· Julai, 2012

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Julai, 2012

Tanzania: Mgomo wa Walimu Watikisa Nchi

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika zoezi la sensa, walimu nchini Tanzania wako katika mgomo kuishinikiza serikali kuwalipa madai yao pamoja na kuboresha mishahara yao. Hatua hiyo imevuta hisia za watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wanaojadili madhara ya mgomo huo.

Tamko la Uhuru wa Mtandao wa Intaneti

GV Utetezi  26 Julai 2012

Hivi karibuni, makundi kadhaa yameungana pamoja kutengeneza Tamko la Uhuru wa Mtandaoni. Mpaka sasa, Tamko hilo limesainiwa na mashirika na kampuni zipatazo 1300 na bado zoezi linaendelea kukua.

Ethiopia: Maandamano ya Waislamu Yashika Kasi

Jeshi la Polisi nchini Ethiopia waliamua kutumia nguvu kupambana na wanaharakati wa ki-Islamu, likituhumiwa kufanya vitendo haramu katika maeneo yanayochukuliwa kuwa matakatifu katika misikiti, kwa mujibu wa habari zilizoandikwa na ukurasa wa kikundi cha waislam katika mtandao wa Facebook uitwao Dimtsachin Yisema (Iache Sauti Yetu Isikike). Tangu mwezi Mei, Wa-Islamu wa ki-Ethiopia wamekuwa wakiandamana kupinga serikali kuingilia mambo yao ya kidini.

Paraguai: Kutoka Kutumikishwa Hadi Kuwa Kiongozi Mzawa.

Sauti Chipukizi  21 Julai 2012

Kutana na Margarita Mbywangi, ambaye katika umri wa miaka mitano, alichukuliwa kutoka kwa wazazi wake na kuuzwa mara kadhaa na kulazimishwa kufanya kazi za nyumbani. Tangu wakati huo amekuwa kiongozi muhimu wa kabila la Aché na hata kuwa Waziri katika nchi yake. Mbywangi sasa anasimulia maisha yake binafsi kupitia Mradi wa Rising Voices.