Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Machi, 2012
India: Gazeti pekee duniani linaloandikwa kwa mkono
Magazeti ya mwanzo yalikuwa yakiandikwa kwa mkono. Inawezekana kwamba hivi sasa gazeti la ‘The Musalman‘ pengine ndiyo pekee lililobaki linaloandikwa kwa mkono ulimwenguni. Gazeti hili linalochapishwa kwa lugha ya Ki-Urdu lilianzishwa mwaka 1927 na Chenab Syed Asmadullah Sahi ambapo hivi sasa linachapishwa kila siku katika jiji la Chennai huko India tangu kuanzishwa kwake.The earliest forms of newspaper were handwritten and now 'The Musalman' probably is the last handwritten newspaper in the world. This Urdu language newspaper was established in 1927 and has been published daily in the Chennai city of India ever since.
Hong Kong: Raia wasema ‘Hapana’ kwa uchaguzi wa meya usio wa kidemokrasi
Kati ya wajumbe wa Kamati ya Kumchagua Kiongozi Mkuu wa Hong Kong wapatao 1,200, wajumbe 689 walimchagua Leung Chun-ying kuwa meya mpya wa jiji la Hong Kong mnamo tarehe 25 Machi. Matokeo yalipotangazwa, maelfu waliandamana ili kupinga jinsi ambavyo Beijing imekuwa ikiuchezea na mchakato wa uchaguzi.
Zambia: Ban Ki-Moon atoa wito kwa taifa kuheshimu haki za mashoga
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliitembelea Zambia mnamo Februari 21; ambapo alilihutubia bunge, alikutana wanasiasa maarufu na kutembelea Maporoko ya Viktoria, hakuna katika haya yaliyogonga vichwa vya habari kama mwito wake wa taifa hili kuheshimu haki za mashoga.
Dondoo za Video: Utetezi wa haki za binadamu
Kuna masimulizi kusisimua katika siku za hivi karibuni kwenye tovuti ya Global Voices Video za Utetezi ikiwa ni pamoja na haki za wananchi wenyeji na habari za hivi karibuni kutoka Amerika ya Kusini, Mashariki ya Mbali, Ulaya Magharibi na Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara zilizochaguliwa na Juliana Rincón Parra.
Iran: Wanawake wapinga ‘Jinamizi la Vita’
Utawala wa Kiislamu wa Iran umepuuza Siku ya Wanawake Duniani kwa zaidi ya miongo mitatu. Utawala huo hauitambui siku ya Machi 8, na umepiga marufuku mashirika ya wanawake kusherehekea siku hiyo. Lakini kila mwaka wanawake wa ki-Iran iwe kwa uwazi ama kificho bado wanasherehekea siku yao hiyo.
Korea Kusini: Wahudumu wa ndege wapigania haki ya kuvaa suruali
Katika Siku ya Wanawake Duniani, wahudumu wa moja ya mashirika makubwa ya ndege nchini Korea Kusini, waliitisha mkutano na waandishi wa habari mbele ya makao makuu ya shirika lao la ndege kudai haki ya kuvaa suruali. Madai hayo yamepata uungwaji mkono mkubwa sana na watumiaji wa mtandao wa nchini humo.
Palestina: Gaza yashambuliwa, watu 12 wauwawa na wengine wengi kujeruhiwa
Usiku kucha wa tarehe 9 Machi na asubuhi ya Machi 10, ndege za kivita za Israel zilishambulia maeneo maalumu katika Ukanda wa Gaza, na kuua takribani watu 12 na kujeruhi wengine 20.
Iran: Wachora katuni ‘wamkalia kooni’ Khatami kwa kupiga kura
Mohammad Khatami, aliyekuwa Rais mwanamageuzi wa Irani, Ijumaa ya tarehe 2 Machi, 2012 alipiga kura katika uchaguzi wa wabunge. Kitendo hicho kilikinzana na kauli aliyopata kutoa siku za nyuma kwamba angegomea kupiga kura hadi wafungwa wote wa kisiasa waachiwe huru na katiba kuheshimiwa. Kitendo chake hicho kimezua shutuma nyingi kutoka kwa wanamageuzi walio makini katika kugomea uchaguzi huo.
Amerika Kusini: Waathirika wa ‘biashara’ ya kukuza matiti waingia mtandaoni
Wanawake wengi wameungana kwenye tovuti za kijamii kusema wanachofikiri na kubadilishana taarifa kuhusu matatizo yanayosababishwa na viini vya kukuzia matiti. Wakati huohuo wanapanga hatua gani za kisheria wachukue. Kumekuwa na ongezeko kubwa la ugonjwa wa saratani huko Amerika ya Kusini. Je, ni kina nani hawa wanaopaaza sauti zao barani humo? Fuatilia ...
Baada ya Kony 2012, “What I Love About Africa” Yanyakua Mazungumzo
Kampeni katika mtandao kuhusu mhalifu wa kivita Joseph Kony umesababisha utata mkubwa barani Afrika. Kampeni nyingine ya kupinga utata huo na kuonyesha upande bora wa bara la Afrika, unaojulikana kama #WhatILoveAboutAfrica (Nini Ninachopenda Kuhusu Afrika) sasa unaenea katika tovuti la Twitter.