizio visivyoisha vinavyotolewa juu ya uzembe wa PHCN (Mradi wa Umeme wa Naijeria), tunaunda kikundi hiki kama sauti kwa ajili ya kizazi chetu. Ni wakati jambo lifanyike, nchi ya 7 kwa uzalishaji wa mafuta ni kati ya nchi zilizo nyuma zaidi katika ugavi wa umeme. Wakati umefika, Naijeria ni yetu sote na kama hatutasema sasa hivi, ni mzigo huo huo tutakaolazimika kuubeba sote. Kwa hiyo jiunge, waambie rafiki zako, familia na yeyote uwezaye, imetosha. Sauti yetu inaweza kuwa ni ndogo sasa lakini kadiri kundi linavyokua na neno likisambaa, serikali itasikia maneno yetu na jambo lanaweza kufanyika. IANGAZENI NAIJERIA ili maendeleo katika sekta nyinginezo yakue pia.

Nishati ni injini inayoendesha maendeleo ya viwanda, inayoboresha mawasiliano, inasaidia maendeleo katika sayansi na teknolojia, inasaidia mfumo wa utoaji wa huduma za afya na kuboresha kiwango cha maisha ya wananchi. Kwa kuwa nishati ni injini inayoendesha maendeleo ya viwanda, sera bora ya nishati ingeweza kwa namna moja ma nyingine kutengeneza nafasi za kazi hata katika sekta zisizotarajiwa.

Archiwiz kwenye tovuti ya To fit or not to fit? Alitoa maoni kuhusu kampeni yenyewe:

Anuani ya twita peke yake haitaweza kufanya mengi ikiwa wale wanaowajibika hawataziona na kufanya jambo sahihi, lakini ni hatua nzuri ya kwanza. Kuelewa au utambuzi mara zote ni muhimu linapokuja suala la harakati za mabadiliko […]

Na mnauliza, #lightupnigeria ni nini? Maneno yanayoitengeneza alama yanajieleza yenyewe kwa Mnaijeria yeyote, au kwa yeyote aliyewahi kukukaa kwa majuma mawili nchini Naijeria na ameshuhudia mwenyewe madhara ya kukosekana kwa umeme nchini Naijeria. Ninaweza kuwapa orodha ndefu ya kile tunachopoteza kutokana na kukosekana kwa umeme, lakini vitu kadhaa vinajitokeza: fedha, muda & uzalishaji.

[…] Harakati hizi zinahitaji kuvifikia vyombo vya habari na masikio ya viongozi wa Naijeria. Hatuwezi kuendelea kubania jicho kutopatikana kwa umeme.


Haya ni baadhi ya mambo yaliyochaguliwa kati ya yale ambayo watu wamekuwa wakiyasema kwenye Twita kama sehemu ya kampeni ya #lightupnigeria:

Olufunmike

Uchumi wa Naijeria hauwezi kubadilika hadi tutakapo #iangazanigeria


imab

#iangazenigeria ili wanaijeria wake milioni 140 waweze kusema usiku mwema na kweli wautegemee usiku mwema

Naijanews

Jambo pekee lililowahi kufahamika na likawa imara nchini naijeria ni giza #iangazenigeria

Edeanijames

fedha tunazozitumia kununua dizeli kwa mwaka zinaweza kulipia bili ya mwanga kwa miaka 10, kwa hiyo tafadhali #iangazenigeria

aliceronke

#iangazenigeria ili watu wasiende kufanya kazi ya udobi mwisho wa juma!

drdammie

#iangazenigeria Viongozi wa Naijeria wanapenda giza, kwa sababu kazi za mikono yao zina giza, na haziwezi kuhimili mwanga wowote

ricdizzle

#iangazenaijeria kwa sababu pasipokuwepo mwanga usiku & ninapohitaji kufanya haja ndogo…kulenga shimo la choo huwa ni kwa kuhisi!! Wacha!

pheonixforever

hatuna umeme kwa siku nne sasa …#iangazienigeria tafadhali


Naijanews

Ninapanga kuhamia naijeria hivi karibuni lakini ninapanga kutembelea London kila juma kwa ajili tu ya kuchaji simu yangu #iangazienigeria

Ebukalashnikov

Ni saa 5 usiku, hii ina maana ni usiku mwingine bila ya umeme. Kwa matumaini tunaweza #iangazienigeria ili kwamba “Usiku mwema” uwe kweli mwema

ohdichi

#iangazenigeria kwa sababu ni nchi yangu na nchi yangu inastahili mwanga

lowla360
Tunapopigania ili hili liweze kufanya kazi, najua wote mmechoka, lakini fikirini juu watoto wenu, kwa kaisi gani mngependa wakue katika mazingira/taifa zuri #iangazenigeria

abiolaalabi

Ningeaibika sana kama mbeleni wanangu wangeniita kizazi cha jenereta na sikufanya chochote #iangazenigeria

edeanijames

si sahihi kwamba katika wakati na zama hii hatuna ugavi unaoaminika wa umeme #iangazenigeria

damilola

#iangazenigeria kwa sababu umeme wa kuaminika haupaswi kuwa jambo la anasa katika mwaka 2009

archiwiz

Uchafuzi wa mazingira kutoka kwenye majenereta unadumaza ubongo wa vijana wa Kinaijeria. Hivi sasa wengi wetu si wabunifu tena. Tafadhali #iangazenigeria!

Olufunmike

Kampeni ya Obama haikusita hadi siku moja kabla ya uchaguzi. Kampeni yetu ya #iangazenigeria haitakoma mpaka tupate umeme masaa ishirini na nne siku saba za wiki. Waambieni

Ezeani

#iangazenigeria kwa sababu tuna vyanzo –vya asili na vya kutengeneza…tunasubiri nini?

zpixel

Hakuna atakayesikiliza #iangazenigeria kwa ku-twita tu, unatakiwa kuua mtu na kumwambia polisi kuwa hakumtambua mtuhumiwa kwa kuwa ilikuwa giza…

bubusn

Changamoto yetu kubwa haipo Abuja. Ipo kwetu sisi wenyewe. Ni ile sauti isemayo: “Hii itakuwa bure” #iangazenigeria


eldeethedon

Wazo ni kutengenezea video gizani kuonyesha serikali “tumetosheka”!! http://bit.ly/XEDX9 #iangazenigeria

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.