· Julai, 2013

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Julai, 2013

Maandamano Yasitisha Ujenzi wa Mtambo wa Nyuklia Kusini mwa China

  16 Julai 2013

Kufuatia siku tatu mfululizo za maandamano, inaonekana kuwa serikali ya Manispaa ya Heshan katika jiji la Jiangmen imesitisha mpango wake wa ujenzi wa mtambo mkubwa wa nishati ya Nyuklia. Baadhi ya watu wanaamini kuwa ushindi huu ni wa muda mfupi tu. Wana wasiwasi kuwa, mradi huu unaweza kuibukia sehemu nyingine karibu na Delta ya mto Pearl, Kusini mwa China mahali palipo na idadi kubwa sana ya watu.

Al Jazeera Yatuhumiwa Kutangaza “Habari za Upendeleo”

Al Jazeera iko kwenye wakati mgumu nchini Misri kwa kile kinachoelezwa na wengi kuwa ni "upendeleo" wake katika kutangaza habari zake wakati na baada ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi mnamo Julai 4. Kituo hicho cha televisheni kilichopo nchini Qatar kinatuhumiwa kuegemea upande wa wafuasi wa Muslim Brotherhood na kimegeuka kuwa mdomo wa kikundi hicho.

Kuelekea uchaguzi wa Kambodia: Matumizi ya Mtandao wa Facebook

  12 Julai 2013

Watumiaji wa mtandao wa intaneti nchini Cambodia wanatumia mtandao wa Facebook kwa kiwango kikubwa katika kujadili, kuendesha midahalo na kushirikishana mambo mapya yanayohusu chaguzi za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika tarehe 28 Julai, 2013. Wakati huohuo, vyama vya siasa pia vinatumia mtandao huu ulio maarufu zaidi katika kuwashawishi vijana wadogo wanaotarajiwa kupiga kura.

Saudi Arabia: Familia za Wanaoshikiliwa Gerezani Zaandamana

10 Julai 2013

Familia za watu wa Saudi Arabia wanaoshikiliwa gerezani yaingia siku ya tatu ya kupinga kushikiliwa kwa wapendwa wao bila sababu maalum. Saudi Arabia ni moja ya nchi chache duniani ambazo bado zipo chini ya mfumo wa utawala wa kifalme na ina rekodi isiyoridhisha kuhusu haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kushikilia gerezani zaidi ya watu 30,000 bila sababu maalum.

Global Voices Yazindua Ushirikiano na Shirika la NACLA

10 Julai 2013

Global Voices na Shirika la Marekani Kaskazini Linaloshughulika na Amerika Kusini (NACLA) wameanzisha ushirikiano mpya ambao utaleta kwa pamoja dira ya Sauti za Dunia ya habari za kiraia na na ile ya NACLA ya uchunguzi na utoaji wa elimu, lengo likiwa ni kuwaletea wasomaji wetu habari halisi na za kina kutoka katika eneo hili la Latini Amerika.