Uganda: Hatimaye Magazeti Yaliyofungiwa na Polisi Yafunguliwa

Uganda imeruhusu magazeti mawili kufunguliwa tena baada ya msuguano uliodumu kwa siku 11 kati ya serikali na vyombo vya habari juu ya barua yenye waliyoipata ambayo iliyoonyesha njama ya kumtayarisha mtoto wa kwanza wa Rais Yoweri Museveni kumrithi kiongozi huyo aliyedumu kwa miaka 27.

Polisi walifunga  ofisi za zageti la Red Pepper na Daily Monitor mnamo Mei 20, 2013 baada ya magazeti hayo kuripoti habari za barua iliyoandikwa na Mratibu mkuu wa Usalama wa nchi kwenda kwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa akiomba kufanyika kwa uchunguzi kuhusu mpango wa kurithishana madaraka, unaojulikana kama Mradi wa Kumwandaa Muhoozi, na juu ya madai kwamba wapinzani wa mpango huo wanalengwa kuuawa.

Kufungwa kwa Daily Monitor pia kuliathiri vituo viwili vya redio, 90.4 Dembe FM na 93.3 KFM, ambavyo viko ndani ya jengo hilo katika kitongoji cha Namuwonga kilichochopo kwenye mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Wakati magazeti yakifungwa, kulikuwa na maandamano nchi nzima ya kuunga mkono uhuru wa vyombo vya habari. Polisi wa Uganda walijibu mapigo kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwakamata baadhi ya waandamanaji.

Tarehe 26 Mei 2013, rais alikutana na uongozi wa Nation Media Group, kampuni inayomiliki gazeti hilo la Daily Monitor, kujadili suala hilo. Serikali ilitoa taarifa baadaye ikisema kwamba kampuni ya Nation Media Group “ilijutia sana habari iliyosababisha kufungwa kwa gazeti la Monitor na KFM na vituo vya Radio Dembe,” na kwamba ilikuwa imekubali “itachapisha au kutangaza tu habari zile zenye chanzo kinachoeleweka, zimethibitishwa na zenye usahihi.”

Siku tano baadaye, vyumba hivyo vya habari vilifunguliwa na kuruhusiwa tena kuendelea na kazi.

Head Of security at Daily Monitor opens the door after the reopening. Photo from Daily Monitor official Facebook page

Mkuu wa usalama katika ofisi za Daily Monitor akifungua mlango baada ya kuruhusiwa kuendelea na kazi zake. Picha kutoka ukurasa rasmi wa Facebook wa Daily Monitor.

Baada ya vyombo hivyo vya habari kufunguliwa, gazeti la Daily Monitor lilisema katika tahariri kwamba walikuwa na furaha kurudi kwa kuwa hatua ya kufungiwa ilisababisha ugumu wa kwa wafanyakazi, familia, wasambazaji, wauzaji, na wengine wengi. Walisisitiza kuwa uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kama nchi inataka kukua kwa amani.

Hata hivyo, watu wengi bado wanafikiri serikali haikulishughulikia vyema suala hilo na hatua yake ya kuvifungia vyombo vya habari kuliandika historia mbaya kwa mustakabali wa uhuru wa habari nchini Uganda.

Mwandishi habari wa Uganda na mwanablogu Mugumya aliandika kwenye blogu yake kwamba siku 11 ambazo vyumba vya habari vilifungwa zilikuwa ni kipindi cha  giza nene kuwahi  kutokea kwa vyombo vya habari nchini Uganda:

 

Lakini ningependa kuweka mambo kadhaa wazi. Kinyume na walichosema wengi katika mitandao ya kijamii, shughuli zilizofanywa na mashirika kadhaa ya vyombo vya habari hazidhoofishi vyombo vya habari nchini Uganda.

Kuzingirwa kulidhoofisha vyombo vya habari lakini hasara kwa kiasi kikubwa ni ya fedha na sio kifo kabisa.

Hali za kuzingira vyombo vya habari huwa haziui makampuni, bali ni ukosefu wa hali kama hizo na kwa wale walioathirika kushindwa kujifunza.

Nina hakika hakuna chumba cha habari kitapata ugumu wa kupona kifedha kwa haraka kutokana na kadhia hii.

Hatua kama hizo zinazochukuliwa na serikali kwa upande mwingine zinavipa vyombo vya habari uhai mpya, na kamwe hazividhoofishi vyombo vya habari nchini Uganda.

Nimesoma ahadi zote na hakuna kitu ambacho hakikuwa katika sera ya wahariri tayari.

Alibainisha pia:

 

Polisi wana nguvu kupindukia na mahakama ni kama haina nguvu yoyote.

Hili lilikuwa wazi sana wakati magazeti yamefungwa.

Nilichokiona kama kitu cha ajabu sana si hatua ya polisi kuzitia kufuli ofisi zetu.

Sheria ya Polisi inawapa nguvu na mamlaka ya kufanya hivyo.

Nilichoona kuwa cha ajabu sana, tena ajabu sana na kwa kweli cha kusumbua sana ni kwamba polisi wanaweza kutia kufuli eneo la kazi kwa karibu wiki mbili, kufanya msako mkubwa na huku wakikwepa kufungua mashtaka dhidi ya mtu yeyote na kisha kuondoka zao utafikiri hakuna kilichotokea na watu tunaona kama vitendo hivyo vinakubalika katika nchi yetu.

Akitoa maoni kwenye tovuti ya Daily Monitor, Mukiibi Mugerwa alitaka kujua ikiwa gazeti la Daily Monitor lililazimishwa kunyanyua mikono na serikali:

Nimelisoma sakata hili zima na nikiwa mkweli, kwa mara ya kwanza sijaweza kujua ni nini mnajaribu kusema! Hivi kupindisha pindisha ujumbe ni sehemu ya sera mpya ya uhariri?. Hivi mmenyamazishwa na kulazimishwa kunyanyua mikono kiasi kwamba sasa mnaweza tu kuwasiliana na wasomaji wa ujumbe uliofichika?. Mlipaswa kuwa na ujasiri sana na kusema waziwazi “Kwa muda wa siku 11, mchana na usiku, gazeti la Monitor na Serikali tuliangaliana usoni, na ndiyo, Serikali ndiyo iliyopepesa kope”

Msomaji mwingine, Charles Kintu, alionyesha shaka yake:

 

“Tutandelea kutenda haki na kuandika habari kwa usahihi” Nina shaka kama si kwa masharti magumu mliyoyatilia saini.

Kwenye Mtandao Wa Twita, mtumiaji @twsgy aliandika:

@twsgy: nikifikiri kuhusu #mediasiege, #monitor na pepper walitenda kosa la jinai chini ya #officialsecretsAct hivi polisi hawajui vitendo vyao havikubaliki

Sheria ya Siri Rasmi ya mwaka 1964 ni sehemu ya sheria ambayo, pamoja na mambo mengine, huviwia ugumu vyanzo vya habari ndani ya serikali kutoa taarifa kwa waandishi wa habari. Ripoti ya Benki ya Dunia inaonyesha kuwa Sheria ya Siri Rasmi inaleta changamoto kubwa kwa Sheria ya Kupata Habari nchini Uganda.

Swali linabakiwa kuwa, kama mwandishi wa habari wa Uganda Mugumya alivyouliza kwenye blogu yake wakati wa kujadili kufungwa kwa magazeti hayo, “Hivi hii inaweza kuwa ndiyo kawaida mpya nchini Uganda?”

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.