· Machi, 2010

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Machi, 2010

Thailand: Utulivu Kabla ya Kimbunga?

  14 Machi 2010

Maandanmano ya kuipinga serikali ya Machi 12 yalimalika salama huku kundi la Mashati Mekundu likiapa kurejea tena mitaani mwishoni maw juma hili ili kuendelea kushinikiza kuvunjwa kwa bunge na kuitisha uchaguzi mkuu. Wanablogu na watumiaji wa Twita wanatoa maoni yao.

Naijeria: Ghasia Zalipuka Huko Jos Kwa Mara Nyingine

Huko Jos, machafuko yanaelekea kujitokeza katika mizunguko inayozidi kuwa midogo: machafuko mabaya yaliukumba mji huo mwaka 1994, 2001, 2008, na – hata miezi miwili iliyopita – mnamo mwezi Januari 2010. Mgogoro wa sasa unasemekana kuwa ulianza katika tukio la kisasi kilichotokana na uharibifu uliotokea mwezi Januari, na, kama ilivyokuwa kwenye machafuko yaliyopita, mapambano ya sasa huko Jos yamekuwa yakipiginwa katika misingi ya kidini.