Macho ya Kimataifa kwenye Uchaguzi wa Marekani

Kadiri uchaguzi wa Marekani unavyokaribia, ndivyo kadiri macho ya kimataifa yanavyozidi kuelekezwa katika sera za nje za taifa hilo na wagombea wakuu. Kazimiradi kama vile ile ya Collective Journalism inayofanywa na Current TV (Uandishi wa Habari wa Umma wa Current TV) na Global Voices’ Voices Without Votes (Mradi wa Global Voices – Sauti Zisizo na Kura) zimechukua jukumu la kukusanya taarifa na kuzipa mtazamo wa kimataifa katika masuala ya ndani ya sehemu fulani tu ulimwenguni.

Programu ya Collective Journalism inayorushwa na Current TV imeanzisha mfululizo wa ripoti za video zinaoonyesha maoni ya watu wengine ulimwenguni kuhusu Marekani. Katika programu ya The View from Over There (Mtazamo Kutoka Kwingineko) watu kutoka mataifa mbalimbali wanatoa maoni yao kuhusu sera ya nje, vita vya Iraki, hali tete juu ya Irani na kumtaja ni nani wangependa awe rais anayefuata wa Marekani. Mahojiano hayo ya video mara nyingine huwa katika lugha mbalimbali, lakini hewekewa tafsiri zake katika Kiingereza.

Video hii pia inatumia vipande vya video vinavyoonyesha Uchaguzi wa Marekani 2008, lakini hasa vile vinavyokazia mtazamo wa kigeni. Hili ni jambo moja ambalo Global Voices na Shirika la Reuters wamekuwa wakifanya kwa kitambo fulani kupitia programu ya Voices Without Votes: kwa kukusanya maoni kutoka pande zote za ulimwengu juu ya uchaguzi wa Marekani. Kama kuna taarifa ungependa kutuma kwenye programu hii, unaweza kufanya hivyo hapa.

Programu ifuatayo ya Collective Journalism inayotolewa na Current TV katika kazi zake itakuwa ni mtazamo wa dunia nzima juu ya sera za Marekani za uhamiaji.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.