Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Februari, 2010
Chile: Tetemeko Kubwa la Ardhi lenye Ukubwa wa 8.8 Laikumba Chile
Saa 9:34 usiku kwa saa za Chile, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 8.8 liliukumba mwambao wa eneo la Maule nchini Chile. Tetemeko hilo liliutetemesha mji mkuu wa Santiago uliopo Kilomita 325 kutoka katika kiini cha tetemeko hilo. Uharibifu mkubwa umeripotiwa nchin nzima, na idadi ya waliofariki inazidi kwenda juu.
Nijeria: Baada ya miezi miwili bila uongozi, kaimu Rais mpya
Baada ya wiki za mivutano ya kisiasa, Baraza la Seneti lilimthibitisha Goodluck Jonathan kama kaimu Rais. Wengi kwenye ulimwengu wa blogu waliliona tukio hilo kama sababu ya kusherehekea… lakini wengine waliliona kama jambo la kutia hofu, wakieleza kwamba japokuwa kutwaa madaraka kwa Jonathan kunaweza kuwa ni ulazima wa kisiasa, kutwaa huko hakujaruhusiwa wazi na katiba ya Naijeria.
Lebanon: wanablogu washinikiza jarida la Daily Star kubadilika
Wanablogu wa Lebanon wanapiga kampeni ya kwenye mtandao ili kulishinikiza gazeti pekee la kwenye wavuti kurekebisha tovuti yake. Mwanablogu mmoja amefanya jitihada kubuni tovuti ya kuiga - ambayo wenzake wanatumaini itahimiza mabadiliko katika gazeti la Daily Star, na kuibadili 'boti moshi ya Kirusi ya miaka ya 1920' kuwa meli ya karne ya 21 ya abiria.
Kadri Liberia inavyotulia, vijana waanza kuzungumzia ngono
Kadri Liberia inavyoendelea kutoka kwenye vita ya kutisha ya wenyewe kwa wenyewe, wengi wanahofu mchanganyiko wa umaskini uliokithiri na maamuzi yenye hatari ya ngono vitaongeza kiwango cha VVU/UKIMWI na idadi ya mimba zisizotarajiwa.
Ethiopia: Wanablogu walitetea Shirika la Ndege la Ethiopia baada ya ajali ya ndege
Wanablogu waishio Ethiopia wameharakia kuitetea rekodi ya usalama wa safari za ndege za nchi hiyo siku ya Jumatatu baada ya ndege moja kuanguka karibu na Beirut, ikihofiwa kupoteza maisha ya watu wote 90 waliokuwepo.
Ghana: Mkuu wa Mkoa, Kofi Opoku-Manu, Anapoteza Umaarufu?
Mkuu wa Mkoa wa Ashanti, Kofi Opoku-Manu, hivi karibuni alionja joto ya jiwe kutokana na matamshi aliyoyatoa kwenye hotuba yake kwa mashabiki wa chama tawala, Nationa Democratic Congress (NDC) tarehe 6 Januari. Kwa mujibu wa Ato-Kwemena Dadzie, Opoku-Manu “aliwasihi mashabiki wa chama kutumia ghasia kusuluhisha tofauti zao.”
Misri: Mwanablogu apoteza kazi kwa kufichua ukweli kuhusu habari ya bikra za bandia
Mwanablogu ambaye pia ni mwanahabari wa Kimisri Amira Al Tahawi amefukuzwa kazi kwa kufichua ukweli kuhusu habari ya uongo juu ya bikra za bandia zinazotengenezwa China katika makala alioyoichapa kwenye yake, ndivyo wanavyodai wanablogu. Yafuatayo ni baadhi ya maoni kutoka kwenye ulimwengu wa blogu za Kimisri kuhusu kisa hicho.
Haiti: Kwa Nini Habari Zote Hizi Kuhusu Yatima?
Mwezi mmoja baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa poiti saba kuangamiza sehemu kubwa ya Haiti ya kusini, mustakabali wa watoto, na hasa hasa yatima, umekuwa ni habari kubwa katika kona mbalimbali. Lakini sauti za Wahaiti kwenye mada husika zimekuwa chache...
Je, Ghana Ipo Tayari kwa Upigaji Kura wa Kwenye Mtandao?
Tukio la siku mbili lililoanza jana; linaratibiwa na Danquah Instite (DI), kituo cha kutafakari sera, utafiti na uchambuzi, kutengeneza jukwaa la kitaifa kwa washikadau kuongoza majadiliano kuhusu uwezekano wa uanzishwaji wa kuandikisha wapiga kura kwa njia za vipimo vya kibaiolojia na hatimaye mfumo wa upigaji kura kwa njia ya mtandao nchini Ghana.
Upinzani Waongezeka dhidi ya Mapendekezo ya Tanzania na Zambia katika Makubaliano ya CITES
Upinzani unaongezeka dhidi ya mapendekezo ya Zambia na Tanzania ya kuruhusiwa na Makubaliano ya Biashara ya Kimataifa ya Makundi ya Mimea na Wanyama Walio Katika Hatari ya Kutoweka (CITES), kuuza hifadhi ya pembe za ndovu walizonazo.