· Mei, 2013

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Mei, 2013

Mfululizo wa Tamthilia ya Runinga ya Nchini Tanzania

  7 Mei 2013

The Team Tanzania (Timu Tanzania) ni mfululizo wa Tamthilia ya Runinga yenye kuzungumzia: […] Bi. Wito, mwalimu mahiri wa somo la uraia, anaigeuza kabisa mitazamo ya vijana makinda watatu anapowauliza maswali mazito mfano “Wewe ni nani”? vijana wale wenye umri wa miaka 16, waliofahamiana vyema tangu wakikua. Katika kuingia katika...

Michoro ya Dar: Sanaa kwa Maendeleo Endelevu

  7 Mei 2013

Dar Sketches (Michoro ya Dar) ni sehemu ya mradi unaoanzia ngazi ya Mtaa jijini Dar Es Salaam, Tanzania ulioanzishwa na msanii na mchoraji Sarah Markes: Ni katika kuenzi urithi wa kitamaduni na wa sanaa ya ubunifu wa majengo kwa jiji la Dar Es Salaam sambamba na juhudi za kukuza uelewa...

TEDXSão Tomé: Mkutano Wanukia São Tomé na Príncipe

Uandikishaji wa awali kwa ajili ya mkutano wa TEDXSão Tomé umezinduliwa rasmi. Mkutano huo una kaulimbiu inayosema “Visiwa Vimeunganishwa : São Tomé + Príncipe = Áfrika Vimeunganishwa na Ulimwengu” na utafanyika tarehe 20 Juni. Wasemaji katika mkutano huo waliothibitishwa ni pamoja: Dynka Amorim, Ismael Sequeira, Profesa Robert Drewes na Aoaní...

Wagombea wa Urais katika Uchaguzi wa Madagaska

  5 Mei 2013

Habari Mpya:  Hapa ni orodha kamili ya wagombea 49 [fr] wanaowania nafasi ya Urais katika uchauzi ujao. Orodha hiyo haina jina la rais wa sasa wa mpito. Siku ya mwisho ya kurudisha fomu kwa ajili ya kugombea Urais katika uchaguzi ujao ilikuwa tarehe 28 Aprili, na inavyoonekana ni wagombea wachache sana...

Ethiopia: Mwanablogu Ahukumiwa Miaka 18 Jela kwa “Kuvunja Katiba”

GV Utetezi  4 Mei 2013

Mnamo Mei 1, Mahakama Kuu ya Ethiopia ilitoa hukumu kali kwa mwandishi aliyeshinda tuzo Eskinder Nega, ambaye sasa atatumikia kifungo cha miaka 18 jela. Mohamed Keita wa Kamati ya Kuwalinda Waandishi anasema, “Kushitakiwa na hatimaye kutiwa hatiani kwa Eskinder na waandishi wengine ni dalili za utawala unaoogopa maoni ya raia wake.”