· Oktoba, 2008

Habari kuhusu Uandishi wa Habari za Kiraia kutoka Oktoba, 2008

Bahrain: Raha na Karaha za Kusoma Ng'ambo

  26 Oktoba 2008

Ingawa Bahrain ina idadi kadhaa ya vyuo vikuu, vya umma na binafsi, raia wengi wa nchi hiyo hupata fursa ya kwenda ng'ambo kwa masomo ya shahada ya kwanza na hata zile za juu, mara nyingi kwa kutegemea ufadhili. Moja ya matatizo ya kwanza wanayokumbana nayo huko ughaibuni ni kwamba watu wachache tu hufahamu ni wapi Bahrain ilipo. Katika makala hii tunafuatilia uzoefu wa wanablogu watatu ambao ndiyo kwanza wamekwenda ng'ambo kwa masomo: kule Japan, Uingereza na Marekani na mwanablogu wa nne ambaye anasoma India kwa kipindi fulani hivi sasa.

Misri: Sisi sote ni Laila

  26 Oktoba 2008

Sisi sote ni Laila, ndivyo wanavyosikika kusema kwa sauti moja wanablogu wa kike wa Misri. Hivi, huyu Laila ni nani na kwa nini wasichana na wanawake wa kiMisri wanapenda kufananishwa naye? Hebu endelea kusoma ili uone ni kwa namna gani wanablogu wa Misri wanavyojihangaisha ili kuvunjilia mbali vikwazo vya jinsia na kufanya sauti zao zisikike.

Macho ya Kimataifa kwenye Uchaguzi wa Marekani

Kadiri uchaguzi wa Marekani unavyokaribia, ndivyo kadiri macho ya kimataifa yanavyozidi kuelekezwa katika sera za nje za taifa hilo na wagombea wake wakuu. Kazimiradi kama vile ile ya Collective Journalism inayofanywa na Current TV (Uandishi wa Habari wa Umma wa Current TV) na Global Voices' Voices Without Votes (Mradi wa Global Voices - Sauti Zisizo na Kura) zimechukua jukumu la kukusanya taarifa na kuzipa mtazamo wa kimataifa katika masuala ya ndani ya sehemu fulani tu ulimwenguni.

Mwangwi wa Sakata la Maziwa China katika Afrika

Nchini China inakadiriwa kuwa watoto 13,000 wameugua tangu sakata la maziwa yasiyofaa kuibuka. Ushawishi na nguvu za China vimeongezeka Afrika, kama ulivyoongezeka uagizwaji wa bidhaa za kila namna, kuanzia viatu vya mazoezi mpaka chakula aina ya tambi. Mabloga hata wale walio mbali kama Kongo au Senegal, wanaguswa na usalama wa bidhaa za kutoka China katika nchi zao, na wanafuatilias habari hiyo (ya maziwa yasiyofaa).