· Disemba, 2012

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Disemba, 2012

Habari za Upotoshaji Kuhusu Afrika Katika Vyombo vya Habari vya Kimataifa

 Kampeni ya kumkamata #Kony2012 ilibeba mambo yaliyorahisishwa mno kuhusu Afrika. Vyombo vya habari vya Afrika vyenyewe, hata hivyo, kwa sasa havina kinga dhidi ya ukosoaji wa aina hii. Hapa ni muhtasari wa watu maarufu, makosa na kutokuwepo umakini katika habari zinazopewa nafasi katika vyombo vya habari vya dunia kuhusu Afrika na katika vyombo vya habari vya Afrika vyenyewe

Mwandishi wa Guinea Atoweka Kiajabu nchini Angola

Yuko wapi Milocas Pereira? Swali hili linarudiwa rudiwa kupitia blogu mbalimbali kwa majuma kadhaa sasa, lakini majibu yamekuwa vigumu kupatikana. Katika mitandao ya kijamii harakati zililipuka kuzishinikiza mamlaka za nchi ya Guinea kuchunguza mazingira ya kupotea kwa mwandishi huyo na mhadhiri wa Chuo Kikuu miezi sita liyopita katika jiji la Luanda, alikokuwa akiishi tangu mwaka 2004.

Kenya: Kufundisha Uvumilivu wa Kikabila Kupitia Hadithi za Sayansi

30 Disemba 2012

Watoto wa Kenya wanafundishwa uvumilivu wa kikabila kupitia hadithi za sayansi: “Kushambuliwa kwa akina Shida:Bunduki za AKA Zaokoa Sayari” ni hadithi inayozungumzia maisha ya jamii tatu zilizoishi katika jangwa katika mji fulani ambazo zilitegemea kisima kupata maji. Lakini wenyeji wanatishika pale wanapogundua kuwa maji wanayoyategemea yanamwagwa kimiujiza usiku.” “Watoto watatu...

Video ya Kuomba Ujenzi wa Vyoo vya Umma huko Jharkhand, India

  30 Disemba 2012

Amit Topno, mwakilishi wa jumuiya ya hiari “inayopiga picha za video” aliripoti kwamba wakati wa kijiji cha Nichitpur katika Jimbo la Jharkhand hawana choo chochote cha umma kinachotumika. Wanavijiji wanaziomba mamlaka za serikali za mitaa kupitia video hii kuhakikisha kuwa vyoo vinavyostahili matumizi ya binadamu vinajengwa.

China Inaelekea Wapi kwa Mwaka 2013?

  29 Disemba 2012

Kadri mwaka wa 2012 unavyosogea karibu, jarida la CHINA DIGITAL TIMES limetoa muhtasari wa mabadiliko na changamoto zinazoikabili China mwaka 2013 kwa kutumia taarifa na bashiri mbalimbali za vyombo vya habari.

Matajiri Wakubwa China na Marekani Walinganishwa

29 Disemba 2012

Liz Carter kutoka tovuti ya Tea Leaf Nation (Taifa la Jani la Chai) alitafsiri taarifa ya picha ya tovuti ya CN politics [zh] (CN siasa), inayojaribu kulinganisha tabia za matajiri wa ki-China na ki-Marekani.

Assad atumia Ndege ya Kivita Kuwaua Raia Wake

Serikali ya Syria imefanya shambulizi kubwa la angani dhidi ya raia wa nchi hiyo -waliokuwa wamesimama kwenye foleni waisubiri mikate kwenye kiwanda cha kuokea miakte huko Halfaya, Hama. Inakadiriwa kwamba watu waliouawa katika shambulio hilo mjini humo ni kati ya 90 na 300, waasi wakisema kuwa watu hao walikuwa wamejitenga na vikosi vya Assad. Mtandaoni, wanaharakati wanashangazwa inakuwaje dunia inaendelea kutazama tu maisha ya watu wasio na hatia wakiuawa kwa mamia.