Pakistani: Tatizo La Sukari Limeifanya Ramadhani Kuwa Chungu

Kila mwaka wakati wa mwezi wa Ramadhani huwa kuna upungufu kwenye masoko ya bidhaa za chakula nchini Pakistani kutokana na kuongezeka kwa mahitaji. Mwaka huu upungufu umetokea hasa kwenye soko la sukari. Ili kudhibiti serikali inapanga kuongeza ukubwa wa mauzo ya sukari kwa kupitia maduka ya vifaa (yaliyopewa ruzuku na serikali) kutoka tani 40,000 mpaka tani 100,000. hata hivyo, unapoendesha nje ya maduka hayo kuna ushahidi mkubwa kuweza kushawishi mtu yeyote kuwa hakuna mgawo wa kutosha wa sukari.

Kwa mujibu wa ripoti katika gazeti la The Dawn, ambalo linaelezea hali ya ugavi mjini Karachi, maduka yanapata mgawo mdogo zaidi ya kawaida na hayana uwezo wa kuhudumia mahitaji ya walaji. Bei ya sukari katika soko la wazi ilipanda kufikia Rupia 55-58 kwa kilo (kama ikipatikana) ambapo bei rasmi ya mauzo kwa sukari ni Rupia 38 kwa kilo.

Hassan Khan anaelezea upande wa kisiasa wa tatizo hili katika blogu yake:

Pakistani ina viwanda vya sukari vipatavyo 80. Vingi ya viwanda hivyo vinamilikiwa na wawekezaji pamoja na wanasiasa. Upeo wa unafiki ni kwamba kabla ya ramadhani, walianza kuhodhi sukari na bei yake ikaruka kutoka Rupia 38 mapaka Rupia 54. Kila unapowasha idhaa ya habari ya televisheni ya Pakistani mambo huonekana kuwa mabaya na yanaonekana mabaya zaidi wakati mgogoro umefikia upeo na waziri akivipasha habari vyombo vya habari kwamba kutokana na ongezeko la bei katika soko la kimataifa la sukari, bei ya sukari inaongezeka nchini Pakistani.

Uzalishaji wa miwa nchini Pakistani. Picha na mtumiaji wa Flickr Omer Wazir

Uzalishaji wa miwa nchini Pakistani. Picha na mtumiaji wa Flickr Omer Wazir

http://www.flickr.com/photos/thewazir/ / CC BY-SA 2.0

Sana Saleem anasema kuwa upungufu wa sukari umetokana na uzalishaji mdogo wa mazao mwaka huu:

Imedaiwa kwamba wakulima wanawalaumu wamiliki wa viwanda vya sukari kwa kutolipa vizuri. Takwimu zinaonyesha kuwa malipo kwa wazalishaji yalicheleweshwa kwa zaidi ya miezi minane mpaka kumi. Hii iliwavunja mioyo wakulima na kuacha kuzalisha miwa na kuchagua kuzalisha ngano badala yake ili kupata vivutio vilivyokuwepo. Na sasa imefika wakati wa visa vya wenye viwanda. Siyo tu kwamba wenye viwanda wanalaumiwa kwa kuchelewesha malipo na kusababisha upungufu wa aslimia 15 mpaka 20 ikilinganishwa na mwaka jana, pia wamehodhi kiwango kikubwa cha mazao. Maza ohayo yamehifadhiwa ili kutengeneza upungufu kidanganyifu kwenye soko.

Bilquis, mtaalamu-mshauri kutoka Lahore, anatoa uchambuzi wa kitaalamu juu ya suala hili katika CHUP:

Mwaka huu ulishuhudia upungufu wa kawaida katika uzalishaji wa sukari. Kwa ujumla, wakulima, sawa na wengine, huzalisha mazao ambayo yatawapatia faida zaidi. Katika mwaka 2008-09, serikali ya sasa iliongeza bei ya (kununua) ngano kufikia Rupia 950 (kwa bei ya chini zaidi) ili kuwahamasisha wakulima wazalishe ngano. Hiki kilikuwa ni kivutio na kilipelekea kuwavutia wakulima wengine kuzalisha ngano (kwa sababu ina faida). Na matokeo yake, wakulima wa miwa walihamia kwenye uzalishaji wa ngano ambko kulisababisha upungufu wa uzalishaji wa miwa.

Zaidi, katika muongo uliopita, uzalishaji wa miwa umepungua kutokana na ugumu ulipo kwenye soko la sukari. Wataalamu mbalimbali wanasema kuwa wakulima wamepunguza maeneo yaliyotengwa kwa uzalishaji kutokana na upungufu wa maji, tabia za utawala za wenye viwanda vya sukari, uchelevu wa malipo, ongezeko la gharama za uzalishaji, magonjwa na mashambulizi ya panya. Na hasa wanawalaumu wamiliki wa viwanda na uchelevu au ukosefu wa malipo kwa wakulima na upungufu wa maji kwa ajili ya kumwagilia, vitu ambavyo vinawafanya wakulima wasite kuzalisha zao hilo. Na hivyo, sababu hizo mbili zimepunguza mgawo wa sukari kwa asilimia 15 mpaka 20 ikilinganishwa na mwaka jana.

Hivi sasa, serikali ya Pakistani inafikiria kuagiza sukari kutoka ng’ambo ili kukabili upungufu. Hata hivyo, wafanyabiashara wan je wa sukari kama vile Brazil na India pia wameongeza bei zao. Kwa hiyo bei haitashuka katika muda wowote hivi karibuni. Kitakachotokea katika siku chache zijazo ni muhimu kwani watu wako tayari kutoka mitaani na kufanya maandamano kupinga tatizo hili la sukari.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.