India: Chakula Chenye Sumu Chaua Watoto 24

Mnamo tarehe 16 Julai, 2013, watoto 22 walio na umri kati ya miaka minne na 12 katika shule moja ya msingi ya serikali katika jimbo la Bihar nchini India, walipoteza maisha mara baada ya kula chakula cha mchana kinachoamikiwa kuwa kilikuwa na sumu.

Wengi wao wakiwa ni wakazi wa kijiji masikini cha Chapra, walilazwa hospitalini kufuatia hali zao kuwa mbaya sana. Chakula walichokula kinaaminika kuwa kilikuwa na dawa ya kuulia wadudu.

Janga hili limekuwa tukio baya kabisa lililotokana na uzembe wa wazi kwa chakula cha mchana cha wanafunzi hao kuchanganyikana na sumu. Katika tukio lingine huko Bihar katika wilaya ya Madhubani, wanafunzi 15 waliugua mara baada ya kula chakula cha mchana. Huko Gaya-Bihar, mwanafunzi mmoja alipoteza maisha baada ya kula chakula cha mchana. Na katika tukio jingine huko Dhule katika wilaya ya Maharashtra, watoto 31 walilazwa hospitalini mara baada ya kupata chakula cha mchana.

A student a government funded Hindi school in Mumbai, India (Photo: Chirag Sutar)

Mwanafunzi wa shule ya Kihindi inayofadhiliwa na serikali nje kidogo ya Mumbai, India, 2012. Picha na mwandishi wa makala hii.

Utaratibu wa chakula cha mchana, ulioanza miaka ya 1960, ni miongoni mwa taratibu za siku nyingi sana nchini India ulio na lengo la kuwapa moyo familia masikini kuwapeleka watoto wao shuleni. Mbali na elimu, kutolewa kwa chakula kwa kila mwanafunzi, imekuwa kama hamasa kwa ajili ya kuwavutia wanafunzi kuandikishwa mashuleni. Hata hivyo, tangu kuanza kwa utaratibu huu, kumekuwa na taarifa za wazi za ubadhirifu wa chakula kilichokusudiwa kwa wanafunzi. Kwa mujibu wa taarifa za habari za mwaka 2006, ilionekana kuwa, wanafunzi wa shule za misingi za Darjeeling walikabiliana na upungufu wa chakula kwa muda wa miezi 18.

Kama ilivyotarajiwa, jambo hili limechukuliwa kisiasa. Chama kilichopo madarakani kilidai kuwa upinzani umejihusisha katika njama za kuwateka watu kimtizamo. Mume wa mkuu wa shule anaelezwa kuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa na ndiye aliyekuwa msambazaji wa chakula shuleni hapo.

Serikali kushindwa kutilia mkazo tukio hili, umewaghadhabisha watu wengi katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Mtumiaji wa Twita aliye na makazi yake nchini India, Vikram Singh (@cynicalvs) aliandika:

@cynicalvs: watoto wanawezaje kufariki baada ya kula chakula cha mchana? Ni chakula. Kunamtu anapaswa kushitakiwa kwa kosa la mauaji. #chappra

Mara baada ya waandishi wa habari kuanza kutembea mahospitalini kwa ajili ya kutoa taarifa za tukio hili, matumizi mabaya ya madaraka yaliendelea kujitokeza. Picha katika mfumo wa video za mtandaoni ziliwaonesha watoto walionusurika wakiwa mamelala kila mmoja karibu na mwenzakeAs soon as journalists began reaching hospitals to report on the situation, more mismanagement came to surface. The streamed video images showed surviving children laid next to each other kwa kubanana kwenye dawati huku wakigawiwa maji ambayo ni myeyusho wa chumvi na maji.

Milind Khandekar, ambaye ni mhariri mkuu wa kampuni ya uhabarishaji ya the managing editor of ABP News (@milindkhandekar), alitoa maoni yake:

@milindkhandekar: picha kutoka Chappra zinawaonesha ndugu wa watoto waliolazwa hospitali wakiwapepea watoto wao kwa makaratasi. Huu ndio ‘mfano mzuri wa maendeleo ya Bihar’?

Mapema kabisa, tukio hili liliwapelekea watumiaji wa mitandao ya kijamii kujadili hali ya dharau na kiburi iliyooneshwa na wanasiasa wa India.

Abhijit Majumder, ambaye ni mwandishi wa habari kutoka Delhi (@abhijitmajumder), alitwiti:

@abhijitmajumder: Wanasiasa wetu hawabagui. 2G kwa wale wanaojiweza au NREGA, chakula cha adhuhuri kwa mafukara, wote wanadanganywa kwa mvuto sawa. #Chhapra

Students of a Hindi school in Mumbai eat on ground with seating arrangement or provision of plates.

Wanafunzi wa shule ya Kihindi nje kidogo ya Mumbai wakipata chakula wakiwa wamekaa chini pasipo kuwa na viti wala bakuli. Mwanafunzi mwingine akionesha kibobo chenye chakula cha adhuhuri huku akilalamika kuhusu ubora wa chakula hicho. 2012. Picha na Mwandishi wa makala hii.

Majumder, alirejelea matukio ya udanganyifu yaliyotokea hivi karibuni, kama yale ya2G na NREGA, ambayo yaligharimu mabilioni ya dola na kupandikiza hali ya kukosa imani kubwa kwa namna serikali ya India inavyotimiza majukumu yake.

Mwandishi mwingine wa habari ambaye makazi yake ni Delhi, Raghavendra Verma (@r_verma), alitoa maoni yake kuhusu namna ambavyo walimu wanavyozichukulia shule zinazomilikiwa na serikali.:

@r_verma: walimu huwapatia watoto chakula cha adhuhuri kana kwamba wamejitolea sana na kwa upendeleo mkubwa. #Chhapra

Fazal Abbas (@fazlabas), ambaye ni mtumiaji wa Twita aishiye Mumbai, alitoa historia kuhusiana na tukio hili:

@fazlabas: Chhapra ni kama ilivyokuwa kwa Rais wetu wa kwanza Dk. Rajendra Prasad aliyefariki miaka 50 iliyopita. Watoto wanafariki kwa ajili ya elimu.

Kiran Bedi (@thekiranbedi), ambaye ni askari mstaafu kutoka Delhi, ambaye anajulikana kwa utendaji kazi uliotukuka na mmoja wa wapinga rushwa nchini India, alitwiti:

@thekiranbedi: Mlo wa adhuhuri, ni wenye majungu na usio katika hali ya usafi. Pia, walimu wanapoteza tu muda wao kupika chakula hicho! Kwa nini wasiwagawie matunda na njugu?

Maelezo ya Bedi yanaunga mkono ushahidi wa picha uliotangulia kutolewa. Sio tu Bihar, miongoni mwa shule zinazomilikiwa na serikali nchini India zilizoweza kuwa na mengi ya kujadiliwa kuhusiana na kutotilia maanani mambo na usimamizi mbovu. Kwa jinsi shauri hili lilivyo, serikali ya India ilipaswa haraka sana itangaze fidia ya lakhs 2 (takribani dola za kimarekani 3,367) kwa familia za wahanga.

Uchunguzi wa ni kwa namna gani chakula hiki kilichanganyika na sumu bado unaendelea-kwa ufupi, mchakato mrefu wa kiuchunguzi unafuata. Je, waliohusika watawajibishwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.