· Julai, 2013

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Julai, 2013

Hali ya Uislamu Katika Asia ya Kusini

  27 Julai 2013

Murray Hunter wa Chuo Kikuu cha Malaysia Perlis anajadili hali ya jamii ya Kiislamu katika Asia ya Kusini pamoja na masuala yanayohusiana na kukua kwa Uislamu katika eneo hilo. Umaskini, kujua kusoma na kuandika, elimu, kuhamishwa, ukabaila, ukosefu wa ajira, ukandamizaji, na udhibiti ni mambo yanayowaonea Waislamu ndani ya ASEAN. Serikali pamoja na...

Barua ya Wazi ya Kushinikiza Kuachiwa Huru kwa Mwanasheria

  24 Julai 2013

Mnamo Julai 23, 2013, zaidi ya raia 400 wa China wamesaini barua ya kushinikiza serikali ya China kumuachia huru Xu Zhiyong, ambaye ni mwanasheria mashuhuri na mpigania haki aliyekamatwa mnamo Julai 16 baada ya kushinikiza kuachiwa kwa wanaharakati pamoja na kuratibu kampeni dhidi ya uovu unaofanywa na serikali. MRADI WA...

Maandamano ya Kudai Uchaguzi nchini Madagaska Yasababisha Vurugu

Blogu ya Vola R ya Ma-Laza inaandika kwamba watu 7 walijeruhiwa [fr] kufuatia matumizi ya nguvu yaliyofanywa na polisi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wanadai kufanyika kwa uchaguzi mjini Antananarivo, Madagaska. Chama kinachoongoza maandamano kinasema kwamba utawala uliopo hauna dhamira ya kuitisha uchaguzi mwaka huu na kwamba serikali imeng'ang'ania madarakani. Kiongozi wa...

Mwana-Habari Menna Alaa Ashambuliwa na Wafuasi wa Morsi

Mwanablogu na mwanahabari wa video Menna Alaa leo hii ameshambuliwa na waandamanaji wenye hasira wanaomwunga mkono Morsi. Mwanablogu huyo ameweka ushuhuda wake kwa lugha ya kiingereza kwenye makala hii iliyo katika blogu inayokusanya matukio nchini Misri iitwayo Egyptian Chronicles. Anaandika: Kofi nililopigwa usoni, alama iliyobaki usoni mwangu pamoja na kuibwa...

Peru: Mchezaji wa Kandanda Afariki Dunia Uwanjani

  22 Julai 2013

Dakika tano kabla ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu zaReal Garcilaso na Sporting Cristal, mchezaji nyota wa timu ya Sporting Cristal mwenye miaka 18 Yair José Clavijo alipata mshituko wa moyo na akapoteza maisha. Madaktari wa timu hiyo walijaribu bila mafanikio kunusuru hali yake akiwa kwenye sehemu ya kuchezea...

Shindano la Wanablogu wa Kiafrika wenye Fikra Pevu.

Mtandao wa Africa Brains watangaza Shindano la Wanablogu wa Kiafrika Wenye Fikra Pevu watakaowania kitita cha dola Hamsini ($50). Ni muda muafaka wa kutangaza mada ya kwanza, ambayo ni “Teknolojia imekuwa na ushawishi gani katika elimu yako?” Tufahamishe hali ya upatikanaji wa teknolojia ulipokuwa shuleni au chuoni? Tangu uanze kutumia...

India: Chakula Chenye Sumu Chaua Watoto 24

  18 Julai 2013

Chakula kilichoua wanafunnzi na kuwaacha wengine katika hali mbaya kinasadikiwa kuwa kilichanganyikana na dawa ya kuulia wadudu. Tukio hili linaibua maswali kuhusiana na ubora wa chakula cha mchana wanachopewa wanafunzi wanaotoka katika familia masikini.